Uchaguzi 2020 Kampeni Bahi: Dkt. Magufuli asema miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, hiyo yenyewe ndio inakuja

Uchaguzi 2020 Kampeni Bahi: Dkt. Magufuli asema miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, hiyo yenyewe ndio inakuja

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mgombea urais wa JMT kupitia CCM, Dr. Magufuli leo anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Bahi.

Watu ni wengi sana na mkutano huu utarushwa mubashara na TBC na Channel Ten.

========

3:00 Asubuhi: Maombi ya kufungua mkutano kutoka kwa viongozi wa dini

Sikutegemea kama ningekuta watu wengi hapa Bahi, leo nina mikutano mingi sana, ningependa sana nikae hapa kwa masaa mengi lakini nimeona maendeleo mliyonayo, miaka mitano iliyopita nilipita nikawaomba kura kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kweli - JPM

Asante Watu wa Bahi kwa kunikaribisha nafahamu hapa Bahi kuna wakulima wazuri, wafugaji tutatua kero zenu zote, zaidi ya tozo 114 zimefutwa ili wakulima mnufaike, kwa miaka 5 tutaendeleza pale tulipoishia, tutaondoa kabisa tatizo la maji hapa -JPM

Tumejenga Hospitali ya Wilaya hapa Bahi kwa Tsh. Bil 1.8 ambayo ujenzi wake umefikia 95%, tumejenga vituo vya afya 3 kwa Tsh. Bil 1.5, nataka hii Hospitali ya Wilaya ikamilike haraka ili Wananchi waanze kutibiwa hapa, ndio maana nawaomba mnipe kura nikamalizie palipobaki -JPM

Ukiwa na tochi ni lazima uwe na betri zote zinazowaka, ukichanganya na gunzi tochi haitawaka. Naomba mniletee betri, mbunge mtarajiwa ndugu Keneth, hata sura tunafanana.

Naomba niwaahidi tutachapa kazi kubwa isiyo na mfano, hii miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, Hiyo yenyewe ndio inakuja.

1598942032533.png
 
Hivi pamoja na kufanya kampeni peke yake kwa miaka yote mitano aliyokuwa rais, bado anahitaji kampeni za nini tena?

Angewaachia vyama vingine kwa hii miezi michache nao wafanye, kwani kama hiyo miaka mitano haikumtosha, sidhani kama hii miezi itamtosha.

Vipi wasanii watakuwepo au, maana watu wanajitokeza kuwasikiliza wasanii na siyo sera za CCM.
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa
 
Watumishi wa umma waliotia Nia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kupita CCM na kukatwa mishahara Yao yote ya mwezi July na August 2020 hawataruhusiwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa. Ila wataruhusiwa kupiga kura tu. TL mungu akupe nguvu
 
Yani tayari saa tatu kasoro hii watu ni wengi sana!!? Tupia basi 2pichapicha, wenye wivu wajinyonge
 
Back
Top Bottom