Kamera za ulinzi kufungwa Kariakoo kwa gharama ya Tsh Milioni 514

Kamera za ulinzi kufungwa Kariakoo kwa gharama ya Tsh Milioni 514

Hizo pesa ni ndogo sana. Kwa Camera arobaini?

Hivi mnataka waweke camera za aina gani hapo Kariakoo? CutePanda? Ring doorbell camera?
=============

Hivi bakresa ametumia kiasi gani cha pesa kufunga cctv camera azam tv? Acheni utani.
Acheni ujinga! Hivi mnafikiri mnaongea na vilaza humu?

Tangu lini gharama ya Camera 40 ikawa milioni 514? Ni Camera zipi hizo zenye twknolojia ipi hiyo ambayo hatuifahamu yenye thamani hiyo?

Hili ni jukwaa la great thinkers. Msifikiri huku ni huko Facebook au Insta walipojaa wajinga
 
sidhani kama kupoteza uhai na maisha hata ya mtu moja tukwasababu za kiusalama kudorora, inaweza kulinganishwa na milioni 514 au hata billion gentleman.

I think ilisha tangazwa na viongozi wetu kitaifa kwamba,
there will be no discussions katika suala la usalama wa watu, makazi na biashara zao.

umoja, amani na utulivu wa waTanzania popote walipo utalindwa kwa nguvu na gharama zote bila mbambamba za kibaka au tapeli yoyote wa kisiasa :NoGodNo:
Kwa hiyo ndo muibe fedha za wananchi kwa kigezo cha usalama?

Sawa endeleeni tu kuiba. Yana mwisho.
 
ramli za kishirikina na imani potofu za mtu moja moja, haziwezi kuzuia ulinzi na usalama wa waTanzania usiimarishwe na kua wa kisasa zaidi :pedroP:
Naona weye ni muumini wa hiyo kitu kwelikweli.

Mie ni mkristo halisi, hayo mambo hata siyazingatiia hurudisha nyuma akili na kuwa zezeta.
 
Mzifunge tu na zote zikamilike tu
😄

Ova
Watajuana wanaofunga mkuu..ila

Naamini zipo gharama zingine humo kwenye TShs 40million.. Ww unafikiri huyu LodiLofa Dearing anaweza funga kwa kiasi gani?
 
Kwa hiyo ndo muibe fedha za wananchi kwa kigezo cha usalama?

Sawa endeleeni tu kuiba. Yana mwisho.
Lengo la serikali sikivu ya ccm ni kuhakikisha usalama wa uhakika kwa waTanzania wote kwa gharama yoyote.

thamani ya usalama wa uhai na maisha ya mTanaznia moja yeyote haiwezi kulinganishwa na thamani ya pesa ya kiasi au kiwango chochote. usalama wa mwanachi ni muhimu kulindwa kwa nguvu zote :NoGodNo:

hayo mengine ya dhana potofu, uelewa na ufahamu mdogo kuhusu usalama, ni mambo binafsi kwa watu wachache sana na hayana maana yoyote:NoGodNo:
 
Tupige hesabu kidogo.

Tuseme kamera zanunuliwa China kwa gharama ya 1 Kamera ni dola 1500 kwa bei ya chini.

Hivyo Kamera 40 X 1500 ni dola 60,000 sawa na shilingi milioni 155 na ushei.

Ukitaka quality zaidi yaani HDMI na iwe Dome na sio Static tuseme ni dola 2500

2500 X 40 = 100,000 sawa na Tshs 260 milioni.

Hivyo milioni 514 ni upigaji, kwani :

514-155 = 359 milioni.

au 514- 260= 254 ukiondoa gharama za vifaa inobaki ni lazima ipigwe.

Ukitoa gharama za usafirishaji, nyaya, vifaa vingine havizidi milioni 2

Inobaki ni lazima igawiwe.
 
Naona weye ni muumini wa hiyo kitu kwelikweli.

