Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Hawa makolo wanatuharibia mpira wetu kwa tabia za ajabu ajabu
 
Mwanzo Mwamuzi huyo Japheth Smarti alidai kua "Alihisi" kua Mkombozi alitoa lugha chafu... Pia alidai "huenda" alimpiga kibao Ateba hivo hakua na namna zaidi ya kumtwanga Kadi nyekundu "umeme" Ili iwe fundisho [emoji23]

Kumbuka pia Mwamuzi huyo Japheth Smarti aliwahi kumalizia mechi kati ya Simba na Coastal Union huku mchezaji wa coastal akiwa kwenye move ya kwenda kufunga goli hali iliyozua taharuki na kupelekea baadhi ya wachezaji kuangua vicheko uwanjani...

Soma hapa... Refa amepiga filimbi ya kumaliza mpira baada ya kuona Simba SC wanataka kufungwa goli nyingine
Ligi yetu ina ujinga ujinga mwingi sana,afu msimu huu maujinga yanataka kuzidi

Nisingekuwa na kibanda umiza nisingekuwa naangalia huu ujinga
 
Hii milio inatokea pande zipi mbona kama volume inaongezeka? Huyo mwamuzi alikaushia kadi nyekundu zingine walau mbili zaidi dhidi ya wachezaji wa Namungo. Hilo hamtaongelea.

Hii siyo mara ya kwanza kufutwa kwa kadi baada ya mechi. Embu tujikumbushe kadi nyekundu ya Lameck Lawi katika mechi ya Coastal Union vs Yanga.

Ubaya Ubwela.
 
Ilikuwa uchezeshaji wa hovyo sana ila binafsi niliwashangaa kina Mbwaduke na Muro maana walikuwa upande wa refa hata kwenye matukio ya hovyo kabisa
 
Ivi walee wazee wa Simba walisema wataamia Burundi mbona wapo kimya sana siku izi??.
 
Ilikuwa uchezeshaji wa hovyo sana ila binafsi niliwashangaa kina Mbwaduke na Muro maana walikuwa upande wa refa hata kwenye matukio ya hovyo kabisa
Washapewa "kitu kidogo" watasema nn? Wachambuzi wote walimpongeza refa
 
Ligi inazidi kunoga, Kila mtu ashinde anavojua...

Kamati ya Masaa 72 imefuta kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi, katika mchezo dhidi ya Simba SC. Uamuzi huu umefikiwa baada ya kamati kupitia kwa kina ripoti ya mwamuzi na kulinganisha na picha za video za tukio husika.

Baada ya uchunguzi, kamati imebaini kuwa maelezo ya mwamuzi hayalingani na kile kilichoonekana kwenye video, hivyo kadi hiyo imeonekana kuwa batili. Kutokana na uamuzi huu, Mukombozi hana hatia yoyote na atakuwa huru kuendelea kuitumikia Namungo kwenye michezo inayofuata.View attachment 3246118
Mwamuzi amepewa adhabu gani?
 
Back
Top Bottom