Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Yule mzee alituona mazwazwa sana...

Kamati inasemaje kuhusu ule uwanja wa kimataifa wa Chato? Njiwa zinatua pale au tufanye uwanja wa ng'ombe kuotea jua wapate vitamin D kwa wingi?
Unadhani hii hasara imeletwa na ujenzi wa uwanja wa chato? Au ni namna serikali yako pendwa inavyozitumia ndege kama daladala?
 
..mtamsingizia Maza kwa hasara hiyo.

..hasara ya billion 400+ lazima ilianza na Magufuli, haiwezekani iwe imepatikana ndani ya muda mfupi tangu atangulie mbele za haki...
Usimsingizie mzee wa watu, ripoti ya kumchafua ilishasomwa wiki tatu baada ya kifo chake ni figures zilikua ni bilioni 60 kwa miaka mitatu, hizo 400+ mtuambie zimepatikanaje ndani ya miezi minne!

Chuki yako dhidi ya mwendazake haibadilishi ukweli kwamba alikua raisi bora!
 
Akili zitarudi tu. Hivi kuna shirika kama hilo hapa nchini? Kwa kuanzia halina ndege zake lenyewe kwani karibia zote ni za kukodi. Hivyo basi wanapaswa kwanza kuwalipa hao waliowakodisha hizo ndege, watoe na fedha za uendedhaji wa hizo shughuli zao ndiposa wabaki na faida! Mkodishaji anafaidika zaidi. Enzi zetu tukiuita uhusiano huu kuwa wa kinyonyaji. Unakaa tu nyumbani, Una majumba 10 mjini uliyoyapangisha na unavuta pesa kiulaini!
Huku umevaa musuli unavuta kiko na kunywa kahawa siku nzima! Mwenye majumba ya kupangisha enzi hizo akiitwa Kabaila!!
 
Bilioni 100 na riba yake za hasara ya yule mhukumiwa ziko fungu lipi?
 
Hilo shirika haijulikani wanachokifanya zaidi ya serikali kupoteza pesa za walipa kodi kuhangaika na shirika mfu kama hilo......kama hao wabunge wanapigwa butwaa basi wananchi wangekuwa wamezimia au kufa kabisa kwa mshtuko.
 
Kwanini ATCL isipate hasara wakati zinatumika na Top three kama boda boda! Utasikia Rais yupo Rwanda na lile dege kubwa Dreamliner, Makamu yupo Burundi na Airbus, huku PM yupo kwao kusalimia kwa Bombardier. Nchi imepoteza dira kabisa.
Watu wanapigwa misele tu
 
Back
Top Bottom