Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa


Anatekeleza amri halali ya waxiri Mkuu aliyepinda aloitoa bungeni wakati ndugai akiwa naibu spika.Wapigwe tu hakuna NAMBA na akirudia apigwe tu!
 
Sheria ichukue mkondo wake haiwezekani mtu akajichukulia sheria mkononi namna hiyo
Hili linatutia doa wana CCM na tusikubali chama kuchafuliwa na watu wenye tamaa ya madaraka kama Ndugai
 

The beginning of an end. Maskini ccm wamelewa pombe ya madaraka.
 
Mbona wanachapana sana kipindi hiki??
 
Alifikiri bado yuko bungeni akiwafokea na kuwakemea akina Lisu.
Unyenyekevu kwa hawa ma ccm ni ndoto. Duu huyu akikatwa huku ataibukia wapi kwa staili hii ya kutumia mgongo?

Kwa mtindo huo wa kupiga watu hakuna atakayempokea hata CCM wameshamchoka
Nadhani ipo haja ya kukinusuru chama kwa jimbo la Kongwa kwa kumuengua huyu jamaa vinginevyo wananchi watafanya maamuzi magumu
 
Msibishe jambo ambalo hata wewe pia huna uhakika nalo,
ndugu Joseph E Chilongani ni amepigwa kweli, na mpaka sasa kalazwa hosptali ya wilaya kongwa, na hali yake bado si nzuri,

kwa hali hii Ndugai inabidi achukuliwe hatua kali za kisheria kwa kitendo hicho, na asitake kuchukua madaraka kwa ubabe, kwanza wanakongwa wengi tumemchoka na ccm yake,
 
Habari wanaJF

Hali si hali kwa baadhi ya vigogo wa ccm kutetea ubunge wao hali inayosababisha haya yote tunayoyashuhudia

Nirudi kwenye mada
Kutoka jimbo la kongwa katika kampeni ya uchaguzi wa kuteuliwa kupeperusha bendera ya ccm ngazi ya ubunge uchaguzi mkuu,
mh. Job Ndugai amemshambulia kwa fimbo hadi kupoteza fahamu mgombea mwenzake katika nafasi hiyo bw. Joseph Chilangane hali hiyo ilitokea baada ya mgombea mwingine aliyekuwa mtumishi wa halmashauri akijinadi akisema nipeni nafasi hii nikaondoe ufisadi uliokithiri pale halmashauri unaoingozwa na mbunge atakayemaliza muda wake hapo october 20 Mh. Job ndugai.

Akijibu tuhuma hizo mh. Job Ndugai alisema yeye ndo mwenye uwezo tu wa kuondoa ufisadi huo na huyo anaesema atamaliza ufisadi halmashauri alikuwa mfanyakazi hapo alishindwaje kumali??

Akiwa anazungumza aligundua mgombea mwenzake bw. Joseph Chilangane anamrecord ndipo alipomgeukia na kumshambulia kwa fimbo hadi kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Kongwa na kupata matibabu.


Upepo umezidi kumbadilikia mh.Job Ndugai hatua inayoonesha kupigwa chini kura za maoni maana amekuwa akizomewa kila anapopita na kufanya mkutano


Job Ndugai+Steven Wassira (Tyson)
 
CCM wana kazi mwaka uu wanaanza kuuana wenyewe. Huko Arumeru Sioi kapigana na mgombea mwenziwe John D.
 
Hivi ni kwa nini vitendo vya uvunjifu wa amani vitokee,kwani ni lazima uwe mtawala au kiongozi siku zote.Je nitakuwa sahihi kusema viongozi tulio nao wanaona ni wao tu lazima waongoze.Mh.Rais ajaye nikuombe utuletee sura mpya TOTALLY katika serkali yako,piga chini kabisa wa sasa hivi.
 
Hivi ukichokwa na wananchi hujijui? Kitendo cha kuzomewa tu kilitodha kumfanya ajiweke pembeni.. watu wana uchu wa madaraka mpaka wanageuka wanyama.. hawatufai!!!
 
Kuna msemo unaosema "nguruwe wakiingia shambani wakala na kushiba huanza kupigana bila kukumbuka kwamba shamba lina mwenyewe" Sasa wabunge wa chama tawala wamesahau kwamba nchi hii wenye nayo ni wapiga kura waliowachagua
badala yake wao wanajifanya ni wamiliki wa nchi hii.

Tujiulize hivi kweli huyu anayemjeruhi mwenzie anapigania kutumikia watanzania kweli au tumbo lake?
Hawa ndio waliotuiletea katiba pendekezwa na Sheria mpya ya mafuta na gesi wakijinadi kwamba wao ni
wazalendo baada ya wapinzani kususa michakato na kutoka.sasa watanzania tujionee wenyewe na kufanya hukumu stahiki.
 
Huyu Ndugai anapiga kampeni za kibabe
Ni vema wakamuengua mapema kwa vitendo vyake hivi vya kuhatarisha amani kwenye mikutano ya kampeni
 
Simpendi kweli ndugai nafurahi sana jinsi anavyojichimbia kabuli lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…