OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Moja kati ya sherehe zake akiwa hai
Wengi wetu tumeona video na picha zilizosambaa za tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.
Kwa mujibu wa shuhuda ambae pia ni Rafiki, Kijana aliyepigwa risasi na kufariki anaitwa Gift na alikua amekaa jirani na Alex na alisimama kumtuliza Alex baada ya kuona ameanza kutishia Watu kwa bastola yake, amesema Shuhuda huyu.
“Gift ni Kijana mwenzangu tukifanya kazi Ofisi moja, alikua ana muomba Alex asipige risasi kama vile na kupoteza amani, yani kitendo cha Gift kumsemesha yule Jamaa imekua kama kosa aligeuka akammiminia Gift risasi nyingi kama mbuzi, Gift kuona vile akakimbia lakini akaishiwa nguvu hatua chache tu”
“Tulishindwa kutoa msaada kwa Gift kwa sababu Jamaa mwenye Bastola (Alex) alikua kama amevurugwa Shetani kama amemuingia anageuka anaangalia nani mwingine ampige risasi.
My Take
Nimeambiwa jamaa Alex alipewa kibali cha kutumia bastola miezi kama mitatu iliyopita. Ni dhahiri kwamba kamati haikufanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa kibali. Tukio linaonyesha huyu mtu ana shida kichwani na mwepesi kuvurugwa. Kamati ya Ulinzi iwajibishwe