Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kumbe Tanzania ilikubali msaada wa Euro Mil 27 za mabeberu za Covid-19 September hii. Sasa wanataka kujua kwa nini Tanzania ilipewa msaada huo wakati wamesema Corona haipo. Na pia wanataka kujua zimetumika vipi? Moja ya masharti ya kupewa pesa hizo ni pamoja na kutoa statics za ugonjwa na kufata maelekezo ya WHO ambapo Tanzania hawafati. Ila swali pia kwa serikali yetu kwa nini wanachukua pesa za mabeberu wanaowapiga vita? Au ndio ule msemo usemao ''Baniani mbaya kiatu chake kizuru'' Basi tutakuwa wanafiki. Na kwa nini hata sisi watanzania hatujatangaziwa kama misaada imetolewa na mabeberu? Zaidi ya serikali kutupa wananchi tu picha ya kwamba tuendelee kuwachukia mabeberu.

Angalia hapa chini VIDEO Rais wa Bunge la EU anavyolaani utawala wa awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuwakandamiza watetea haki, wapinzani na kutolinda demokrasia. Hivyo amesema Umoja wa Ulaya utabadilisha siasa yake kuhusu Tanzania ili isipewe misaada moja kwa moja kwa serikali.
Waambie tumezitumia kuzuia kuenea kwa Corona nchini na sasa maisha yanaendelea. Pesa zao zimetumika vizuri ndomaana hatuna Korona. Wao walitaka waone pesa au Kutoweka kwa Korona?. Roho zinawauma kuna pesa zimetumika na Korona hakuna
 
Bunge la Ulaya hivi punde limejadili hali ya kisiasa nchini Tanzania kabla na baada ya uchaguzi, na kuzishauri nchi washirika kupunguza zaidi misaada inayotolewa kwa Tanzania.

Wachangiaji wengi wamependekeza kusitishwa au kupunguzwa kwa misaada inayotolewa na nchi washirika wa EU. Wanahoji nini maana ya misaada yao kama lengo lao la utawala bora halitekelezwi na watawala.

Msaada wa kibajeti uliokuwa unatolewa na EU umesitishwa hadi mwafaka wa kisiasa ufikiwe.

“No budget support until EU Commission sees a fundamental improvement in the political dialogue!” - H. Stausboll.

“We must consider ECONOMIC SANCTIONS TO TANZANIA because of the elections and the TERRORIST ATTACKS in the South of Tanzania and North of Mozambique” -PauloRangel_pt EPP.

“We have had a very difficult relationship with the government of Tanzania. We will reconsider Budget support unless we see a clear direction in the political environment “ - @HStausboll.

“The elections in Tanzania was a travesty of Justice. It was Lukashenko style type of an election. Can we still trust The Tanzania govt with aid?” - Gahler Michael, @Europarl_EN.

Wameshauri kuliko kuipatia serikali ambayo inaweza kuitumia vibaya kufifisha haki za binadamu ni bora kuvipatia moja kwa moja vikundi vinavyojihusisha na kutetea haki za binadamu.

Wamehoji EU kuipatia serikali ya Tanzania Euro 27m kwa ajili ya Korona ambayo serikali inasema Tanzania haina Korona.

Mkataba wetu na EU.

View attachment 1629980
Safi kabisa jeuri yote kwisha
 
Sawa waendelee tu kujadili....wanaleta Berlin Conference nyingine baadala ya I'll ya 1884
Hay ndio makualiano ya Modern chief Mangugo Tundu Lisu na Modern Karl Peters Robert Amsterdam waliyokubaliaa kwenye Modern Berlin Conference European Union Conference!!!

Chief Mangungo Lisu mtaka kuweka Rehani madini yetu agenda zako hazitafanikiwa mwambie Karl Peters Amsterdam wako
 
Naona wameanza na mambo ya TIN namba sijawaona popote mtumishi awe na tin.
Kisheria kila mtu anatakiwa arejeshe hesabu za mapato TRA. Na ili uweze kulipa ikiwa utakuwa umefikia vigezo lazima uwe na namba ya mlipa kodi.(TIN)

Haki elimu waliwahi kusema.."Kandambili sio Kiatu" simply kwa kuwa ilikuwa haifanyiki au hukujua kama inapaswa kufanyika haimaanishi kuwa Haipaswi Kufanyika.

Kila Mtu lazima alipe Kodi, Kwa Maendeleo Jumuishi.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Amani iwe nanyi tena wadau!!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.

Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi Kwa nini walitoa hela za ku support harakati za covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati TanZania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free

4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwa nini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?????

5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa serikali.


Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu
Mkuu hongera sana kwa taarifa hii ni very accurate , maana nimesikiliza Dochovele jioni hii wamepita mulemule ulipoandika , haya mataga endeleeni kumuimbia mapambio Jiwe ,tayari kaishaingia kwenye kumi na nane za mabeberu ni suala la muda tu wamnyooshe kwelikweli .
 
