3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 5,350
- 15,426
Mbona kuna uzi mwingine unasema hawajafuta kwa maelezo ya balozi wa Tanzania Ubelgiji na kwamba mapendekezo hayo ni ya wabunge wa5 tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona kuna uzi mwingine unasema hawajafuta kwa maelezo ya balozi wa Tz Ubelgiji na kwamba mapendekezo hayo ni ya wabunge wa5 tu
Hilo azimio liko wapi??Bunge la Ulaya kwa kauli moja limeazimia kuifutia Tanzania misaada na mikopo yote ambayo imeomba kwenye Umoja wa Ulaya (EU) na mashirika yake.
Moja ya misaada mikubwa ambayo Tanzania imefutiwa ni ule wa £626M (sawa na TZS Trilioni 1.6) ambazo tumekuwa tukipewa kila mwaka tangu 2014 kwa ajili ya kuimarisha demokrasia, utawala bora, kujenga miundombinu na kusambaza nishati ya umeme vijijini.
EU imefikia uamuzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Pia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola na madai ya serikali kushindwa kudhibiti matukio ya ugaidi kusini mwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya nje wa bunge la Ulaya (Chairman of the European Parliament Foreign Affairs Committee), David McAllister amesema pamoja na kuinyima Tanzania msaada huo wa TZS Trilioni 1.6 pia EU inafikiria kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi (Economic sanctions) ikiwa ni pamoja na kuizuia Tanzania kufanya biashara na nchi yoyote ya Ulaya.
McAllister amesema vikwazo hivyo vikiwekwa havitaondolewa mpaka pale serikali ya Tanzania "itakapojicommit" kwa maandishi kuheshimu demokrasia, kuruhusu ushindani wenye usawa wa vyama vya siasa na kulinda haki za binadamu. Mjadala wa kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi bado unaendelea.
BUNGE LA ULAYA LIELEZWE BILA KUPEPESA MOJA KWA HERUFI KUBWA KWAMBA: TANZANIA NI TAIFA HURU KWA ASILIMIA MIA MOJA na kwamba kimsingi ina haki zifuatazo:-
1) Haki na Demokrasia:
Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:
Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.
Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."
Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?
Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo £626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazi walitakiwa watulipe kama kodi.
Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?
3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:
Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.
(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.
(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.
(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.'
Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.
Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana." Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?
4) Soko la Umoja wa Ulaya.
Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.
Ushauri Wangu.
Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."
Cha Kufanya:
- Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
- Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.
Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.
Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.
Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.
mkali@.co.uk
19/11/2020
Wanayo Akiba ya chenji pesa za uchaguzi tokea China chenji ya ununuzi Ndege michango kwenye mikataba ya siri ya madini watazikusanya kisha kuwahadaa watanzania kuwa pesa za corona zipo na hazijatumika ili wale watanzania wepesi wa kuamini ujinga wa CCM waamini pesa za corona ipo imetulia haijapigwa na wajanja wa huko CCMhili ni pigo kwa Serikali ya CCM kwamba haiaminiki tena mbele ya macho ya mataifa... hii ni mbaya sana, sana. Sasa hawakawii kuitisha auditng kuona hizo pesa zilitumikaje - hili ni lao waache wapambane!! sisi tunatibu majereha kwa sasa, watuache.
Alishasema yeye huwa hashauriwi na wala hapangiwi.Kwa vyovyote itakavyo Kuwa wachumia tumbo na walio mshauri vibaya Rais ndio tutalala nao mbele. Hatuwezi teseka ilihali Tunajuwa Rais anawashauri
.... balozi kaingiza propaganda za kisiasa badala ya ukweli!Hii habari si imekanushwa na balozi wa Tanzania pande za huko ama!!??
Ni propaganda tu. Hata Jana Sirro alikuwa anaongea na jumuiya ya Ulaya huku akizunga kuongea na waandishi wa habariMbona kuna uzi mwingine unasema hawajafuta kwa maelezo ya balozi wa Tz Ubelgiji na kwamba mapendekezo hayo ni ya wabunge wa5 tu
Watanzania wameiepuka corona kwa kunywa limau tangawizi kupiga nyungu kwa bidii siyo vinginevyo, lakini CCM wanachukua pesa za corona na kuchukuchia kimya kimya mpaka sasa wameanza kuumbuka na nina imani muda huu CCM wapo busy kutengeneza majibu ambayo wajinga watupu ndiyo watayakubaliMsalaba huo abebeshwe Nduhai na Magufuli. Wao ndio waliopanga na kutekeleza mambo ya kipuuzi kisha kuahangilia upuuzi ule.
Ha ha ha ha ha hawacha beberu ampande mbuzi jike sasa, hakuna namna lazima amtie mimba safari hii