Kamishina Aretas Lyimo: Wanaovaa nguo zenye picha ya Bangi kuchukuliwa hatua

Kamishina Aretas Lyimo: Wanaovaa nguo zenye picha ya Bangi kuchukuliwa hatua

Wao mbona wametia mabango ya kupambana na dawa za kulevya picha ya bibi wa mipasho ya kwenye majukwaa
 
na sie tunaovaa nguo zenye pcha ya snacks na bites,janabi anatuzoom tu.
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya nchini Aretas Lyimo amesema serikali itaanza kuwachukulia hatua za kisheria wanaovaa mavazi yenye picha ya bangi.

Lyimo amesema hayo jijini Dodoma wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya kwa mwaka 2024 ambapo amesema hatua hii inatekelezwa kama sehemu ya juhudi za kudhibiti matumizi na ushawishi wa dawa za kulevya katika jamii.

"Kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya inakataza mtu yoyote kuvaa mavazi au kuhamasisha kwa namna yoyote ili ya kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya na sheria hiyo kifungu namba 24 ukikutwa na hatia hiyo inakupeleka gerezani kwahiyo mtu yoyote anayevaa mavazi hayo tunamchukulia hatu" Aretas Lyimo - Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya

Kamishna Lyimo amesisitiza kuwa mavazi yanaweza kuwa na athari kubwa katika kuhamasisha na hivyo ni muhimu jamii iungane katika mapambano dhidi ya utumiaji wa bangi na dawa nyingine za kulevya.

Katika hatua nyingine amesema serikali imeanza kufanya mazungumzo na kupokea maoni juu ya namna ya kudhibiti matumizi ya Shisha baada ya kugundulika kuwa kuna baadhi ya watoa huduma wameanza wanachanganya shisha na dawa za kulevya ili kuvutia wateja.

Najaribu kuwaza, kama atatokea Mkuu wa nchi fulani ......; amevaa nguo yenye alama za madawa ya kulevya; kwa mfano kama bangi nk, itakuwaje kwa mujibu wa itifaki akishuka kwenye chombo cha usafiri ?
 
Siyo kila raia anajua bangi inaonekanaje hadi aitofautishe kwenye t-shirt. He can’t criminalize fashion juu ya ignorance ya mimea, yeye afocus on real dealers, not designs.
 
Kuna vitu hata kama sijui sheria hunifungi.
Umenikamata nimevaa T-shirt yenye urembo wajani.

Unanishitaki kwa kosa gani?
 
Kupata vichekesho kama hivi andika neno MSANDO kwenda Waliofunga Ving'ora wakamatwe
 
This is too much sasa loh...!!!!
Ulitaka wasemeje?

Vaa basi zenye bangi

Za jeshi mbona hamvai

Tatizo mnataka ta samia iwe nchi ya kingese kama kenya

How do you glorify bangi in public?

Kesho mtataka mvae picha za condom na punyeto, na hata mikundu iwe public…. This is stupid

Mshana ulikua very balanced

Something is wrong with you
 
Nimemshusha vyeo bro Lyimo.. Hii sio akili yake asee
 
Kwa hiyo mtu akivaa nguo yenye nembo ya HIV/AIDs ile wanaita utepe mwekundu naye achukulie anahamasisha kuambukiza huo ugonjwa?
 
Watu kama hawa ndo husababisha serikali idhalilike mahakamani. Kuvaa nguo yenye picha za mimea iwe kosa kisheria? Kamishna aweke juhudi zaidi kudili na mapapa ya unga badala ya kudili na vitu vya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom