Kambi ya Jeshi Gongo la Mboto ihamishwe kijengwe kituo cha basi

Unaongea mambo ya zamani sana zama za vita vya Kagera.

Huu ndio ujinga na hoja za kipuuzi mnazotumia kuitawala Zanzibar kimaguvu sasa hivi mpaka mtu wa Mkuranga anakuwa Rais Zanzibar wakati Wazanzibar wenyewe wapo.
Hujui unachoongea.
 
Wewe ndio hujui lolote, ndio mnaowadanganya watu eti Zanzibar ni muhimu kwa usalama wetu wakati sasa hivi unaweza kushambuliwa kutokea mbali.
Sio Zanzibar tu.... Comorros na Seyschelles zote ni muhimu kwa usalama wetu.

Kama hujui umuhimu wa kuwa macho na majirani, nenda Eastern DRC ukaone kinachoendelea.
 
Amani inalevya sana. Kwa vile watu hawajaona au kushudia vita Dar es Salaam, sasa wana pendekeza kambi za jeshi zilizoko hapa hazina umuhimu hivyo zihamishwe.
 
Waende Misri (Masri) wakajifunze jeshi lao limetumia njia zipi kumiliki uchumi mkubwa?

Mfano pale Victoria kuna Masri Military detachee zile ni appartment zinamilikiwa na jeshi la Masri, huwa kukuta fremu kwenye base zao Masri.

Hapa ieleweke hatukatai jeshi letu kumiliki uchumi, lakini siyo uchumi wa wa fremu.

Binafsi nyumba yangu ipo mtaa mkubwa wenye movement lakini nimekataa ujinga wa kugeuza makazi kuwa na fremu za maduka, wajinga wengi huwa wananishauri kuweka fremu lakini nawajibu hapa ni residence siyo cormecial premises.
 
Mkitaka kujua umuhimu wa Kambi za Jeshi katika mkoa muhimu ambao ni Lango la Tanzania ... Fanyeni zihame
Nafikiri kambi hazina shida, bali shida ipo kwa watu wa mipango miji hawana maono ya mbali
Jeshi lilipaswa kutengewa eneo la kutosha kiasi kwamba inakua ngumu kufika kwenye ina core ya jeshi
 
Mbele Kituo Cha Mwendokasi Huoni Fremu Zetu Kuzunguuka Kikosi Chote
 
Kwa tuliopo Dar kitambo hizo kambi zilikuwa maeneó sahihi, lakini sasa hivi kambi zote zimezingukwa na makazi mji umepanuka sana.

Kambi zenye sifa ya kubaki mjini ni Air wing na Navy peke yake. Angalau na kambi ya Twalipo.
 
Wananchi ndio wanalifuata jeshi, uliza wenyeji kati ya kambi na wao nani alitangulia kuwepo..?

Hoja ya kuweka frame kwenye maeneo ya jeshi sio kosa ila wangekusanya hela waweke miradi mikubwa kama mahoteli, malls
 
Rubbish
 
Nakushauri nenda pale gongo la mboto halafu omba kuonana na CO wa pale then mueleze haya maneno atakusikiliza maana nawajua wanajeshi ni watu waelewa sana. Tafadhali sana usisahau kuleta mrejesho mzee.
 
Kweli tuko kwenye UCHUMI WA MAFRAME

mpaka kambi wanazungushiaa frame za biashara

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…