Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Ulitaka kunifanyaje dada? Tunaendelea kuwanyoosha sasa BAWACHA sasa haipo inabidi muanze upya! Huko siyo kunyooshwa huko?
Nenda kawalambe wote Covid 19 uwageuze kama chapati hawana kazi utawapata kirahisi sana. Muhimu uwe rijali tu
 
Naomba hili niliweke wazi ili lieleweke vizuri kwa wadau wa JF na wanaofuatilia , ikumbukwe kwamba hawa wasaliti karibu wote ni viongozi wa BAWACHA na wengine BAVICHA , sasa kwa protocol ya Chadema kwanza wanavuliwa vyeo halafu ndio wanavuliwa uanachama .

Haya yote yamefanyika leo , kwa maana ya kwamba Halima Mdee na mamluki wenzake wamevuliwa uanachama wa Chadema bila huruma yoyote na kwamba kuanzia dk hii hawatakiwi kufanya chochote kwa niaba ya Chadema .

Mkuu mleta mada

1. Nusrat hakuapishwa saa moja usiku kama ulivyomnukuu Mbowe kila mmoja aliona tukio hilo ilukwa ni mchana kweupe;
2. Mh Freeman Mbowe kudai taratibu na kanuni za kudumu za bunge zimekiukwa na kwamba mbunge anaapishwa ndani ya bunge pekee wakati akijua anasema uongo wa wazi kabisa maana yeye pamoja na wabunge wengine walishiriki kubadilisha kanuni Agosti 2020 (Rejea TANGAZO LA SERIKALI NA. 626 la tarehe 7/8/2020) na mabadiliko ni haya:
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya
(1), endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, Spika atamwapisha katika: (a) kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge; au (b) eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.

(3) Wakati wa kuapa, Mbunge anayeamini kuwa kuna Mungu, atalazimika kushika Biblia au Kuran au kitabu kingine kitakatifu kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(4) Iwapo Mbunge haamini kuwa kuna Mungu, hatashika Biblia au Kuran au kitabu chochote kitakatifu au kutamka maneno, “Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie,” bali atalazimika kuinua mkono wake wa kuume juu.
(5) Kiapo cha uaminifu cha Mbunge kitakuwa na maneno yafuatayo: “Mimi, ………..., naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.”
 
Hata hivyo, tayari hawatakua tena wanaaminika na taasisi ya CHADEMA, kwa sababu chama ni watu na kuaminika(intergrity)
 
1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.

2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.

3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.

4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!

Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?

Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?
 
Jumatatu Wataenda High Court Halafu Watabaki Wakiwa Na Ujanjaujanja Tu, Mpaka Miaka Mitano Iishi
Usiku Sasa Hivi Ccm Na Wakina Mama Wataweka 4WD Na Lock Dif Ili Wavuke Salama!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…