Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Katika kuhakikisha biashara zinafanyika saa 24, Jiji la Dar es Salaam limeingia mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unaogharimu jumla ya shilingi milioni 514 wa usimikaji wa mifumo ya kamera za ulinzi katika barabara na maeneo ya Kariakoo ambapo jumla ya kamera 40 zitakazofanya kazi kwa saa 24 zitafungwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo kwa ajili ya ufuatiliaji wa hali ya usalama na udhibiti wa matukio ya kihalifu.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema lengo la mpango huo ni kuimarisha usalama wa wanachi na wafanyabiashara na kuongeza ufanisi wa shughuli za kibiashara.
Amesema, kamera hizo hizo zitasaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu na kutoa ushahidi wa haraka inapohitajika.
My take:
Hawa watu wanaliibia sana hili Taifa na ifike wakati wenye akili kwenye vyombo vya dola waungane na Wananchi Wazalendo wachukuliwe hatua.
Baada ya Wizi mkubwa uliofanywa kwa kuongeza gharama za ujenzi wa viwanja vya michezo, leo umesainiwa mkataba kufunga Kamera 40 tu Kariakoo kwa gharama ya milioni 514.
Acha niendelee kuwaamini CHADEMA kuwa No Reform No Election. Nchi hii inaibiwa sana