Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Yule mwenyekiti yuko bold vibaya sana. Amenufurahisha pale aliposema tunawezaje kutoa hela za walipa kodi wa ulaya kwa mtu ambae anadidimiza Haki za binadamu!!
Wewe utanyooka tu na mabeberu wako. Watz hatutishiwi nyau sisi! Mtabadilisha gia angani in vain!
 
Wazungu wapumbavu na wasio na akili . Hawakuona juhudi za kupambana na corona wakati mikono ilikuwa inaoshwa mpaka stendi za Daladala. Wanafikiri vitendea kazi vile vilitoka wapi? Hoja za tahira Lissu mwishowe zitawaumbua.
 
Uzuri ni kwamba ,ukiwasifia au kuwazomea hao wapuuzi wanaotumia pesa zao kututawala,madhara tutapata wote hasa sisi wa chini,huyo magufuli hatoathirika na lolote.

Tutaumia sisi watu wa kawaida tu,kwahiyo hapo wewe shangiria au zomea ila hali itatukumba wote
 
Nenda waambie bado tunauguza wagonjwa
 
Upinzani unaotoka nje kila inapoletwa hoja ya maana bungeni kushindwa ulivyoshindwa sio jambo la ajabu.

Upinzani unaosusa kijinga tu kupigwa chini na wananchi lilikuwa ni jambo la wakati tu.

Magufuli alieleweka kwenye kampeni hao wazungu wanakariri maisha wakiongozwa na ego ya kujiona wao ndio binadamu wa kwanza kwa ubora.
Hata kama...bado tunahitaji vichwa vichache vya kupiga kelele.....sio 100%!
 
Waliokuwa wanamiliki magenge ya watu wasiojulikana walidhani watatawala nchi kwa njia za kimafia ,hadi umafia mkafanya kwenye uchaguzi na kuwapitsha wabunge wote wa CCM, yaani Mungu hamfichi mwovu.

Mmekatwa misaada yote mdai mnaweza kujitegemea covid tu mmeiba hela za watu.

Mtawekewa vikwazo vyote,shughuli zote zimefungwa ,viwanda vinavyotegemea hela za nje vitakufa,kodi mtapandisha na bado kuendesha shughuli za serikali zitakuwa ngumu ,hao askari walikatwa posho na mishahara haitoki mnakuja kung'olewa tu kirahisi kama Mugabe mnawekwa pembeni
 
Kumbe Serikali yetu ilipokea pesa za msaada wa Covid wakati sisi hatuna Corona, sasa watuambie hizo pesa zilipelekwa wapi? na kwanini tukawadanganya wazungu wakatupa pesa wakati sisi ni donor kantre.

Hali yetu huko nje ni mbaya, sasa hilo halina mjadala, sijui tutaweza vipi kuishi kama kisiwa, wakakataa kuwaacha Chadema waende bungeni, sasa wana msalaba mkubwa zaidi wa kuubeba aheri ya wapinzani wangekuwa bungeni.

Zile calculations walizopiga Ndugai na Magufuli kabla ya uchaguzi mkuu zimefeli miserably.
Wakuambie wewe bweg kwa kigezo gani? Lakini si ni nyinyi mlikuwa mnatangaza kuwa corona inaua sana watz mpaka wanazikwa usiku? Labda walifuata maneno yenu kutoa msaada huo. Rais wetu hukumsikia alikataa mikopo yao akasema kama wanataka wasamehe madeni
 
Mpaka Leo najiuliza magufuli aliogopa nini kwenye uchaguzi mpaka kuchafua uchaguzi kiasi kile.?
Yaani Bora wale waliokamatwa na zile kura feki wangefunguliwa mashtaka.kidogo ingekuwa afadhali.lakini mnawalinda kwanini mnawalinda?
Tulikuwa tunataka ushindi wa tsunami na si kimbunga cha kawaida.
 
Wazungu wapumbavu na wasio na akili . Hawakuona juhudi za kupambana na corona wakati mikono ilikuwa inaoshwa mpaka stendi za Daladala. Wanafikiri vitendea kazi vile vilitoka wapi? Hoja za tahira Lissu mwishowe zitawaumbua.
Mmenyolewa kiduku. Bado
 
Wasalaam!

Declaration of Interest, mimi sio mwanachama wa chama chochote kile hapa Tanzania, Ni mtanzania wa kawaida na muumini wa demokrasia, na usawa kwa ujumla!

Moja kwa moja kwenye mada, Kuna taarifa zipo na zinanea Sana kwenye mitandao kuwa umoja wa nchi za ulaya kwa pamoja kupitia bunge lake, wamedhamiria kuifungia Tanzania kutopata mikopo na misaada waliyokuwa wanatupatia hapo awali , hii inaelekea na kutuwekea vikwazo vya kiuchumi(economic sanction)!!!

Tujadili Kama taifa, je Ni athari zipi tutakumbana nazo ? Tulijiandaa kwa hili ? Au tupo uchumi wa kati Hakuna shida ?

