Kumpa pumzi CCM kwa siku 7 litakuwa kosa kubwa sana kwenye huu uchaguzi wa kihistoria.
Kukubali kutekeleza amri za kinyonyaji za NEC maana yake ni kipimo pia cha kukubali kuibiwa kura na kutokufanya chochote.
Naomba msimamie msimamo wenu wa 'Hatutakubali' na Lissu ameshasema jana, kwa mazingira ya sasa ambayo haki haipo, lazima NEC na CCM waelewe kwamba amani haitakuwepo na tunaanza sasa, kampeni ziendelee kesho na kinachotokea kitokee.
Huku mtaani moto umeshachochewa na kinachotakiwa ni moto uendelee kuchochewa hivyo hivyo ukizingatia zimebaki wiki tatu tu, kupoa kwa siku saba kutapooza sana huu moto tuliouwasha.
Ushauri wangu ni Lissu endelea na kampeni, liwalo na liwe, kama wanakuengua tuelewe kimoja, kwamba uchaguzi hautakuwepo, halafu sasa tuone kinachotokea.
Shetani na auawe ni dhambi kumpa pumzi shetani.