Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Sasa kwa taarifa yako jiandae. Wewe na hao mabwana zako. Mtajuta kuiba uchaguzi mwaka huu.

Eti Tanzania haijawai kuwalamba miguu wakati kila siku mbatembeza bakuli kwao kuomba hela za misaaada na mikopo.

Na jiandaeni kula jeuri yenu. Bado ICC sasa
 
Mta
Mtasubili ujinga wenu wakati nchi inasonga,
Kama walizuia vi pesa vyao vya umeme na tuaendelea kuweka umeme sasa vi jipesa vyao ni tisho gani?
Sana sana wanatufundisha kujitegemea na siku wakirudi wanakuta tupo uchumi wa kati b+ ndo watajuta.
Fedha zaidi ya TZS billion 70 ambazo EU imeipa Tanzania katika kupambana na Corona ambayo serekali ilijinasibu haipo hadi kukataza watu kuvaa barakoa zipo wapi?Huu ni ufisadi wa karne na ufisadi wa kimataifa.Ufisadi across borders.Kwa mara ya kwanza tokea uhuru Tanzania imefanya ufisadi wa mabillion ya hela nje ya mipaka yake!
 
Sisi ni donor country tusiogope. Tumepewa misaada tangu uhuru lakini hatusogei, misaada hiyo hadi bwashee? Sisi tuombe fair trade nao sio misaada. Hakuna msaada wa bure mzee. Ukiona yuko mtu anampa misaada mingi dada yako, shituka.
 
Sidhani kama uchumi wetu unategemea EU. Tulishatoka huko kwenye utegemezi.
D3350739-6870-4AE8-816E-9B91CD2219D7.jpeg
 
Fedha zaidi ya TZS billion 70 ambazo EU imeipa Tanzania katika kupambana na Corona ambayo serekali ilijinasibu haipo hadi kukataza watu kuvaa barakoa zipo wapi?Huu ni ufisadi wa karne,ufisadi wa kimataifa.Ufisadi across borders.Kwa mara ya kwanza tokea uhuru Tanzania imefanya ufisadi nje ya mipaka yake!
Lazima wajute mwaka huu
 
Bila kupoteza Muda naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja,

Leo nilitenga muda wa kusikiliza kile kilichokuwa kinajadaliwa na Hawa Viumbe wa "EU" (External affairs), Kama tulivyo taarifiwa juzi katika vyombo vya habari vya kwao huko na baadhi ya nyuzi hapa JF.

Ila Nimesikitika Sana kuwa nilichotarajia kukisia kutoka kwao na nilichosikia ni Kama "Vatican na Saud Arabia" (quit different).

In summary; Hiki ndo nilitarajia kukisikia kutoka kwa hawa Nguri wa Hoja duniani;.

1.Uchaguzi wa 28Oct202.
Nilitajia kusikia maswali kama; Kwanini CCM imeishinda kwa asilimia kubwa vile kuliko vyama vingine?
Je baada ya Matokeo Wananchi waliopiga Kura hizo wameridhika na Matokeo Yao au hapana na Kama Ni hapana, Kuna ishara yeyote waliyoionyesha kutokubaliana na walichokichagua( Hapa Wapigiwa kura hawahusiki).
Je baada ya Matokeo wagombea nafasi wa upinzani walioshindwa waliyachukulia je matokeo, Kama Ni ndio sawa na Kama Ni hapana, je Kuna njia zozote za kisheria walizochukua kupinga Matokeo hayo ili kupata haki Yao(ukiondoa ya Matokeo ya urais).

2. Ukandamizwaji wa haki za binadam na Ugaidi;
Nilitarajia kusikia hoja Kama hizi kutoka kwao;
Kwanini msumbuji imeshindwa kuwathibiti Wana mgambo walioweka makazi kwenye nchi yao mpaka Wanasababisha maafa na kukandamizwa kwa haki za binadam nchi jirani Kama Tanzania(Mtwara Kama walivyotaja wao)?. Na Wala siyo kuilaumu Tanzania kisa inapakana na sehemu ambayo magaidi wapo. Nikweli EU hawajui kuwa Msumbuji ni nchi huru na ina mipaka na jeshi lake ambalo haliwezi ingiliwa na jeshi lolote lile pasipo ruhusa?.

