Kamati maalum ya TLS kuchunguza Mkataba wa uendeshaji bandari ya Dar

Kamati maalum ya TLS kuchunguza Mkataba wa uendeshaji bandari ya Dar

Hicho chama sijawahi kusikia kimeigimea au kuiambia serikali iachane na mkataba wowote. Huko ni sawa na Bunge la kina Prof Msukuma🙄
 
Ccm Kimya Wao Wanasema Wana Ilani Vp Hili La Bandari Lipo
 
hao lazima wapigwe mpunga mrefuu na wataleta jibu linalowafurahisha waarabu. waarabu wanajua sana kumwaga pesa.

Hawa watu ni wanafki, mkataba umesainiwa October, tuseme hawakujua? Mpaka makelele ya socual media ndio waamke! Kwanza hakuna watakachofanya ni kutafuta popularity ya hovyo! And this tells alot juu ya vyombo ambavyo havina meno!
 
hao lazima wapigwe mpunga mrefuu na wataleta jibu linalowafurahisha waarabu. waarabu wanajua sana kumwaga pesa.

Hawa watu ni wanafki, mkataba umesainiwa tangia October, tuseme hawakujua? Mpaka makelele ya social media ndio waamke!

Kwanza hakuna watakachofanya ni kutafuta popularity ya hovyo! And this tells alot juu ya vyombo ambavyo havina meno!
 
Team members must observe high integrity in making the investigation properly.

Wajue waTZ wanawategemea.

Wamuogope Mwenyezi Mungu aonaye mpaka sirini.
 
Ccm Kimya Wao Wanasema Wana Ilani Vp Hili La Bandari Lipo
30. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitahakikisha Serikali inachukua hatua ili Taifa liendelee kunufaika na fursa zake za kijiografia kwa kutekeleza yafuatayo🙁a) Kubuni na kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ili Tanzania iweze kunufaika zaidi na fursa hiyo ya kijiografia; (b) Kuboresha na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi kwa lengo la kudumisha uhusiano wenye tija kiuchumi na nchi zinazotuzunguka; (c) Kubuni mikakati itakayowezesha kuimarika kwa Jiji la Dar es Salaam kuwa kitovu cha biashara kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati; (d) Kubuni na kutekeleza mikakati itakayowezesha kuainisha maeneo yote ambayo yatakuwa na manufaa kiuchumi ili kuweza kuzitumia fursa hizo kwa ajili ya kukuza uchumi; na (e) Kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na shughuli nyingine za lojistiki na uchukuzi ili Taifa letu liweze kutumia fursa za kijiografia ipasavyo.
 
EYote yatapita na Mwarabu atachukua bandari tutaishia kupiga zogo kwenye keyboard ,kuonyesha hasira zetu twende Kwa road watanzania


Tunahitaji mkaba mzuri haya mambo ya uarabu, uchina na wazungu hauna tija. Tumejaribu kwa wazawa matunda yake ni kujuana na wizi tu!
 
BARAZA la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) limeunda kamati maalum ya wataalamu kuchambua makubalino yaliyoainishwa katika mkataba wa uendeshaji bandari ya Dar es Salaam kati ya serikali ya Tanzania na Kampuni ya Dubai ya DP World.

Rais wa TLS, Wakili Harold Sungusia amesema kamati hiyo itaongozwa na Makamu wa Rais wa TLS, Wakili Aisha Sinda na itakuwa na wajumbe wengine wanne

Sungusia amewataja wajumbe wengine kuwa ni

Dk. Hawa Sinare – (Makamu Mwenyekiti),

Wakili Mpale Mpoki – (Mjumbe),

Wakili Stephen Mwakibolwa – (Mjumbe) na Wakili Mackphason Mshana - Katibu“

TLS inatambua uwepo wa mijadala inayoendelea nchini kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai… Kamati itatoa ripoti yake na mapendekezo yake kwa Baraza la Uongozi tarehe 12/06/2023 ili TLS iweze kutoa maoni na kwa hatua zaidi,” amesema Wakili Sungusia.

====

TLS inatambua uwepo wa mijadala inayoendelea nchini kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai. Kutokana na unyeti wa swala hili, Baraza la Uongozi la TLS likiongozwa na Rais, Wakili Harold Sungusia limeunda kamati ya wataalamu kuchambua makubaliano hayo. Baraza hili litaongozwa na Makamu wa Raisi wa TLS, Wakili Aisha Sinda, likiwa na wajumbe wafuatao.
1. Dkt Hawa Sinare – Makamu Mwenyekiti
2. Wakili Mpale Mpoki – Mjumbe
3. Wakili Stephen Mwakibolwa – Mjumbe
4. Wakili Mackphason Mshana – Katibu
Kamati itatoa ripoti yake na mapendekezo yake kwa Baraza la Uongozi tarehe 12/06/2023 ili TLS iweze kutoa maoni na kwa hatua zaidi.
Huyo hawa sinare si dada yake na mwanaidi maaja ambaye ni rafiki ya na saa100 unategema nini hapo
 
Hao TLS si ndio walisifiwa juzi na Samia?

Bladifakeni.
 
Huyo hawa sinare si dada yake na mwanaidi maaja ambaye ni rafiki ya na saa100 unategema nini hapo
na ni mmojawapo wa wanasheria waliokuwepo REX ATTORNEYS, waleee wa mkataba wa richmond kama mnakumbuka.
 
Huu upepo utapita maisha yataendelea

Ova
 
Dawa ni wananchi kuingia barabarani kuweka pressure ,kwenda mahakamani kuweka pingamizi, kulizunguka bunge usiku na mchana lizuie na kusimamisha mkataba wowote, kuzuia hili lazima ufanye mambo bila akili
 
Watahongwa hata wao hamuwajui waarabu kwa ufisadi!
 
Back
Top Bottom