Kamati ya Amani yapiga marufuku Magufuli kuitwa "Mwendazake", Wametumia sheria gani?

Mwendazake,Mwendazake,Mwendazake,Mwendazake,piga kelele kwa mwendazake ake!
 
Nafuu hao wanafiki wa makanisani wange kaa kimya hilo jina lingekufa lenyewe. Ila baada ya kulisemea hapo ndiyo wameli PROMOTE.

Magufuli atabakia Mwendazake tu
 
Wamepotoka tu. Watu wakiamua kutukana wanaweza kugeuza neno lolote kuwa tusi tu. Maneno kama tigo na masaburi, kimsingi sio matusi lakini kuna muktadha watumiaji wanayatumia kama matusi......unawea hata kusita kuyatamka mbele ya watu!

Watu wameamua kutumia neno mwendazake badala ya jina Magufuli.....sijaona shida hata kidogo. Kama kuna wanaomlaumu au kumtukana, wanaweza kufanya hivyo kwa kutumia jina lolote. Kama kule twita republic, wanavyomuita meko!
 
Kamati ya amani inachochea,
Ingetathimini kwa nini wasiitwe marehem wengine hilo jina.

Inawapasa kushauri kuunda tume huru kuchunguza yanayotamkwa mitandaoni ili kuepusha Siku zijazo yasitokee haya.
 
Sasa hivi kila kitu kinaletwa JF. Hivi kweli maelezo kama haya unastahili kuyaleta hapa kwa majadiliano? Watu wanapotumia matusi huwa yanatafutwa kwenye kamusi? Wowowo imo ndani ya kamusi? Neno mshenzi ni tusi lakini mtaani wanaoitwa washenzi kweli kweli wanatukanwa?

Nawe kweli unaona Malisa ana elimu ya kutuelimisha JF? Mbona munakuwa wapuuzi kiasi hiki?
 
MWENDAZaKE ni Mmoja tu...Ili Jina ni la Kipekee na Linatumiwa Kumaanisha Mtu Mmoja tu Kama Mjumbe hapo Juu...MWENDAZAKE alishaendazake Hakuna Namna tukubaliane na Khali. Ukilitaja Jina la MWENDAZAKE Mawazo na fikra za Watanzania Yanawafikisha kwa SABAYA NA BASHITE means Binadamu wenye roho mbaya , katili na Watesi.
 
Wangeanza kuwazuia na kule kenya kutumia neno mwendazake, maana wao ndo wanapenda kutumia sana misamiati ya kwenye kamusi ambayo haijazoeleka kwa wabongo.
 
Tunaanza kupangiana Vocabulary za kutumia ? Akija Mgeni asiyejua matatizo lukuki tuliyonayo anaweza kudhani tumeshatatua issue zote za maana ndio maana tunaanza kushughulikia mambo yasiyo na tija...
 
Anunuliwe kamusi ili ajifunze lugha. Cha msingi yeye ahimize watawala na vyombo vyake kutenda haki kwa raia pamoja na kudai katiba mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…