Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Unatumia nguvu nyingi sana kufikisha ujumbe ambao hata ufahamu nao hauna. Kwa hiyo kwa imani yako na ufahamu wako ukisign ndiyo umechukua posho? Be serious!
Nikubaliane na ww kuwa siyo lazima uichukue,na km unajua kusoma vizuri kiswahili sidhani km ungeuliza hilo swali. Nilichosema mimi kitendo cha kusaini mahudhurio ni kuidhinisha posho itoke kutoka ktk mamlaka inayoshughulikia posho hizo. Swali langu ambalo nalirejea kwako,je! Hiyo posho mbunge akiiacha inaenda wapi? Labda nikuambie jambo moja,zitto huenda kweli hachukui posho. Lkn kitendo hicho kinaongeza ufisadi,ni bora hata angezichukua na kuzipeleka jimboni kwake. Kwa sasa zinapotea bure,halafu nyie misukule wake wala hamjiulizi kwa nn hajawahi kuuliza posho yake huwa inaenda wapi..!!? Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Wakuu JF amani iwe Nanyi.

Kuna upotoshaji Mkubwa sana ulioanzia jana Facebook kuwa ile kamati teule ya kufuatilia madai ya ongezeko la Posho kwa wabunge la Bunge la katiba kupendekeza ongezeko la posho Mpaka kufikia 500,000

Leo kwenye gazeti la Mwananchi kuna hii Habari

Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.
Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.
Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.

Dodoma. Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.

Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.

Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.

Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.

"Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha," alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Mjumbe mwingine, ambaye pia hakutaka kutajwa, alisema kuwa watakaa leo kukamilisha taarifa ya utafiti wao, kabla ya kuikabidhi kwa Mwenyekiti Kificho.

Alisema pamoja na umuhimu wa kazi za mbunge, lakini isingekuwa rahisi kuongeza posho katika mazingira ya sasa, ambapo wananchi wanalia hali ngumu ya maisha.

Wajumbe hao walioteuliwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho ni William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari.

Awali, taarifa kutoka ndani ya Bunge zilidokeza kuwa wajumbe hao walikuwa wakutane jana saa 9:00 alasiri ili kuandaa ripoti itakayopelekwa kwa Kificho ikiwa imebeba ushauri kuwa kiwango cha sasa cha posho kinatosha.

Sh300,000 wanazolipwa wajumbe wa Bunge Maalamu la Katiba zinajumuisha Sh80,000 kwa siku ambayo ni posho ya kujikimu na Sh220,000 kwa siku kama posho maalumu ya kuhudhuria kikao.

Posho maalumu ya Sh220,000 inajumuisha posho ya dereva inayopaswa iwe kati ya Sh40,000 na Sh45,000 kwa siku, usafiri wa ndani (mafuta ama teksi), mawasiliano na matumizi mengine binafsi.

Ofisi ya Bunge Maalumu

Alipoulizwa kuhusu jambo hilo mmoja wa makatibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alisema suala la posho linashughulikiwa na Serikali.

"Ninachokifahamu ni kuwa suala la posho limetoka mikononi mwa Kificho na sasa lipo serikalini. Kamati iliyoundwa bado inalishughulikia suala hilo. Hicho ndiyo ninachokifahamu," alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.

Kwa nyakati tofauti gazeti hili lilimtafuta Kificho, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao za mkononi zilikuwa zikiita bila majibu.

Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao ni wabunge wa CCM waliodai kuwa kiwango cha Sh300,000 wanacholipwa, hakitoshi kwa kile walichodai kuwa ni kuishi Dodoma ni gharama kubwa.

Hata hivyo uchunguzi wa kina umebaini kuwa baadhi ya wajumbe wanaishi katika hoteli za kati ya Sh20,000 na Sh40,000 kwa siku huku baadhi yao wakiishi katika hosteli kwa Sh8,000 kwa siku.

Mmoja wa wajumbe, Augustino Mrema alidai kuwa baadhi ya wajumbe wanataka kuligeuza Bunge hilo ‘shamba la bibi' kwa kudai posho zaidi kwa kisingizio cha kupanda gharama za maisha.

Mrema alisema kiasi cha Sh300,000 wanacholipwa wajumbe kinatosha kwani zipo hoteli nzuri za kati ya Sh15,000 hadi Sh40,000 ambazo zina hadhi na sifa ya kuishi wajumbe wa Bunge la Katiba.

"Mjumbe ameamua kwenda kuishi chumba cha Sh200,000 wakati akijua atalipwa posho ya Sh300,000 halafu analalamika kupanda kwa gharama za maisha, hizi gharama zimetengenezwa," alisema Mrema.

