Bunge la Ulaya kwa kauli moja limeazimia kuifutia Tanzania misaada na mikopo yote ambayo imeomba kwenye Umoja wa Ulaya (EU) na mashirika yake.
Moja ya misaada mikubwa ambayo Tanzania imefutiwa ni ule wa £626M (sawa na TZS Trilioni 1.6) ambazo tumekuwa tukipewa kila mwaka tangu 2014 kwa ajili ya kuimarisha demokrasia, utawala bora, kujenga miundombinu na kusambaza nishati ya umeme vijijini.
EU imefikia uamuzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Pia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola na madai ya serikali kushindwa kudhibiti matukio ya ugaidi kusini mwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya nje wa bunge la Ulaya (Chairman of the European Parliament Foreign Affairs Committee), David McAllister amesema pamoja na kuinyima Tanzania msaada huo wa TZS Trilioni 1.6 pia EU inafikiria kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi (Economic sanctions) ikiwa ni pamoja na kuizuia Tanzania kufanya biashara na nchi yoyote ya Ulaya.
McAllister amesema vikwazo hivyo vikiwekwa havitaondolewa mpaka pale serikali ya Tanzania "itakapojicommit" kwa maandishi kuheshimu demokrasia, kuruhusu ushindani wenye usawa wa vyama vya siasa na kulinda haki za binadamu. Mjadala wa kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi bado unaendelea.
BUNGE LA ULAYA LIELEZWE BILA KUPEPESA MOJA KWA HERUFI KUBWA KWAMBA: TANZANIA NI TAIFA HURU KWA ASILIMIA MIA MOJA na kwamba kimsingi ina haki zifuatazo:-
1) Haki na Demokrasia:
Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:
Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.
Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."
Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?
Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo £626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazi walitakiwa watulipe kama kodi.
Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?
3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:
Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.
(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.
(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.
(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.'
Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.
Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye
mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana." Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?
4) Soko la Umoja wa Ulaya.
Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.
Ushauri Wangu.
Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."
Cha Kufanya:
- Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
- Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.
Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.
Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.
Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.
mkali@.co.uk
19/11/2020