Tulishuhudia kampeni za uchaguzi wa 2015 Lowassa akizunguka na timu nzima ya viongozi wakuu wa CHADEMA na karibu wabunge wote kila alipokuwa anakwenda kufanya kampeni.
Mwaka huu ni tofauti kidogo, tunaona kila Kanda ikijitegemea inatumia ratiba yake siyo kupangiwa na Makao Makuu, ndio maana ni nadra sana kumuona Mkiti wa chama Mh. Mbowe wala Katibu mkuu akiambatana na mgombea urais Tundu Lissu.
Kila mgombea ubunge anafanya kampeni kwenye jimbo lake na anajaza watu kama kawaida. Tumeona kampeni za Salim Mwalimu, John Heche, Sugu, Ester Bulaya, na wengine zikifanya vizuri bila kutegemea ujio wa mgombea urais ili wajaze watu, tofauti na wagombea ubunge wa CCM wanaosubiri ratiba ya Magufuli.
Hii imewafanya wagombea kujiamini kufikisha ujumbe hadi vijijini kwa wakati na haraka zaidi na pengine imejenga imani kwa wapiga kura kulinda kura kwenye maeneo yao, kwa sababu wanakuwa ni wapigakura wa maeneo hayo tofauti na kampeni za CCM zinazotembea na wasanii kibao na watu wasio wenyeji wa maeneo hayo.