Alisema gharama za teksi kutoka bungeni hadi maeneo ya Area C na D haizidi Sh12,000 wakati chakula kinaanzia Sh6,000 hadi Sh20,000 na kuhoji iweje Sh300,000 zionekane hazitoshi.

Hoja ya baadhi ya wajumbe kudai posho zaidi imepigiwa kelele nchi nzima huku wananchi wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo, kama wataendelea kung'ang'ania kupanda kwa posho.

Mjumbe mwingine wa Bunge hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ameahidi kuanzia leo kukusanya saini za wajumbe wanaopinga suala hili ili ampelekee Rais Kikwete kama ushahidi.

Source: Mwananchi

My take
Kutaka sifa na kurejesha Heshima iliyopotea kutawaponza wengi sana

Kwa mantiki hii hatua ya Mtatiro haona tena mantiki...
 
Zitto ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa wa kucheza na akiliza za vilaza hiiinatokana na unafki wake wa hali ya juu.Kwa mfano kwenye hili swala la posho zitto amedhililisha hilo na wengi wenye uelewa mdogo wamemuona shujaa.
Baada ya baadhi ya wabunge wa ccm kudai nyongeza ya posho (lejea post ya mtatiro fb) kuliibuka makundi mawili moja likipinga ongezeko la posho (hasa wapinzani) na linguine likitaka posho iongezwe .
Kutokana na swala hilo kuhalibu ratiba ya bunge ilibidi mwenyekiti wa mda aunde kamati itakayo enda kukutana na serikali ili kutafuta suluhu ya hili jambo . Hiyo kamati ikihusisha wabunge wanao unga mkono ongezeko la posho na wale wanao pinga (washindane kwa hoja). Na kwaupande wanao pinga hasa wapinzani iliongozwa na mbowe, ambapo kabla ya kukutana na kamati alikaa na wapinzania na kutoka na azimio moja la kupinga nyongeza yoyote ya posho.
Kitu ambacho zitto hakukipenda na makusudi akaanza kuupotosha umma kua kamati imeundwa ili kwenda kuongeza posho. (Ana taka yeye aonekane ndie mtetezi wa wanyonge). Sababu ya yote ni kua hakuteuliwa yeye kwenye kamati hiyo. Baadae kwa habari zisizo za kweli, zitto akaandika facebook kua posho zimeongezwa kufikia laki 5 ili uma umchukie mbowe aonekane alienda kutetea posho.
Baadae anakuja na hoja nyingine aliyo kuja nayo Mtatiro ya kukusanya sahini za wabunge (mtatiro alimuwahi) baada ya kuona hivyo zitto akaandika facebook kua atamuunga mkono Mtatiro kwa kusaini fomu ya za kupinga posho eti kamati ya akina mbwe imeongeza posho mpaka laki 500,000 (uongo mkubwa).Swali la kujiuliza utakusanyaje saini kabla kamati haijaleta majibu yake?kama walikua hawaiamini kamati kwa nini waliipendekeza?.Aibu imemfika baada ya kusikia hoja ya Mbowe ya kupinga posho imekubarika hivyo njia yake ya kutafuta njia ya kuonekana mzarendo imekwama.
Lakini tujikumbushe kidogo zitto huyu huyu kabla bunge hili halijaanza alisema hatapokea posha kwa sababu anapokea mshahala wa ubunge, pia ndani ya hiyo posho ya sh 300,000/= kuna seating allowance ya 24,000/= ndani yake .(vilaza wakasema kweli huyu mzalendo).Baada ya kuona watu wameisha mshtukia kua anatafuta umaarufu wa kinafki akaja na hoja nyingine kua atapokea posho lakini sio nyongeza ya posho watu wakahoji huyu mzalendo vipi tena si alisema hata pokea posho iweje abadilike na kusema hata pokea nyongeza mabayo anajua kwa kuna uwezekano mkubwa isiongezwe?. Ndipo wenye akili tusha mjua kua kijana nimnafki na wala sio mzalendo . Soma comment ya kwanza hapo kwenye picha iliyo muumbua.
2Q==
 
