Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Ushahidi wa simu ni kazi kweli kweli walahi
Chadema imekufa natural death walahi
 
Ushahidi wa simu ni kazi kweli kweli walahi
Chadema imekufa natural death walahi
kweli jembe hata hii press releases from mnyika ni ushahidi tosha
 
Ujumbe wako tumeshaanza kuufanyia kazi hata kabla hujauleta humu jf. Soon watatiwa nguvuni.
 
Wangejaribu kuwafukuza ndo ulikua mwisho wa Mbowe na chagadema yake,hao ndio wameshikiria button ya uhai wa Mbowe na saccos yake,wanajua dhambi zote
Yani wewe na wenzako uv got reckless hatred towards Chaggas.

You too low and boring

Bongo zenu zimejaa makapi ya mavi

Mbaafff
 
aisee makamanda hivi huu uzi una husiana na nini 😉
 
Kwa maoni yangu, na kwa Chadema ninayoijua mimi, ni Komu ndiye kamuokoa
Kubenea. Naomba msiniulize kamuokoaje.
P
 
Ni kweli tulikuwa tumelewa na tulikuwa tukiendesha gari. Yalikuwa ni maongezi ya kawaida.
 
Mkuu wangu; tatizo ni kuwa hawaamini kuna tatizo. Labda hekima imetamalaki hadi tatizo litakapojitokeza tena...
Mkuu yanayoendelea kuna 'state of denial' kwamba hawaamini kuna tatizo.
Katika matibabu, mgonjwa akiwa katika state of denial ni ngumu kwa tiba na huishia pabaya

Baada ya uchaguzi wa 2010 tuliwaeleza kuna matatizo ya aina mbili wayaangalie
(1)Internal- matatizo ndani (2)External- yanayotokea nje ya uwezo wao

Matatizo ya ndani; Kwamba, kiongozi anapoongoza mapambano mara 2 au 3 na kushindwa, lazima ifanyike analysis. Tatizo la waraka wa Kitila ilikuwa dalili kuna kutoridhika miongoni

Kosa la waraka kwa mtazamo wangu ni njia iliyotumika ambayo ikilenga kujenga udhaifu kabla ya uimara. Kwa wakati uliokuwepo haikuwa njia nzuri, ili set bad precedent.
Nilisema pia, waraka ulitakiwa uangaliwe hasa hoja za uongozi na mabaliko ya katiba

Jibu lingekuwa kuondoa udhaifu wa ndani kwa kufanya uchaguzi ili kutoa mandate ya uongozi
Hili lingejenga hali ya watu kuamini panapotokea matatizo kuna muda wa kuyarekebisha

Miaka 5 iliyopita tulijadili jamvini, kama hawatafanya hivyo wanatengeneza weakness itakayotumika kuwadhuru siku za baadaye. Sikuwa mbali na ukweli

External; Kwamba, lengo liwe kujenga mazingira ya kuwa na chaguzi huru.
Kipaumbele kiwe katika kushika mhimili mmoja kati ya miwili, bunge au serikali.

Kwa wakati ule, kushika serikali ikiwa na ''vyombo vyetu'' ni safari ndefu.
Njia ya mkato ni Bunge. Hawakusikia, tukasikia ''kanyaga twende''.

Lengo llikuwa shinikizo la mabadiliko yatayojenga uwanja sawa wa ''mapambano''

Kwa hali ya sasa, mahasimu wao wanatumia udhaifu wa ndani kuwahujumu.
Na kupitia njia hiyo hawana uwezo wa kupambana na external factors.

Wanarudi kule walikotoka , kushughulikia wasaliti kama wakati wa waraka.

Laiti wangekuwa na mfumo imara wa uongozi uliojengwa katika mazingira halali, hii isingekuwa hoja na mahasimu wasingeweza kuwahujumu, wangekuwa na agenda ya kupambana na matatizo ya nje ya kujenga mazingira huru na sawa katika sanduku la kura

Kilichofanyika jana ni busara mbovu. Kwamba ni busara yenye ubovu kwasababu imefunika matatizo haikuondoa matatizo. Ili kuwa na busara njema, lazima waende katika mzizi wa tatizo

1. Wakubali kuna tatizo linalohitaji suluhu ya kudumu na si dawa ya kutuliza maumivu

2. Wasikilize hoja wasizotaka kuzisikia ili kuelewa, grievance, grudge, concern and reservations zinazosababisha tatizo kujirudia

3. Watengeneze mazingira ambayo mtu atakaposhindwa kuyafuata hakuna vikao vya masaa mengi bila kujali wanahitaji masaa mengi kuhangaika na mfumo unaowanyima haki

Ni lazima wawe na uongozi legit ukiwa na mandate na support ya kila mmoja
 
Back
Top Bottom