Uchaguzi 2020 Kamati Kuu ya CHADEMA msimtie huzuni Lissu, kukubali adhabu ya kinyonyaji maana yake ni kukubali hata jaribio la kuibiwa kura

Uchaguzi 2020 Kamati Kuu ya CHADEMA msimtie huzuni Lissu, kukubali adhabu ya kinyonyaji maana yake ni kukubali hata jaribio la kuibiwa kura

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Kumpa pumzi CCM kwa siku 7 litakuwa kosa kubwa sana kwenye huu uchaguzi wa kihistoria.

Kukubali kutekeleza amri za kinyonyaji za NEC maana yake ni kipimo pia cha kukubali kuibiwa kura na kutokufanya chochote.

Naomba msimamie msimamo wenu wa 'Hatutakubali' na Lissu ameshasema jana, kwa mazingira ya sasa ambayo haki haipo, lazima NEC na CCM waelewe kwamba amani haitakuwepo na tunaanza sasa, kampeni ziendelee kesho na kinachotokea kitokee.

Huku mtaani moto umeshachochewa na kinachotakiwa ni moto uendelee kuchochewa hivyo hivyo ukizingatia zimebaki wiki tatu tu, kupoa kwa siku saba kutapooza sana huu moto tuliouwasha.

Ushauri wangu ni Lissu endelea na kampeni, liwalo na liwe, kama wanakuengua tuelewe kimoja, kwamba uchaguzi hautakuwepo, halafu sasa tuone kinachotokea.

Shetani na auawe ni dhambi kumpa pumzi shetani.
 
Naunga mkono hoja! Hili watu wengi hawalioni. Huwezi kupumzika kumpiga adui. Apumzike kwa lipi?
Msimamo ni haki lazima itendeke. Ubaki msimamo huo huo. Wenye unyonge wabaki na dhana zao za uoga na unyonge. Akifanya kutii hiyo amri ameshakwisha! Ccm wanapima upepo kuona reaction itakuwaje.
 
Nitofautiane na weye.
Shukran
 
CCM hawajamjua Lissu vizuri, ingekuwa ni binadamu wa aina yangu na wewe msomaji basi baada ya kupona risasi zote zile tusingethubutu hata kurudi Tanzania, achilia mbali kupaza sauti kwenye uwanja wa siasa cc (Ulimboka). Wanaiweka rehani amani ya nchi kwa maamuzi ya kijuha!
 
Naunga mkono hoja! Hili watu wengi hawalioni. Huwezi kupumzika kumpiga adui. Apumzike kwa lipi?
Msimamo ni haki lazima itendeke. Ubaki msimamo huo huo. Wenye unyonge wabaki na dhana zao za uoga na unyonge. Akifanya kutii hiyo amri ameshakwisha! Ccm wanapima upepo kuona reaction itakuwaje.
Ndo hapo sasa, kumpa pumzi adui maana yake unampa muda wa kukumaliza
 
Kama unajiamini upo kwenye haki hakuna kuogopa. Ccm ilipofikia haihitajiki kutumia hekima zote zilishafeli huko nyuma. Lugha moja tu ndiyo inawafaa. Ni anayotumia Lissu.

Acheni uoga.
Kabisa, CCM haihitaji busara tena, falsafa ya kutokukubali ndo inatowafaa kwa sasa, la sivyo tutazidi kuonewa kwa mda mrefu sana
 
Ndo hapo sasa, kumpa pumzi adui maana yake unampa mda wa kukumaliza
Maamuzi yote waliyofanya kwa Lissu ni batili. Tangu mwanzo mpaka sasa walipofikia. Lissu tangu mwanzo alionyesha msimamo wa kiume. Mbinu zote wanazotumia CCM ni kupima mapigo yatakuwaje. Mbinu moja juu ya nyengine yote ni kuangalia wapi ni penye udhaifu. Udhaifu wowote atakaonyesha Lissu atakuwa ameshakwisha.
 
Mpuuzi wewe lisu 1 nisawa na ccm 1000 ndio maana tume.police.viongozi waccm wote.msajili.wote haowanapambana na mtu1 lakini bado wanapwaya sana hakuna sababu ya mbowe kuzunguka waendelee namikakati mingine
Sawa.

Wakati utaongea na Mtajuta kumsimamisha T.Lissu kama mgombea wenu wa Urais Tz.
 
Lissu yupi huyu mwenye kashfa?[emoji2]
Lissu hana kashfa. Mwenye kashfa ni Meko.
Kashfa zenyewe ni hizi:

1. Wizi wa Tshs. Tril 1.5

2. Kujimilikisha ardhi ekari 25,000 kule Karagwe.

3. Kuuza na kuhonga nyumba za serikali kinyume na utaratibu.

4. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake.

5. Kutoa zabuni kwa mtu aliyeoa naye nyumba moja pasi kumshindanisha na wengine.

6. Kumteua mpwa wake kuwa mlipaji mkuu wa serikali wakati hajakidhi vigezo. Na kashfa nyingine lukuki.
 
Hizo porojo Watanzania hawajui hata moja ni uzushi wa Chadema

Ukitaja jina la Rais Magufuli mtaani wanamalizia MCHAPAKAZI

Huyo ndio Magufuli kipenzi cha Watanzania
Lissu hana kashfa. Mwenye kashfa ni Meko.
Kashfa zenyewe ni hizi:

1. Wizi wa Tshs. Tril 1.5

2. Kujimilikisha ardhi ekari 25,000 kule Karagwe.

3. Kuuza na kuhonga nyumba za serikali kinyume na utaratibu.

4. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake.

5. Kutoa zabuni kwa mtu aliyeoa naye nyumba moja pasi kumshindanisha na wengine.

6. Kumteua mpwa wake kuwa mlipaji mkuu wa serikali wakati hajakidhi vigezo. Na kashfa nyingine lukuki.
 
Kabisa, CCM haihitaji busara tena, falsafa ya kutokukubali ndo inatowafaa kwa sasa, la sivyo tutazidi kuonewa kwa mda mrefu sana
Kwa awamu hii msimamo wa Lissu polisi nao wanauogopa wanafanya mengi lakini kwa kujaribu. Tume ya Uchaguzi nayo inafanya hatua kwa hatua ili kuangalia uchochoro upi ambao watakaopita nao kwa Lissu. Ccm na watu wake wanachofanya ni hesabu. Wanaangalia formula ipi itakayo win.

Udhaifu wowote watakaoupata kwa Lissu huo ndiyo mwisho wa Lissu, na haya mahesabu hayataisha mpaka wapate hitaji lao. Hazitoisha kwa sababu zote ni kuangalia na kutafuta udhaifu wa LissuWanajaribu kutafuta udhaifu uko wapi.

Wananchi wanapiga mahesabu ya kiraia. Ambayo ni makosa makubwa.
 
Back
Top Bottom