Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Mazungumuzo ya faragha kati ya wabunge hao wawili waliyanasa kwa kutumia high communication technology. Ni technology gani hii ambayo wanaitumia kufuatilia faragha za wabunge wao na watu wengine? Jee kitendo cha kuingilia na kufuatilia faragha za mtu kwa sheria zetu si kosa la jinai kweli? Vyombo hivi si ndivyo vinatumiwagwa na majasusi? Walivipata wapi na kwa madhumuni gani? Jee wabunge hao waliofanyiwa ujasusi huo wanaweza kufungua kesi ya jinai dhidi ya chama hiki?

Kubenea na Komu fanyeni maamuzi magumu kabla Pole pole hajafunga mlango.
Kamuulize jiwe ile flash aliyokuwa anatamba nayo ni sheria gani inamruhusu kurekodi faragha za watu?

Akili ushuzi.
 
Wangejaribu kuwafukuza ndo ulikua mwisho wa Mbowe na chagadema yake,hao ndio wameshikiria button ya uhai wa Mbowe na saccos yake,wanajua dhambi zote
Vp Slaaa alikuwa hazijui dhambi zote?
 
Mkuu yanayoendelea kuna 'state of denial' kwamba hawaamini kuna tatizo.
Katika matibabu, mgonjwa akiwa katika state of denial ni ngumu kwa tiba na huishia pabaya

Laiti wangekuwa na mfumo imara wa uongozi uliojengwa katika mazingira halali, hii isingekuwa hoja na mahasimu wasingeweza kuwahujumu, wangekuwa na agenda ya kupambana na matatizo ya nje ya kujenga mazingira huru na sawa katika sanduku la kura

Kilichofanyika jana ni busara mbovu. Kwamba ni busara yenye ubovu kwasababu imefunika matatizo haikuondoa matatizo. Ili kuwa na busara njema, lazima waende katika mzizi wa tatizo

1. Wakubali kuna tatizo linalohitaji suluhu ya kudumu na si dawa ya kutuliza maumivu

2. Wasikilize hoja wasizotaka kuzisikia ili kuelewa, grievance, grudge, concern and reservations zinazosababisha tatizo kujirudia

3. Watengeneze mazingira ambayo mtu atakaposhindwa kuyafuata hakuna vikao vya masaa mengi bila kujali wanahitaji masaa mengi kuhangaika na mfumo unaowanyima haki

Ni lazima wawe na uongozi legit ukiwa na mandate na support ya kila mmoja
Mkuu Nguruvi3, asante kwa hii, kwanza ningekuomba upandishe uzi mahsus wa ushauri kwa Chadema, baada ya kilichotokea, na mimi kwa ruhusa yako, naomba kuipush hii, ili ushauri huu, Chadema wauone independently kwenye threads za ushauri na sio tuu kama mcha kwenye threads za events.

P
 
Ruzuku kwa sasa itakuwa kiasi gani?

Wezi wanapopigania kuiba kama wanavyotuibia waliopo wananchi inabidi tujihami.


2020 njoo haraka.

Kamuulize aliyewatuma kuwa baada ya hawa maspy wao kuwa exposed watamtumia nani kukivuruga chama..
 
Mkuu Nguruvi3 laiti hawa Chadema wangefikili kama unavyofikili
Hata Chadema angeondoka Mbowe kama Wezi wa kijani wanavyotamani bado Chadema ingesimama imara.

Hata hivyo Fanya kama Mkuu Pascal Mayalla alivyoshauri.


Wenda hawa Malaika wakakuelewa....


Maana kwao kila MTU ni shetani wa kijani.
 
Zito hakupanga njama za kuteka kiongozi yeyote.
Zito hakupanga njama za kumbambikia kesi ya uhujumu uchumi Mbowe,lakini alifukuzwa.
Hawa pamoja na njama hizo bado hawakufukuzwa..
Unadhani ni kwasababu ya kukiri tuu !?
Hapo kuna khofu ndio iliyopelekea maamuzi hayo
Adhabu imetolewa ndani ya mamlaka ya Kamati Kuu shida yako nini? haiwezekani KK ya Cahdema itoe adhabu zile zitakazo mpendeza Polepole na wewe? mbona wenye Chama wanaipongeza KK kwa kusimamia haki na kutoa adhabu satahili na huruma kidogo? mbona waliohukumiwa hawajalalama kama wewe?
 
Ninachoona mimi hapa ni tishia toto tu kweli chadema hawana ubavu wa kuwavua uanachama na ubunge maana watabaki uchi,walichofanya ni kuwavua nyazifa zisizo na maana.chamaana watengeneze nyumba yao maana hapakaliki na ukweli ndio huo.na kamwe wasijifariji kwa hili.
 
Back
Top Bottom