Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii yote inasababishwa na uchu wa madaraka huku wakijivuna kwamba wao ndio wao. Huko bungeni walikuwa wanaleta nyodo dhidi ya upinzani kujifanya wanakubalika sasa wanaona watadondokea pua inabidi watumie njia haramu kupata ushindi. Kama walipata hela za bwerere wakashindwa kufungua miradi itakayowapa kula basi wajue imekula kwao kwani wao hawana hati miliki ya nchi hii. Kwa mfano Mwigulu Nchemba amekuwa na kiherehere akijifanya anazijua siasa kumbe ndio mabingwa wa hila, fitina na chuki. Sasa leo ile tabia yao ya uchu wa madaraka inazidi kudhihiri.
Watu waongo sana, hv ukipigwa na gogo usitoke ngeu...? Acheni kuwa kama mabinti .. sema alimtishia labda, ktk kuamua ndio mkutano ukavunjika...!!! Midume mingine kama mijike tu...!!!
Yaani upigwe na gogo..? Unajua gogo ww..? Yaani hawa wagogo ni shida, watu waongo waongo sana.... gogo unajua ukubwa wake..?
Mbona wanachapana sana kipindi hiki??
Mkuu kuna mwingine Savimbi(mwigulu) nae naskia anawaletea wenzake mauzauza
hahahah huyu ngoja kwanza takukuru wamnyooshe...sisiem hawajui karma z bytch..
Hakuna video tuona huo mtama uliozimisha kama ni sawa na ule wa Kalokola?
hahahah nimeshaisikia ulishawahi kusoma kile kitabu cha things fall apart...hahah kakirudie naona wameanza kuanikana wenyewe kwa wenyewe...hii hatari mkuu hadi lowasaa kasema sisiem si ya baba angu kimenuka hahahaah tutarajie mengi mie kadi yao narudisha...nishachafukwaa SIMBA45Hahahaha u made my day mkuu.. umepata clip ya mark mwandosya lakini(Magufuli ajawai kuwa mwenyekiti mkoa,wilaya,kijiji,mtaa,kata,ata tawi leo ndyo aje kuwa mwenyekit wa ccm taifa?!!! by mark mwandosya clip)
Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM
Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.
Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.
Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.
Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.
Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.
Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..