Mie ni mkristo halisi, hayo mambo hata siyazingatiia hurudisha nyuma akili na kuwa zezeta.
inawezekana ukawa ni mkristo, lakini mkristo jina na fuata upepo tu asie na imani thabiti :pedroP:
 
Umoja, amani na utulivu wa waTanzania wote Taifa katika kila kona na pembe ya nchi yetu, vitalindwa kwa nguvu na gharama yoyote bila kujali kelele au mdomo wa kibaka au tapeli yoyote wa kisiasa nchini. :NoGodNo:


Gentleman 😂
Naona umekosa cha kutetea Leo
Umeamua kuja na upande mwingine haha

Camera 40 Kwa milion 500 wow Just wow
 
Kamera moja yauzwaje?
Unaniuliza mm? Muulize huyo aliyesema kuna wizi huko. Huyo ndie aliyefanya tafiti na kugundua wizi huo. Muulizeni.

Mm binafsi hizo 40million ni pesa ndogo sana kwa Camera 40 na gharama zinazoambatana, tena za public na sidhani ni sahihi kuita huo wizi, sidhani zinatosheleza kuwaasa wananchi na vyombo vya usalama kufanya Uasi kwa sababu tu wanataka kumsimika mtu wa kwao waje watuibie maradufu ya wizi walioufanya.
 
Watajuana wanaofunga mkuu..ila

Naamini zipo gharama zingine humo kwenye TShs 40million.. Ww unafikiri huyu LodiLofa Dearing anaweza funga kwa kiasi gani?
Mitaani kwetu tulifunga ilitumika 2m na usheh tu...

Ova
 
Pamoja na bei hiyo utakuta za solar maana umeme wenyewe wasiwasi mara ukatike
Hizi hela wamechanganuaje?
Au watafungiwa wenye maduka?
Maana sidhani kama kuna watu watapata ajira kwa kuangalia uhalifu labda Polisi
. Vyovyote vile mna safari ndefu sana
 
nadhani ilifaa kua 1 billion kabisa,
kwasababu usalama wa Taifa na wananchi wake ni muhimu sana na gharama yake haipimwi kwa fedha

ni muhimu ikafahamika kwamba kwa nguvu na gharama yoyote ile usalama wa waTanzania utazingatiwa na serikali sikivu ya CCM gentleman bila mbambamba yoyote:NoGodNo:

Hahahaha
Najua kimoyo Moyo unasema kudadeki 500M? Haha
 
Gentleman 😂
Naona umekosa cha kutetea Leo
Umeamua kuja na upande mwingine haha

Camera 40 Kwa milion 500 wow Just wow
nadhani ilifaa kua zile za 1billion ambazo ni za kisasa zaidi,

kwasababu thamani ya uhai na maisha ya mtanzania moja tu haulingani na thaman ya pesa kiasi chochote kile.

ulinzi na usalama wa waTanzania katika makazi na biashara zao utaimarishwa kwa nguvu na gharama yoyote ile bila kujali kelele au midomo ya watu wachache wenye uelewa na ufahamu finyu dhidi ya usalama wa waTanzania na thamaini ya uhai wa wananchi :NoGodNo:
 
Tuichambue M514 alafu tujue zinafungwa kamera gani, watuonyeshe quotation ya hizo bidhaa. Yan kakubali
kabisa kamera million Mia tano?.
unasahau taratibu za manunuz lazim bei huenda inapanda sabab kwa uzoef wangu procedure za procurement ndio kikwazo kokubwa sana cha miradi. kakitu kadogo tu kutokana na procedure kanakula hela na hela. hapo kamera unakuta ina price, price +vat bado labour charge. supervisions ya kipind cha mradi.10% ya wazee wa kaz ni kipimo cha utu. mambo ni mengi so hio bei ni sawa
 
Pamoja na bei hiyo utakuta za solar maana umeme wenyewe wasiwasi mara ukatike
Hizi hela wamechanganuaje?
Au watafungiwa wenye maduka?
Maana sidhani kama kuna watu watapata ajira kwa kuangalia uhalifu labda Polisi
. Vyovyote vile mna safari ndefu sana
Kikubwa zifungwe tu 😄
Maana nnavyowajua jamaa
Wanaweza wakwala hela na kamera zisifungwe....

Ova
 
Pamoja na bei hiyo utakuta za solar maana umeme wenyewe wasiwasi mara ukatike
Hizi hela wamechanganuaje?
Au watafungiwa wenye maduka?
Maana sidhani kama kuna watu watapata ajira kwa kuangalia uhalifu labda Polisi
. Vyovyote vile mna safari ndefu sana
Mitaa mingi ya uhindi,kisutu, Libya Street nk wDosi wamefunga wenyewe

Ova
 
Back
Top Bottom