Kamishina wa mchezo na Meneja wa uwanja hawafahamu kanuni? au walishindwa vipi kuwasiliana ili Simba wafanye mazoezi?? Kuna kitu hakipo sawa.

Matteo Vargas

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2019
Posts
803
Reaction score
1,329
Kuna mambo hayahitaji elimu ya juu kujua kwamba Kuna mambo ya ajabu ajabu yanafanyika kwenye mpira wetu. Hivi hata kama Meneja wa uwanja hana taarifa kutoka kwa kamishina wa mchezo kwa uzoefu wake wa uendeshaji wa uwanja anajua kabisa ni lazima timu ngeni itakuja kufanya mazoezi.

Kwa busara tu ya kawaida tu alishindwa vipi kumtafuta kamishina wa mchezo huo na kumuuliza mbona bado yeye kama Meneja wa uwanja hapewi au hajapewa taarifa kuhusu ujio wa timu ambayo itakuwa mgeni kuja kufanya mazoezi??

Lakini pia baada ya hiyo sintofahamu kutokea hapo uwanjani kwanini yeye kama Meneja wa uwanja hakumtafuta kamishina wa mchezo au viongozi wa TFF Ili wampe go ahead ya kuiruhusu Simba kufanya mazoezi?? Hapa Kuna kitu hakipo sawa.

Why always Simba ndio anakuwa (victim) mhanga kwenye haya mambo ya figisu figisu kwenye mechi zake??
 
Swa
Swali je simba na yanga ni wageni kwenye uwanja wa Mkapa?
 
TFF,Kamishna na Meneja mnamlaumu kwa ujinga na mazoea mliyo yaweka kwa miaka kibao na sasa yamekuwa sheria. Miaka yote Derby ya Kko Mgeni huingia uwanjani siku ya mechi akitokea kambini, huku uwanja anapewa mwenyeji.

Sasa kwa mwenye akili sababu hii culture wameiweka wao wenyewe kwa miaka mingi, wangetakiwa kwanza wampe taarifa meneja, kwamba tumebadilisha culture yetu,sasa tumeachana na mazoea tunafuata kanuni. Sasa meneja hamja mwambia na meneja kichwani mwake anajua bado mnaendelea na tamaduni zenu zile zile, hamkumpa taarifa na mmekuja mda ambao sio wa kazi ,sasa ulitegemea meneja afanye nini kama si kuwakataa.

Hata timu kutokupata nafasi ya kucheza kabla ya mechi hakuzuii kuendelea na mechi, CAF ukienda nchi za kiarabu ni kawaida ila still mechi inaendela.

Hapa wakulaumiwa ni Watani wenyewe ambao walichagua mazoea ya mechi zao na kuacha kanuni na kwa kuwa wana nguvu TFF waliwaacha na ikawa sheria na ndio maana meneja hakuwa na taarifa.
 
Hiyo culture uchwara umeitoa wapi, derby iliyopita Yanga walikagua uwanja vzr na mazoezi wakafanya
 
Mkuu umesikiliza mahojiano kati ya mtangazaji na mwenyekiti wa bodi ya ligi? Simba walienda kufanya mazoezi kwenye uwanja huo juzi. Sasa hapo ni nani anaweza kujua kama watarudi tena kufanya mazoezi katika uwanja huo siku ya Ijumaa zaidi ya hao wenyewe Simba kutoa taarifa?

Na kanuni imesema angalau mara moja kabla ya siku ya mechi, hivyo pengine wahusika wa uwanja walishaona kanuni ya msingi imeshatekelezwa.
 
Hiyo culture uchwara umeitoa wapi, derby iliyopita Yanga walikagua uwanja vzr na mazoezi wakafanya
Nitumie hiyo clip wakikagua uwanja.

Asante vibertz
Haya references nyingine,kumbuka kwenye kanuni wamesema walau mara moja.
"
Mkuu umesikiliza mahojiano kati ya mtangazaji na mwenyekiti wa bodi ya ligi? Simba walienda kufanya mazoezi kwenye uwanja huo juzi. Sasa hapo ni nani anaweza kujua kama watarudi tena kufanya mazoezi katika uwanja huo siku ya Ijumaa zaidi ya hao wenyewe Simba kutoa taarifa?

Na kanuni imesema angalau mara moja kabla ya siku ya mechi, hivyo pengine wahusika wa uwanja walishaona kanuni ya msingi imeshatekelezwa."
 
Jana simba alienda kwa mkapa gari alienda nalo halikuwa na wachezaji ni watu wakamati tu sijui wengine siwafahamu, inshort waache uoga uwanja wa mkapa unatafuta uzoefu gani timu km simba ?
Mpira unaongozwa na kanuni sio mazoea. Watu wamekosa hoja wamebaki kusema Simba ana ugeni gani na uwanja wa mkapa. Ni kanuni zinafuatwa boss
 
Huu ni uongo Derby iliyopita Yanga kama mgeni alipata fursa ya kufanya mazoezi na Deberby ya mzizima Azam kama mgeni alipata fursa ya kufanya mazoezi iweje kwa Simba iwe tofauti??
 
Hii kanuni umeilewa ukilinganisha na maelezo yako??
 
Huu ni uongo Derby iliyopita Yanga kama mgeni alipata fursa ya kufanya mazoezi na Deberby ya mzizima Azam kama mgeni alipata fursa ya kufanya mazoezi iweje kwa Simba iwe tofauti??
Nitumie hiyo clip Yanga akikagua mechi.Halafu rudi kwenye posting yangu namba 13.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…