Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Huyo jaama wala haelewi arguments kama hizi. Unajisumbua tu.
Hahaaa unadandia hoja za mwenzio za kwako ziko wapi?!

Nimekuuliza maswali mawili madogo tu umeishia kurusha mateke tu hapa, tulia soma wenzio.
 
Utakuwa wa jinsia ya Ke wewe. Tabia yako imenifanya nianze kufikiria kuhusu jinsia yako.
Hahaaa unadandia hoja za mwenzio za kwako ziko wapi?!

Nimekuuliza maswaki mawili madogo tu umeishia kurusha mateke tu hapa, tulia soma wenzio.
 
Maswali yako ni ya kitoto kabisa (sorry). Endelea kuamini kuwa Aida anaweza kupata Tume huru yeye mwenyewe Bungeni. Sana sana anakwenda kuhalalisha udhalimu uliofanyika. Ndio maana CCM wanataka aende.
Hili ndio jibu la hayo maswali?!

Ushafeli.
 
Utakuwa wa jinsia ya Ke wewe. Tabia yako imenifanya nianze kufikiria kuhusu jinsia yako.
You pretend uko vizuri upstairs but nothing. Unaruka ruka tu. Gud day.

Hua sipanikishwi niropoke upuuzi kwa sababu ya mjinga kama wewe, bye.
 
Tangu lini chadema ikaushauriwa? Watu walishauri hapa kuhusu kubadili gear ila hawakumsikia mtu walifanya vile watakavyo na nyie mkaishia kuuunga mkono na hiyo ndio nafasi yenu kushabikia sio kushauri au kukosoa.

Vyama vyetu ndio viko hivyo.
 
Mkubwa naomba kwanza uelewe, Chadema sio chama binafsi, ama chama cha mtu, Chadema is apublic institution. Na inaendeshea kwa mujibu wa katiba ya Nchi hii.
2) Chadema haina Mbunge na wala Haijawa kuwa na wabunge wake. Ila Chadema imekwisha toa kama chama kwa wanachama wake wawe kwenye bunge la taifa (Member of National Assembly)

Chadema au chama chochote hata CCM ni njia tuu ya kukufika mtanzania Mjengoni.
 
Ingawa naelewa unakotokea lakini kwenye hili natofautiana na wewe. Mimi nadhani kuwa kuna umuhimu wa Chadema kuwepo Bungeni kwa sababu zifuatazo:

1. Ingawa tutaliita kuwa ni Bunge la CCM lakini ukweli ni kuwa ni Bunge la taifa la Tanzania lenye wajumbe wengi kutoka CCM. Kwa sababu hiyo kuna haja ya uwepo wa wajumbe wataowatetea wananchi na kusimamia taifa lao.

2. Kuingia kwenye Bunge sio ishara kuwa wamekubali matokeo ya uchaguzi. Wao wanaweza kusema kuwa wanaingia under protest. Watakapoapa hawataapia CCM au NEC bali wataapia Katiba ya taifa lao la Tanzania.

3. Wakiwa Bungeni watakuwa na nafasi nzuri ya kuwatetea na kuwasemea kwa Mamlaka wale wote ambao kwa namna moja ya nyingine wataona kuwa hawajatendewa haki na serikali.

4. Watapata nafasi ya kuwakumbusha wananchi na serikali kuwa kuna wanachama wao, wafuasi wao na watu wengine ambao wako ndani kwa kesi ambazo hazina mashiko. Wataweza tena kuikumbusha serikali kuwa majibu bado yanahitajika kuhusu wale ambao wamepotea katika mazingira potofu.

5. Wakiwemo watampa ujasiri mbunge mwenzao wa Nkasi ambae kuweza kuwasemea watu wake. Ingawa inabidi wamuangalie vizuri kwa sababu kuna uwezekano wa yeye kuhamia upande wa pili.

6. Wakiwa wabunge wa viti maalum wasio na majimbo watapata fursa kuwasimamia wabunge waliotoka katika maeneo yao na kuwakumbusha wananchi kuhusu ahadi zao. Halima anaweza kumuuliza kila siku Askofu kuhusu maendeleo ya chuo cha uvuvi na safari za kwenda Marekani.

7. Wabunge watakuwa huru zaidi kusimamia masuala ya kitaifa bila kuathirika sana na wao kutokuwepo majimboni mwao.

8. Chadema inahitaji pesa za kujiendesha. Ruzukuwatakayopata itawasaidia sana katika kupunguza gharama za kujiendesha na kujijenga upya. Hawataweza kufanya hivyo kwa kutegemea ada na michango.

Angalizo kubwa ni katika uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Kipaumbele kitolewe kwa wale ambao wameonyesha wazi kuwa wana uwezo ws kujenga hoja na wana msimamo usiotetereka. Watu kama Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko, Pendolino Peneza, Salome Makamba, Jesca Kishoka, Suzan Kiwanga na wengine wa calibre hiyo bila kusahau vijana kama yule waliyempora ushindi na kumpa John Mrema, yule aliyegombea Muheza na watu kama Mama Mollel.

Aidha waendelee kuwajenga wapambanaji vijana waliojitokeza kama yule wa Chato. Watu kama Heche, Lema, Msigwa, Sugu, Profesa Lwaitama, Askofu Mwamakula watumike kukijenga chama na kuendelea kuisimamia serikali wakiwa nje ya Bunge.
Waongeze ushirikiano na vyama kama ACT WAZALENDO na CHAUMMA kuendeleo shinikizo la kutaka Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi na mabadiliko katika utendaji wa vyombo vya dola.