Nikubaliane na ww kuwa siyo lazima uichukue,na km unajua kusoma vizuri kiswahili sidhani km ungeuliza hilo swali. Nilichosema mimi kitendo cha kusaini mahudhurio ni kuidhinisha posho itoke kutoka ktk mamlaka inayoshughulikia posho hizo. Swali langu ambalo nalirejea kwako,je! Hiyo posho mbunge akiiacha inaenda wapi? Labda nikuambie jambo moja,zitto huenda kweli hachukui posho. Lkn kitendo hicho kinaongeza ufisadi,ni bora hata angezichukua na kuzipeleka jimboni kwake. Kwa sasa zinapotea bure,halafu nyie misukule wake wala hamjiulizi kwa nn hajawahi kuuliza posho yake huwa inaenda wapi..!!? Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Pale unaponiita msukule wa Zitto huwa tayari umejionyesha ni mtu mwenye uwezo kiasi gani cha kujenga hoja. I cant waste my time arguing with your likes
 
Hv huwa mnafikiria kwa kutumia viungo gani ktk mwili..!? Ushujaa wake uko wapi wakati anasaini mahudhurio? Ukisaini mahudhurio,maana yake umeidhinisha posho yako itumike. Na kutosaini mahudhurio ni kosa kwa kanuni za bunge. Tupe maelezo toka aanze kukataa posho,zile pesa huwa zinapelekwa wapi? Au kwa akili yako zinarudishwa hazina!? Unalishwa sumu ya kijinga wewe unashabikia! Pia umesema ile kamati imejaa wasomi ndo maana wamemzidi ujanja mbowe. Kumbe kuwa msomi ni kuwahadaa wasiosoma ili uwaibie!? Km jibu ni ndiyo,kuna haja gani ya kuwa na wasomi wezi? Ndo maana tumefika hapa kwa kuongozwa na wachumia tumbo..!!

Ndugu punguza jazba!
 
Zitto ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa wa kucheza na akiliza za vilaza hiiinatokana na unafki wake wa hali ya juu.Kwa mfano kwenye hili swala la posho zitto amedhililisha hilo na wengi wenye uelewa mdogo wamemuona shujaa.
Baada ya baadhi ya wabunge wa ccm kudai nyongeza ya posho (lejea post ya mtatiro fb) kuliibuka makundi mawili moja likipinga ongezeko la posho (hasa wapinzani) na linguine likitaka posho iongezwe .
Kutokana na swala hilo kuhalibu ratiba ya bunge ilibidi mwenyekiti wa mda aunde kamati itakayo enda kukutana na serikali ili kutafuta suluhu ya hili jambo . Hiyo kamati ikihusisha wabunge wanao unga mkono ongezeko la posho na wale wanao pinga (washindane kwa hoja). Na kwaupande wanao pinga hasa wapinzani iliongozwa na mbowe, ambapo kabla ya kukutana na kamati alikaa na wapinzania na kutoka na azimio moja la kupinga nyongeza yoyote ya posho.
Kitu ambacho zitto hakukipenda na makusudi akaanza kuupotosha umma kua kamati imeundwa ili kwenda kuongeza posho. (Ana taka yeye aonekane ndie mtetezi wa wanyonge). Sababu ya yote ni kua hakuteuliwa yeye kwenye kamati hiyo. Baadae kwa habari zisizo za kweli, zitto akaandika facebook kua posho zimeongezwa kufikia laki 5 ili uma umchukie mbowe aonekane alienda kutetea posho.
Baadae anakuja na hoja nyingine aliyo kuja nayo Mtatiro ya kukusanya sahini za wabunge (mtatiro alimuwahi) baada ya kuona hivyo zitto akaandika facebook kua atamuunga mkono Mtatiro kwa kusaini fomu ya za kupinga posho eti kamati ya akina mbwe imeongeza posho mpaka laki 500,000 (uongo mkubwa).Swali la kujiuliza utakusanyaje saini kabla kamati haijaleta majibu yake?kama walikua hawaiamini kamati kwa nini waliipendekeza?.Aibu imemfika baada ya kusikia hoja ya Mbowe ya kupinga posho imekubarika hivyo njia yake ya kutafuta njia ya kuonekana mzarendo imekwama.
Lakini tujikumbushe kidogo zitto huyu huyu kabla bunge hili halijaanza alisema hatapokea posha kwa sababu anapokea mshahala wa ubunge, pia ndani ya hiyo posho ya sh 300,000/= kuna seating allowance ya 24,000/= ndani yake .(vilaza wakasema kweli huyu mzalendo).Baada ya kuona watu wameisha mshtukia kua anatafuta umaarufu wa kinafki akaja na hoja nyingine kua atapokea posho lakini sio nyongeza ya posho watu wakahoji huyu mzalendo vipi tena si alisema hata pokea posho iweje abadilike na kusema hata pokea nyongeza mabayo anajua kwa kuna uwezekano mkubwa isiongezwe?. Ndipo wenye akili tusha mjua kua kijana nimnafki na wala sio mzalendo . Soma comment ya kwanza hapo kwenye picha iliyo muumbua.
2Q==

