Uchaguzi 2020 Kampeni Bahi: Dkt. Magufuli asema miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, hiyo yenyewe ndio inakuja

Uchaguzi 2020 Kampeni Bahi: Dkt. Magufuli asema miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, hiyo yenyewe ndio inakuja

yani anamaanisha jinsi wafanyakazi hawajapandishiwa mishahara kwa miaka 5 hiyo ilikua ni trailer round ya pili watapunguziwa kabisa hiyo mishahara hadi wakome kuichagua CCM.
 
IMG_20200901_122546.jpg
IMG_20200901_122546.jpg
IMG_20200901_122643.jpg
 
Watumishi halmashauri hiyo ya Bahi wameshurutishwa kuhudhuria mkutano huo wa mgombea urais wa ccm kwa kusaini karatasi za mahudhurio ili kuongeza wingi wa wahudhuriaji.
 
Mgombea urais wa JMT kupitia CCM, Dr. Magufuli leo anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Bahi.

Watu ni wengi sana na mkutano huu utarushwa mubashara na TBC na Channel Ten.

========

3:00 Asubuhi: Maombi ya kufungua mkutano kutoka kwa viongozi wa dini

Sikutegemea kama ningekuta watu wengi hapa Bahi, leo nina mikutano mingi sana, ningependa sana nikae hapa kwa masaa mengi lakini nimeona maendeleo mliyonayo, miaka mitano iliyopita nilipita nikawaomba kura kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kweli - JPM

Asante Watu wa Bahi kwa kunikaribisha nafahamu hapa Bahi kuna wakulima wazuri, wafugaji tutatua kero zenu zote, zaidi ya tozo 114 zimefutwa ili wakulima mnufaike, kwa miaka 5 tutaendeleza pale tulipoishia, tutaondoa kabisa tatizo la maji hapa -JPM

Tumejenga Hospitali ya Wilaya hapa Bahi kwa Tsh. Bil 1.8 ambayo ujenzi wake umefikia 95%, tumejenga vituo vya afya 3 kwa Tsh. Bil 1.5, nataka hii Hospitali ya Wilaya ikamilike haraka ili Wananchi waanze kutibiwa hapa, ndio maana nawaomba mnipe kura nikamalizie palipobaki -JPM

Ukiwa na tochi ni lazima uwe na betri zote zinazowaka, ukichanganya na gunzi tochi haitawaka. Naomba mniletee betri, mbunge mtarajiwa ndugu Keneth, hata sura tunafanana.

Naomba niwaahidi tutachapa kazi kubwa isiyo na mfano, hii miaka mitano ilikuwa ni onjaonja, Hiyo yenyewe ndio inakuja.

kiboko ya mabeberu
 
Back
Top Bottom