Pia watu wengi (hususani ) upinzani inaonekana hili jambo wamelipokea kwa shangwe kubwa, kwa maneno mengine wamelifurahia., Lakini madhara Yake Ni makubwa huko tuendako(siku zijazo)

Inakuwaje baadhi ya watu wanafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo ama kunyimwa mikopo ? Ni kukata tamaa ama Ni kukosa uzalendo ? Au Ni Bora liwalo na liwe ? Kwamba watakaoumia Ni wote , wanaccm na wasio wanaccm pamoja na wasio upande wowote ?

Mods tafadhali msiunganishe huu Uzi na Uzi mwingine !
 
Jumuiya ya ulaya ndio unatolea mfano wa hii jumuiya dhaifu ya East Afrika? Hii jumuiya iliyoshindwa hata kuwa na sarafu ya pamoja zaidi ya miaka kumi? Umeishiwa mifano nadhani.
Tanzania tuna Mungu tulishirikisha viongozi wa dini kubwa waongee na Mungu kuwa anataka nchi raisi ikabidhiwe kwa mashoga na wasagaji wa ndani au wa nje au watetea ushoga na usagaji wawe CCM, chadema etc au wawe kawe au ubelgiji nk? Akakataa
 
hata kama. vikwazo vije tu. sisi miafrika ndivyo tulivyo hatuwez kujitawala mpaka tuchapwe.

hatutaki kutawaliwa kijima kimabavu. potelea pote wananchi tutasimama na mabeberu
Labda kama ww ni mu EU. Ila kama ni Mtanzania, simama na nchi yako.
 
Nyerere alisha wahi kurudisha msaada wa fedha na kukataa misaada mingine kutoka Jumhuri ya Shirikisho la Ujerumani baada ya kupewa sharti la kuvunja uhusiano na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani.

Alishawahi rudisha fedha za misaada pia kutoka Uingereza kesho yake tu baada ya Uingereza kuipa Tanzania mwezi mmoja kufuata masharti yao huku wakitishia kufuta misaada.



Baada ya muda wakarudi wenyewe.

Baada ya uchaguzi wa 2015 na Zanzibar matokeo kufutwa, si waliojitoa tena kwenye misaada ikiwemo Marekani. Mwaka mmoja mbele, wakarudi.
20201119_202550.jpg
 
Mkuu haya mambo ni madogo sana. Nyerere alifukuza mabalozi wa huko huko Ulaya kwa akili zao za kikoloni za kipumbavu.

Huwezi kuipangia nchi huru ifanye nini na isifanye nini. Magufuli kiburi anacho cha kutosha tu.
Bukililoooooo lo! Bado uko katika Enzi za Nyerere! Amka! International relations and world politics zimegeuka sana. Exactly, tangu mauaji ya Rwanda imeamulika kuwa hii 'haki ya kutoingilia' nchi yeyote ndiyo ilifikisha huko. Hivi leo, 'jamii ya kimataifa' ina haki ya kujiingiza pale inapoona dalili za udikteta na ufashisti zinachomoza…..hawangojei tena ifikie kama Rwanda. Soma kitabu cha Kofi Anan 'The right of intervention'
 
Wewe unaleta nadharia na mimi ninakwambia kwa mujibu wa sheria...

Watanzania tuna mambo sana..Mbona tukisafiri ughaibuni tunakuwa Subject to Paying tax na hatulalami..

Ni takwa la kisheria kupeleka taarifa zako za mapato TRA. Wao ndio watakwambia kama unapaswa kulipa kodi au hapana.. wakisha kukukagua.

Ili uweze kufanya hilo, au kutimiza takwahilo kisheria inahitaji kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi.

Leo unaweza kuwa huna mapato mengi ya kutosha kukufanya ulipe kodi kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoendesha TRA ila we hope for the best kesho utafanikiwa na itakubidi ulipe kodi.

Swala indirect na direct hilo sioni linaingia wapi hapa.
Ukijua aina za Kodi utajua
 
Ngoma inogile!

Hapo pia kuna uwezekano wa nchi moja moja kuja na maamuzi yake mbali na yale yatayokubaliwa na EU.

Bado US nao kukamilisha shughuli.

Sitashangaa Benki ya Dunia nayo ikasitisha kutoa mikopo.

Sasa itakuwa ni zamu yao kuandamana kwenda Ulaya na Marekani kutafuta suluhu.

Kweli kadri giza linavyozidi, ndivyo nuru inakaribia.

Je, kuna watu watapigwa chini katika kutafuta suluhu na kuridhisha wahisani?Tusubiri.

NB:Media za kibongo haziwezi kutangaza hizi habari, na hata wakitangaza, basi itakuwa ni kwa kugusigusia tu tena kwa uoga mwingi-ndio tulipofika na sio

Amani iwe nanyi tena wadau!!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.


View attachment 1630138

Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi kwanini walitoa hela za ku support harakati za Covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free

4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwanini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?

5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.


Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.

Soma pia > https://www.jamiiforums.com/threads...4-5-za-michango-ya-covid-19-zimeliwa.1786433/
Jambo limezua jambo
 
Wazungu wamekuwa washirika muhimu wa maendeleo kwa miaka mingi, tusiwachukulie poa tujibu hoja zao.
 
Back
Top Bottom