3. COVID19.
Nilitegemea kusikia ni, njia gani ilizotumia Tanzania kuondokana na janga la Corona mpaka kufikia hatua ya watu wake kuendelea na maisha yao Kama kawaida bila vifo Wala athari yeyote?
Na wala siyo kulialia kwanini Tanzania haina Corona na tunaipatia pesa, Mara pesa za Corona zimetumikatumika je, Mara Sijui Nini ,
Hapa kwakweli imeonesha wazi kabisa jinsi gani mataifa ya ulaya yalivyo na wivu mkubwa juu ya Tanzania hasa katika suala hili la Covid19.

My take; Tanzania ni nchi yangu na Nina ipenda Sana na Sina shaka na Kiongozi wangu mkuu Yani "JIWE" juu ya kudili na Mabeberu naamini nachokiwaza mimi kuanzia Sasa na kuendelea ndo anachokiwaza Rais wangu. Hizi hoja za Leo niza kupuuza na kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea maana inaonekana watu wenyewe wamejadili huku mioyo yao ikiwa imejaa chuki binafsi na wivu juu ya Tanzania pamoja na kulialia pasipo kuwa na "deep Intelligences".

Na nilichokugundua Tangu tupate Rais jiwe kwelikweli Tanzania imekuwa femous sana ndani na nje ya Mataifa ya Ulaya. Na wanavyotenga muda wao kutujadili namna hiyo kwetu ni faida kubwa Sanaa maana Kupitia wao ndo wana tangaza na soko letu la utalii na kuwafanya watu wengi zaidi kuja Tanzania kujionea uteule wake.

Mfano; Suala la kututangaza juzi Kati kwenye media zao kuwa "Tanzania ndo nchi pekee dunian ambayo haina maambuzi ya Corona kwa takribani wiki46" na leo walivyosema kwenye mkutano wao kuwa, "tunawapa je Msaada Tanzania angali hawana Corona". Hii itaongeza idadi ya watu wengi Sana wa ulaya waliochoka na lockdown kuja kula maisha kwenye Peace land ya Tanzania huku soko letu la utalii likipanda siku Hadi siku.

#Mungu Mlinde Jiwe, Mungu tulinde Watz wote, Mungu ilinde nchi yangu.

#I love my country [emoji1241].
 
Unajua pesa za REA zimetokana na nini wewe??? Au ndo unaaamini kama mnavyodanganywa kuwa ni pesa za ndani??
Kokote zilikotoka haijalishi, nilichotaka ufahamu kwamba US na Ulaya kuzuia vijimisaada vyao si mwisho wa Tanzania kuendelea. Tanzania ina wadau wengi wa maendeleo. Akifunga mlango mmarekani kuna nchi zitafungua.
 
Kokote zilikotoka haijalishi, nilichotaka ufahamu kwamba US na Ulaya kuzuia vijimisaada vyao si mwisho wa Tanzania kuendelea. Tanzania ina wadau wengi wa maendeleo. Akifunga mlango mmarekani kuna nchi zitafungua.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
Kuna mdau gani wa maendeleo anayekuchangia zaidi ya hao????

Unafikiri China mliyekamata Bank yake leo ndo anamsaada???? Sasa subirini muoneee
 
Hakuna Beberu yeyote atakaye mgusa JPM si kwa vikwazo wala adhabu nyingine yoyote. Wote baada ya muda wataendelea kushirikiana na JPM. JPM kwasasa ameibeba Tanzania Mabegani mwake, chini yake Tanzania itaendelea kung'aa na kuwa na nguvu za ushawishi duniani. Ni swala la muda tu wasio elewa wataelewa.
uko sahihi mzee, misaada ni njia kuu wa ukoloni mamboleo, mzungu hana free lunch aisei, anatuambia tusubiri misaada hana maana kabisa. usikubali jirani yako atoe misaada kwenye familia yako, iku siku utajutia.
 
Sijaona hata kilichokufurahisha hapo! Tanzania ni nchi huru, tusipangiane vitu vyakufanya! Ukoloni ulikoma tarehe 9.12.1961!
Unaefurahia hayo, hutokuwa salama kabisa siku yakija mabaya!
 
Back
Top Bottom