Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Waambie tumezitumia kuzuia kuenea kwa Corona nchini na sasa maisha yanaendelea. Pesa zao zimetumika vizuri ndomaana hatuna Korona. Wao walitaka waone pesa au Kutoweka kwa Korona?. Roho zinawauma kuna pesa zimetumika na Korona hakuna
 
Safi kabisa jeuri yote kwisha
 
Sawa waendelee tu kujadili....wanaleta Berlin Conference nyingine baadala ya I'll ya 1884
Hay ndio makualiano ya Modern chief Mangugo Tundu Lisu na Modern Karl Peters Robert Amsterdam waliyokubaliaa kwenye Modern Berlin Conference European Union Conference!!!

Chief Mangungo Lisu mtaka kuweka Rehani madini yetu agenda zako hazitafanikiwa mwambie Karl Peters Amsterdam wako
 
Naona wameanza na mambo ya TIN namba sijawaona popote mtumishi awe na tin.
Kisheria kila mtu anatakiwa arejeshe hesabu za mapato TRA. Na ili uweze kulipa ikiwa utakuwa umefikia vigezo lazima uwe na namba ya mlipa kodi.(TIN)

Haki elimu waliwahi kusema.."Kandambili sio Kiatu" simply kwa kuwa ilikuwa haifanyiki au hukujua kama inapaswa kufanyika haimaanishi kuwa Haipaswi Kufanyika.

Kila Mtu lazima alipe Kodi, Kwa Maendeleo Jumuishi.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hongera sana kwa taarifa hii ni very accurate , maana nimesikiliza Dochovele jioni hii wamepita mulemule ulipoandika , haya mataga endeleeni kumuimbia mapambio Jiwe ,tayari kaishaingia kwenye kumi na nane za mabeberu ni suala la muda tu wamnyooshe kwelikweli .
 
Safi kabisa
 
Nyie si nchi tajiri mnaonewa vipi? mbona nyie mnawaonea akina Mdude? shame on you
 
Dada KAYAFA hajakupa miwaya kweli maana hizi akili zimeliwa vibaya sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wajinga nyie,

Mlifikiri unagombaniwa umonitor wa darasa la nne mpaka mnamleta yule mbelgiji?

Umeona wenzenu wa uganda? Wako serious wao hawajibebishi kwa akina Amsterdam kama mnavyofanya nyie humu, wameenda road.

Mpaka 2025 akili zitakuwa zimewakaa sawa wajinga nyie.
 
Muache huyo ka-panic usimuongezee pressure.
 
Suburini wasaka uteuzi waanze kujitokeza kuwajibu EU pasipo kuwa na hoja za msingi zaidi ya propaganda.
Kwa wale waliopigwa chenga na lugha:
Huyu mbunge wa bunge la Ulaya kwa kifupi anasema:' Program ya Shirikisho la Nchi za Ulaya (SNU) kwa Tanzania tangu 2014-2020 ilikuwa imeweka kipa umbele utawala bora, ikiwemo kulinda haki za binadamu, kupiga vita ubaguzi wa ki jinsia, uhuru wa kusema...nk (Yaani misaada iliyotolewa wakati huo ni baada ya kudhaminiwa kuwa hayo yatatendeka). Anaendelea, 'lakini tangu 2015 wameshuhudia mporomoko wa kwenda chini tu wa haki za binadamu na mambo hayo hapo. ' Hatuwezi kuendelea kuamiliana na Tanzania namna hii. Hatuwezi kuendelea na siasa za namna hii. Ni lazima misaada tunayoitoa ifuatiliwe na maswali yaulizwe imetumika vipi? Tulitoas EURO milioni 27 kwa sababu ya janga la Korona. Lakini "nidhamu hii ya sasa' (Angalia anaiita 'regime' na si 'serikali'... kama vile wanavyoziita Syria na Iran!) inatoa maelezo ya ajabu ajabu 'bizzare explanation' (Hiyo ya kusema Mungu ameepusha), na inakataa kabisa kufuata maelekeo ya Shirika la Afya Duniani, WHO, kama vile kutoa idadi na takwimu (statistics) za waathirika, vifo, waliopona….nk..
Nataka nikuulize wewe uliotoa fedha hizo ambazo ni KODI ya wananchi wa Ulaya: 'Chini ya vigezo gani umezitoa? Kitu gani kinaedlea huko Tanzania, unajua? Serikali isiyotaka kushirikiana kwa njia ya kiisaarabu (decent means)…..
Sasa nakutaka unipe majibu. Na kama huna, nakutaka uandike majibu hayo na unipe katika kipindi cha dakika 10 zijazo' ! MWISHO WA UDOKOZI KWA MUHTASARI.

ONGEZO LANGU: Hata kama nina maswali juu ya uongozi wa nchi yetu, hasa hasa inapokuja kwenye upinzani na uhuru na haki za kiraia, sifurahii kabisa Tanzania kuingia katika mzozo na jamii ya Kimataifa. Ninaloomba na kutarajia kwa diplomasia ya nchi yetu ni kuepusha mzozo huo kwa kuzungumza kwa kidiplomasia na weledi, na si kujifanya Nunda na maneno ya kuwa sisi ni sisi! Haikufaa kwa waliokuwa na nguvu kuliko sisi.
 
Nchi inapoingia kwenye msoto ,mwananchi huna pa kukwepea zaidi ya ukimbizini
Nakwenda Zimbabwe🚶🚶🚶
 
Kwa nini wapambe hawamtafsirii jiwe!

Mimi naamini hata hajui kinachoendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…