Yote haya yanaweza kufanyika hata wakiwa na wawakilishi ndani ya Bunge.
Wakiamua kususa wajue kuwa Chama Tawala kitaendelea kama walivyofanya Zanzibar na hamna watakachoweza kufanya. Presha kutoka nchi za nje si za kutegemea.

Amandla...
 
Njia pekee ya kuleta significant impact ni maandamano, tatizo hatuiwezi, nyingine zote ni kupoteza muda tu.
Maandamano kwa wabongo yameshindikana kutokana na tabia mbaya ya wanasiasa kuwasaliti wananchi waliowapigania. Ile nunua nunua ya wanasiasa imeharibu spirit ya watu kujitoa kwa ajili ya wanasiasa.

Watu walikufa ktk uchaguzi wa 2010 wakiwapigania wapinzani washinde, halafu kiulaini tu mwanasiasa anajitoa na kuunga mkono juhudi.

Wakati ule wa CUF na Chadema ya Dr Slaa watu walikuwa tayari kwa lolote. Usaliti na ulaghai wa wanasiasa ulikuwa bado haujatamalaki.
 
Wakiwa Bungeni watakuwa na nafasi nzuri ya kuwatetea na kuwasemea kwa Mamlaka wale wote ambao kwa namna moja ya nyingine wataona kuwa hawajatendewa haki na serikali.
Kuwasemea kwa mamlaka ipi? Wakati wizi umebarikiwa na rais, waziri mkuu, spika na majaji.

Hao wabunge watakaokuwa bungeni watakuwa wamepatikana kwa uchaguzi gani (halali) na watakuwa wanalalamika uchaguzi gani (haramu)?

Mpk hapa tayari kuna mgawanyiko ndani ya upinzani. Wapo wanaotaka wabunge waende kwa maslahi mapana ya wao na matumbo yao na jamaa zao. Wapo wanasema wasiende kwa maslahi mapana ya chama. Kazi kwao.
 
Maandamano kwa wabongo yameshindikana kutokana na tabia mbaya ya wanasiasa kuwasaliti wananchi waliowapigania. Ile nunua nunua ya wanasiasa imeharibu spirit ya watu kujitoa kwa ajili ya wanasiasa.

Watu walikufa ktk uchaguzi wa 2010 wakiwapigania wapinzani washinde, halafu kiulaini tu mwanasiasa anajitoa na kuunga mkono juhudi.

Wakati ule wa CUF na Chadema ya Dr Slaa watu walikuwa tayari kwa lolote. Usaliti na ulaghai wa wanasiasa ulikuwa bado haujatamalaki.
Mimi nina amini wabongo tunaogopa zaidi marungu ya polisi kuliko hiyo sababu nyingine ya wanasiasa kuwasaliti wananchi. Kina Mambosasa huwa wanaropoka sana.

Kwasababu maeneo mengi Chadema bado imeonekana kuwa na uungwaji mkono mkubwa licha ya yale manunuzi ya CCM, hii inaonesha wananchi bado wanaiamini Chadema.

Halafu kwenye kusaliti, hilo sio kosa la chama, ni maamuzi ya mtu binafsi anaekubali kununulika, sasa huwezi kukilaumu chama kwa maamuzi ya mtu binafsi.
 
Kuwasemea kwa mamlaka ipi? Wakati wizi umebarikiwa na rais, waziri mkuu, spika na majaji.

Hao wabunge watakaokuwa bungeni watakuwa wamepatikana kwa uchaguzi gani (halali) na watakuwa wanalalamika uchaguzi gani (haramu)?

Mpk hapa tayari kuna mgawanyiko ndani ya upinzani. Wapo wanaotaka wabunge waende kwa maslahi mapana ya wao na matumbo yao na jamaa zao. Wapo wanasema wasiende kwa maslahi mapana ya chama. Kazi kwao.
Hapa niruhusu nimjibie ukipenda.

Wabunge walioenda bungeni isivyo halali majority ni CCM, hao wapinzani wote wameenda bungeni kwa kura halali za wananchi au njia nyingine halali kisheria (viti maalum) na hawa ni huyo mmoja wa jimbo na wale wa viti maalum kama wataenda. Hizi ni njia halali zilizowapeleka bungeni.

Uchaguzi unaitwa batili pale ambapo wabunge wa upinzani walipoporwa ushindi kwa lazima, wizi wa wazi, sasa hapa, mfano wabunge wanawake, wanaweza kulalalimika bungeni hawakutendewa haki kwenye uchaguzi, na kuwawakilisha wenzao wanaume, lakini wakiwa ni wawakilishi halali bungeni japo sio kwa njia ya sanduku la kura.

Usisahau negative impact ipo kwa njia zote, wakienda au wasipoenda.
 
Kweli chadema Mambo ya viti maaluum achana nayo Kama ni pesa za kuendesha chama wanachama watachangia, sio mda wa viti mahalum kwa Sasa mje na FAMILIA YA CHADEMA NCHI NZIMA KUSHIKAMANA NA KUSAIDIANA KATIKA SHIDA NA RAHA
 
Back
Top Bottom