Bila kupoteza Muda naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja,
Leo nilitenga muda wa kusikiliza kile kilichokuwa kinajadaliwa na Hawa Viumbe wa "EU" (External affairs), Kama tulivyo taarifiwa juzi katika vyombo vya habari vya kwao huko na baadhi ya nyuzi hapa JF.
Ila Nimesikitika Sana kuwa nilichotarajia kukisia kutoka kwao na nilichosikia ni Kama "Vatican na Saud Arabia" (quit different).
In summary; Hiki ndo nilitarajia kukisikia kutoka kwa hawa Nguri wa Hoja duniani;.
1.Uchaguzi wa 28Oct202.
Nilitajia kusikia maswali kama; Kwanini CCM imeishinda kwa asilimia kubwa vile kuliko vyama vingine?
Je baada ya Matokeo Wananchi waliopiga Kura hizo wameridhika na Matokeo Yao au hapana na Kama Ni hapana, Kuna ishara yeyote waliyoionyesha kutokubaliana na walichokichagua( Hapa Wapigiwa kura hawahusiki).
Je baada ya Matokeo wagombea nafasi wa upinzani walioshindwa waliyachukulia je matokeo, Kama Ni ndio sawa na Kama Ni hapana, je Kuna njia zozote za kisheria walizochukua kupinga Matokeo hayo ili kupata haki Yao(ukiondoa ya Matokeo ya urais).
2. Ukandamizwaji wa haki za binadam na Ugaidi;
Nilitarajia kusikia hoja Kama hizi kutoka kwao;
Kwanini msumbuji imeshindwa kuwathibiti Wana mgambo walioweka makazi kwenye nchi yao mpaka Wanasababisha maafa na kukandamizwa kwa haki za binadam nchi jirani Kama Tanzania(Mtwara Kama walivyotaja wao)?. Na Wala siyo kuilaumu Tanzania kisa inapakana na sehemu ambayo magaidi wapo. Nikweli EU hawajui kuwa Msumbuji ni nchi huru na ina mipaka na jeshi lake ambalo haliwezi ingiliwa na jeshi lolote lile pasipo ruhusa?.
3. COVID19.
Nilitegemea kusikia ni, njia gani ilizotumia Tanzania kuondokana na janga la Corona mpaka kufikia hatua ya watu wake kuendelea na maisha yao Kama kawaida bila vifo Wala athari yeyote?
Na wala siyo kulialia kwanini Tanzania haina Corona na tunaipatia pesa, Mara pesa za Corona zimetumikatumika je, Mara Sijui Nini ,
Hapa kwakweli imeonesha wazi kabisa jinsi gani mataifa ya ulaya yalivyo na wivu mkubwa juu ya Tanzania hasa katika suala hili la Covid19.
My take; Tanzania ni nchi yangu na Nina ipenda Sana na Sina shaka na Kiongozi wangu mkuu Yani "JIWE" juu ya kudili na Mabeberu naamini nachokiwaza mimi kuanzia Sasa na kuendelea ndo anachokiwaza Rais wangu. Hizi hoja za Leo niza kupuuza na kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea maana inaonekana watu wenyewe wamejadili huku mioyo yao ikiwa imejaa chuki binafsi na wivu juu ya Tanzania pamoja na kulialia pasipo kuwa na "deep Intelligences".
Na nilichokugundua Tangu tupate Rais jiwe kwelikweli Tanzania imekuwa femous sana ndani na nje ya Mataifa ya Ulaya. Na wanavyotenga muda wao kutujadili namna hiyo kwetu ni faida kubwa Sanaa maana Kupitia wao ndo wana tangaza na soko letu la utalii na kuwafanya watu wengi zaidi kuja Tanzania kujionea uteule wake.
Mfano; Suala la kututangaza juzi Kati kwenye media zao kuwa "Tanzania ndo nchi pekee dunian ambayo haina maambuzi ya Corona kwa takribani wiki46" na leo walivyosema kwenye mkutano wao kuwa, "tunawapa je Msaada Tanzania angali hawana Corona". Hii itaongeza idadi ya watu wengi Sana wa ulaya waliochoka na lockdown kuja kula maisha kwenye Peace land ya Tanzania huku soko letu la utalii likipanda siku Hadi siku.
#Mungu Mlinde Jiwe, Mungu tulinde Watz wote, Mungu ilinde nchi yangu.
#I love my country [emoji1241].