Amani iwe nanyi tena wadau!!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.

Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi Kwa nini walitoa hela za ku support harakati za covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati TanZania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free

4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwa nini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?????

5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa serikali.


Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu
Safi kabisa
 
Wazungu wanapaswa kuelewa kuwa Tanzania tulipambana na Corona na tukaishinda hivyo msaada tuliopewa na EU ulikuwa ni halali yetu.

Nani asiyejua hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali kupambana na Corona ikiwemo social distancing, kuvaa barakoa, kuweka sehemu za jamii kunawa mikono, kufanyia kazi nyumbani, shule na vyuo kufungwa nk nk.

Wazungu watafute sababu nyingine za kutubania misaada lakini hili la Covid 19 wanatuonea bure.

Maendeleo hayana vyama!
Nyie si nchi tajiri mnaonewa vipi? mbona nyie mnawaonea akina Mdude? shame on you
 
Dada KAYAFA hajakupa miwaya kweli maana hizi akili zimeliwa vibaya sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wajinga nyie,

Mlifikiri unagombaniwa umonitor wa darasa la nne mpaka mnamleta yule mbelgiji?

Umeona wenzenu wa uganda? Wako serious wao hawajibebishi kwa akina Amsterdam kama mnavyofanya nyie humu, wameenda road.

Mpaka 2025 akili zitakuwa zimewakaa sawa wajinga nyie.
 
Nafikiri unaongea tu kwa kufuata mkumbo, sidhani kama unafahamu hata maana ya neno "Sovereignty".

How can you claim sovereignty when you can't stop roaming around with an empty bowl begging for food?

A sovereign state is the one that is capable of governing herself without depending on the handouts from a foreign country, Tanzania deserves no that status.
Muache huyo ka-panic usimuongezee pressure.
 
Suburini wasaka uteuzi waanze kujitokeza kuwajibu EU pasipo kuwa na hoja za msingi zaidi ya propaganda.
Kwa wale waliopigwa chenga na lugha:
Huyu mbunge wa bunge la Ulaya kwa kifupi anasema:' Program ya Shirikisho la Nchi za Ulaya (SNU) kwa Tanzania tangu 2014-2020 ilikuwa imeweka kipa umbele utawala bora, ikiwemo kulinda haki za binadamu, kupiga vita ubaguzi wa ki jinsia, uhuru wa kusema...nk (Yaani misaada iliyotolewa wakati huo ni baada ya kudhaminiwa kuwa hayo yatatendeka). Anaendelea, 'lakini tangu 2015 wameshuhudia mporomoko wa kwenda chini tu wa haki za binadamu na mambo hayo hapo. ' Hatuwezi kuendelea kuamiliana na Tanzania namna hii. Hatuwezi kuendelea na siasa za namna hii. Ni lazima misaada tunayoitoa ifuatiliwe na maswali yaulizwe imetumika vipi? Tulitoas EURO milioni 27 kwa sababu ya janga la Korona. Lakini "nidhamu hii ya sasa' (Angalia anaiita 'regime' na si 'serikali'... kama vile wanavyoziita Syria na Iran!) inatoa maelezo ya ajabu ajabu 'bizzare explanation' (Hiyo ya kusema Mungu ameepusha), na inakataa kabisa kufuata maelekeo ya Shirika la Afya Duniani, WHO, kama vile kutoa idadi na takwimu (statistics) za waathirika, vifo, waliopona….nk..
Nataka nikuulize wewe uliotoa fedha hizo ambazo ni KODI ya wananchi wa Ulaya: 'Chini ya vigezo gani umezitoa? Kitu gani kinaedlea huko Tanzania, unajua? Serikali isiyotaka kushirikiana kwa njia ya kiisaarabu (decent means)…..
Sasa nakutaka unipe majibu. Na kama huna, nakutaka uandike majibu hayo na unipe katika kipindi cha dakika 10 zijazo' ! MWISHO WA UDOKOZI KWA MUHTASARI.

ONGEZO LANGU: Hata kama nina maswali juu ya uongozi wa nchi yetu, hasa hasa inapokuja kwenye upinzani na uhuru na haki za kiraia, sifurahii kabisa Tanzania kuingia katika mzozo na jamii ya Kimataifa. Ninaloomba na kutarajia kwa diplomasia ya nchi yetu ni kuepusha mzozo huo kwa kuzungumza kwa kidiplomasia na weledi, na si kujifanya Nunda na maneno ya kuwa sisi ni sisi! Haikufaa kwa waliokuwa na nguvu kuliko sisi.
 
Nchi inapoingia kwenye msoto ,mwananchi huna pa kukwepea zaidi ya ukimbizini
Nakwenda Zimbabwe🚶🚶🚶
 
Back
Top Bottom