Acha kuendeshwa kwa hisia, Unajua hadidu za rejea walizopewa kwenye ile kamati? kama hujui basi kafuatilie kwanza kisha utaelewa kwanini ile kamati watu wanaiita ya "Kuongeza posho"
 
Naumia sana ninapoyaona haya yakiendelea huku tukiwa na Viongozi wakubwa ndani ya bunge maalumu la Katiba wanaojiita wapigania haki na maendeleo ya nchi yetu.... Hivi hili ndugu zangu wasiopenda posho mbona sijasikia WAKITOA tamko tofauti na ZZK.
 
Unaandika juu juu mno alafu unategemea watu watakuelewa ulichoandika
 
Hi posho watu wanapiga kelele lakini itapitishwa
Hii ni kwasababu kuna makundi yana rasimu yao mfukoni ili ipite itakuaje ? shari posho ingezwe ili kuwahonga wabunge

Hi ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Hebu niambie bila jaziba,utaratibu wa kupata hiyo posho ni kusaini mahudhurio,jambo ambalo hata zito anafanya. Kitendo cha kusaini mahudhurio,ni kukubali kupokea posho. Haya,tufanye amesaini halafu akaziacha,lkn serikalini zimetoka. Kwa akili yako hizo pesa zinaelekezwa wapi? Ukinipa hayo majibu ntarudi kwako kukupa maoni yangu. Kitendo cha wewe kuanza na matusi,umedhihirisha tu kwamba unafikiri kwa kutumia kiungo kingine..!!

Kwa taratibu za fedha, serikali au mashirika ya kimataifa ambapo nia experience na maeneo hayo, ni lazima kuwe na form mbili tofauti. Fomu ya mahudhurio na fomu ya malipo hivyo sidhani kwamba akisaini kuhudhuria ndio amesaini na kuchukua fedha. Hii si sahihi kwa misingi niliyokueleza hapo juu.

Hata, hivyo open your mind to a minimum level of thinking. Kutochukua fedha za posho kwa Mbunge mmoja hakuleti kuokoa fedha (kwa wakati huo), kunalenga kuonyesha kwamba hakubaliani na mfumo husika hivyo fedha itaokolewa tu iwapo wote (In Aggregate) wangelitekeleza msimamo huo. Hii ni sawa na kama unaposikia watu wameandamana kupinga jambo fulani, sio kwamba kupinga kwao ni kuondoa lile dhara papo kwa papo ila kujenga asbabu ya kurekebisha policy husika.
 
Lkn hebu tuwe wakweli na tuache unafiki..! Kati yetu tunaopinga hiyo posho,tunapinga kwakuwa ni wazalendo au ni wivu na unafiki tu..!? Kuna ambae anaweza kukataa kweli km angeteuliwa yeye? Zzk,ndo mnafiki zaidi,hivi anavyopinga facebook inasaidia nini? Chadema wamekubaliana kutoka nje ya bunge km kamati itaridhia posho iongezwe. Tutauona hapo uzalendo wa zitto kma nae atatoka nje. Kweli nchi hii bila unafiki haiendi..!!

Unachuki na Zito,jadili Hoja,hii inshu haina chama ni uroho wa Mtu
 
Tuacheni nasisi wauza madawa tupige hela kivyetu maana hizo za serekalini hatuna uwezo nazo

*****!!!!! yani nimepitia uzi zote ni wachache wanaojielewa kama wewe mkuu, mkuu we kazana tu kutenegeneza pesa,lakini achana na madawa kwani yanatuharibia hata watoto wetu wenyewe,ila kama unaweza ingia hadi kwenye biashara ya pembe za ndovu, ngozi za chui, simba n.k..huu mwaka unaitwa wa mavuno, we waache wabwabwaje humu akati yale majitu yanukula MAPESA, hakianani we Mbunge wangu nakuhakikishia ukichukua hiyo 500, 000/= usitie uso wako huku tuliko..
 
Naumia sana ninapoyaona haya yakiendelea huku tukiwa na Viongozi wakubwa ndani ya bunge maalumu la Katiba wanaojiita wapigania haki na maendeleo ya nchi yetu.... Hivi hili ndugu zangu wasiopenda posho mbona sijasikia WAKITOA tamko tofauti na ZZK.
Ni kwasababu wana hekima na hawakurupuki kutafuta sifa.
 
Back
Top Bottom