Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Amani iwe nanyi tena wadau!!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.

Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi Kwa nini walitoa hela za ku support harakati za covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati TanZania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free

4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwa nini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?????

5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa serikali.

Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu

Amani iwe kwako @Lord denning!!

Bunge la EU wamepanick na kuamua kukutumia muda wao kuijadili Tanzanian jinsi ilivyoshtuka kuhusu uharamia wao wa vibaraka wao😁😁😁

Wewe nenda kawaambie hivi;

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania
- Waambie Tanzania haina hali mbaya kuliko DRC, Libya, Somalia.... waambie waijadili vizuri sana Tanzania na wajiulize kwanini rais John Pombe Magufuli alishauri Africa wapewe debt relief badala ya ile mikopo ya walimwengu. Waambie pia tunajua wanatishia kuondoa wanachokiita misaada kwa sababu haikua misaada ila ilikua kishawishi cha kutufanya kuendelea kuwa watumwa wao

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania
- Waambie wajiangalie kwanza wao na vibaraka wao kwa jicho makini zaidi. Kuhusu kufuatilia hali ya kukandamizwa kwa haki za binadamu waanze na wale vibaraka wao waliokua wanawaahidi vijana vyeo, waliokua wakiwapa pombe na pesa ili wapigane na askari na kuchoma moto mali za watu kwa kisingizio cha haki na demokrasia. Waambie pia waishauri Belgium kuanza kuwalipa Congo fidia kwa mauaji na mateso ya waafrika yaliyofanywa na mfalme wao King Leopold II. Wasifikiri tumewasahau fisi ni fisi hawezi kuwa kondoo hata siku moja

3. Wamehoji hadi Kwa nini walitoa hela za ku support harakati za covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati TanZania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free
- Waambie mpango wao wa kututesa na kutuua kwa njaa, kukosa huduma na stress kwa kisingizio cha COVID ulifeli sababu tuna serikali makini. Waeleze kwamba pamoja na kuwanyima VISA kutoka nje ya EU na nchi nyingi chache za America na Asia tunajua kabisa kwamba wana mpango wa kuwanyima raia wao haki kwa kuwawekea masharti magumu kuhusu kuja na kuwekeza Tanzania.

4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwa nini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?????
- Waambie walitakiwa kufanya hayo kabla pesa haijatoka kwani sisi tunasema kiendacho kwa mganga hakirudi!

5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa serikali.
- Washauri watoe misaada kwa vyama vya Siasa kupitia account Amstadam na Tundu hukohuko ulaya ila wajue tuu kwa Tanzania ya sasa hiyo pesa pesa sio ushindi. Hata wafanyaje tumeshawashtukia na hawawezi toboa hapa tanzani

Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂
- Ukipata updates tuletee

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu
- Subiri hapohapo utawaona wakijiandaa🤣🤣🤣

Hao ni mbwa mwitu waliovaa ngozi za kondoo kamwe hatuwezi wasahau kwa ukatili wao juu ya mtu matusi
Screenshot_20201118-222615.jpg
 
Hovyo! Kabisa. Mazuzu wanaojitekenya na kujichekesha wenyewe wanatia kichefuchefu!
Wanashindwaje kujua km hatua zozote za kuihujumu Tanzania na raia wake, zitamuathiri hata yeye na jamaa zake, kwa namna moja ama nyengine!

Wakati huu ambapo tunajitambua kuwa maendeleo yetu lazima yaletwe na jitihada za sisi wenyewe, badala ya kutegemea bakuli la wafadhili ni muhimu kila raia kuunga mkono jitihada hizo, na kuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wetu kama taifa na utashi wetu kama binaadamu. Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako!
Uchaguzi ungekuwa huru na wa haki haya yote yasingekuwepo. Tuambie kwanza kutetea uhuru gani?.
 
2025 magufuli ndo anampigia anaefuata kampeni kama kikwete alivompigia magu! sasa 2025 ebu rikisha vizuri kwanza 2035 kuanzia uko tunaweza kuja kidogo kujadili watakua wanasemaje
Hawa jamaa ni wajinga kweli mkuu,

Hawajui kama hata hiyo misaada wazungu hutoa akitegemea return.
 
Hakuna neno, tunajua rafiki yetu wa kweli na wa kihistoria China ata cover the deficit
 
Endelea tu kukifurahisha. Nakwambiaje jiandae kuona majina ya viongozi wenu takotolew na ICC kuwa wanachunguzwa
kamanda uchwara, wacha nkuelimisha ICC tayar imeshawekewa vikwazo vya kiuchumi na marekani juzi juzi apa! china hawataki kuiskia kabisa, kwahio sasa you make sure you fund it
 
Wewe ni jinga kweli toka lini mzungu akakupa msaada bila kuwa na interests zake.
Hizi elimu za kuunga unga zitakuja kuligharimu Sana taifa letu.
Kwahiyo wewe unaposikia tanzania imepata msaada akilini mwako unaelewa kuwa ni kama msaada wa chumvi unaopewa na jirani yako
Yale mamillion ya uero ya covid19 mliyapokea kama hisani, msaada wa sabuni na chumvi au mlipokea mkidhani zinatoka kwa kaguta?
 
Watunyime tu mahela yao.. mtu fulani kajua kutuaibisha kimataifa. Dunia nzima inatucheka. Tukiwa kwenye umaskini mkubwa ndio Watanzania watashtuka kuwa huyu jamaa na ndugu zake (watoto wa dada, etc) sio.
 
kamanda uchwara, wacha nkuelimisha ICC tayar imeshawekewa vikwazo vya kiuchumi na marekani juzi juzi apa! china hawataki kuiskia kabisa, kwahio sasa you make sure you fund it
Hujui kuwa EU ndo funder wa ICC na Kamisheni ya UN ya haki za binadamu. Mbaya zaidi hao wote wametoa tamko dhidi ya ufedhuli wenu mliofanya mwaka huu. Sasa jiandaeni tu
 
Hakuna Beberu yeyote atakaye mgusa JPM si kwa vikwazo wala adhabu nyingine yoyote. Wote baada ya muda wataendelea kushirikiana na JPM. JPM kwasasa ameibeba Tanzania Mabegani mwake, chini yake Tanzania itaendelea kung'aa na kuwa na nguvu za ushawishi duniani. Ni swala la muda tu wasio elewa wataelewa.
Let wait. time will tell kama uliyoandika hapa yatatimia.
 
Kumbe Kuna manyumbu hadi wakizungu, Kwani Corona haikuwepo TZ? Corona ilikuwepo ila iliisha
 
Huyu Lord dening anatia huruma sana.

Nlimuonya kwamba baada ya uchaguzi ajiandae kisaikolojia ila naona ameanza kuinesha madhara ya kile nilichokuwa nasema
 
Back
Top Bottom