Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Ha ha ha! Umenikumbusha yule mtafiti wa pale Kibasila S.S. aliyekuwa anatunza vinyesi vyake kwenye sahani na vyombo vyake vya ndani. Nadhani hapo air freshener itagonga kisiki.

Kwa hiyo wataka kuniambia nini?Maana umeniacha njia panda kama CDM walivyoniacha upenuni mwa sebule yao.........:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
Mtu kama huyo hafai, ameshapoteza sifa ya kugombea.
......... Pole sana Dr.......................
 
Mkuu kuna mwingine Savimbi(mwigulu) nae naskia anawaletea wenzake mauzauza


Huyu yeye TAKUKURU imeshaanza kumpa vidonge vyake! Sasa ile skafu ataivaa wakati akichunga au kuuza karanga! mbona analo huyo
 
Ukizingatia walivyokuwa wana hasira sasa, hata nyumbani wakae chonjo maana kile kiti cha bungeni pale juu kwenye mimbari anaona tartiiiibu kinaanza kumkimbia, masikini wee huruma!!!!
 
Aliyekuwa Naibu Speaker Job Ndugai amempiga Fimbo ya Kichwani Mtia nia Dkt Joseph Chilongani eneo la Kata ya Ugogoni na amekimbizwa Hospitali ya Kongwa
Mkuu wa Wilaya na Katibu wa CCM Kongwa wamekimbilia huko kumuona !!!!!!!


Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..
View attachment 271919

Hakika ule mnara wa babeli umeashabomoka na hiki tunachokiona ni dhambi ya dhulma na ubadhirifu vinawatafuna.
 
Du kampiga mwenzake kwa ubunge. Tuweni waangalifu sote ni watanzania, tuna haki sawa. Hakuna alie juu ya sheria. Hapo ni lazima sheria ichukuwe mkondo wake na adhabu kali itolewe iwe ni fundisho kwa wenziwe.
 
Mkuu kuna mwingine Savimbi(mwigulu) nae naskia anawaletea wenzake mauzauza

Hii yote inasababishwa na uchu wa madaraka huku wakijivuna kwamba wao ndio wao. Huko bungeni walikuwa wanaleta nyodo dhidi ya upinzani kujifanya wanakubalika sasa wanaona watadondokea pua inabidi watumie njia haramu kupata ushindi. Kama walipata hela za bwerere wakashindwa kufungua miradi itakayowapa kula basi wajue imekula kwao kwani wao hawana hati miliki ya nchi hii. Kwa mfano Mwigulu Nchemba amekuwa na kiherehere akijifanya anazijua siasa kumbe ndio mabingwa wa hila, fitina na chuki. Sasa leo ile tabia yao ya uchu wa madaraka inazidi kudhihiri.
 
  • Thanks
Reactions: G3T
ndugai alime karanga tu huko kongwa, alizania bunge la mama yake lile. Alikuwa na nyodo sana anapokalia kiti cha enzi pale mbele. Wana kongwa mnyoosheni mpuuzi huyu
 
Huyu yeye TAKUKURU imeshaanza kumpa vidonge vyake! Sasa ile skafu ataivaa wakati akichunga au kuuza karanga! mbona analo huyo

TAKUKURU awawezi kumfanya kitu.. kumbuka takukuru yenyewe ndyo ile taasisi isyokuwa na meno, na pia ni chombo dhaifu kilichotengenezwa na ccm kula kodi za wananchi bure tu. na ccmndyo walisema nchi ni yao na dola ni lao. kwa hyo nothing new hapo
 
Mtunga sheria, mwanasheria anakiuka sheria na jee yupo kwa maslahi ya nani? hovyooo kabisa Ndungai!!
 
Back
Top Bottom