Uchaguzi 2020 Kampeni za uchaguzi huu zimetufundisha mengi kuhusu CCM, hata wakishinda uchaguzi kwa hila siku zao madarakani si nyingi

Uchaguzi 2020 Kampeni za uchaguzi huu zimetufundisha mengi kuhusu CCM, hata wakishinda uchaguzi kwa hila siku zao madarakani si nyingi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
CCM hawawezi siasa za ushindani, Wanachojua ni kutawala kwa mabavu. Kama CCM wangekua ni watawala wema, wangesikiliza matakwa ya wananchi kupitia uongozi wa mashina mpaka wabunge. Kinacho wasaidia CCM ni woga wa raia.

Kampeni za CCM zilizohudhuriwa na wanafunzi na wafanya kazi wa serikali kwa lazima. Pia kutumia wasanii kujaza nyomi viwanjani. Mjitafakari.

Ni wazi kuwa CCM itatumia hila nyingi kupita uchaguzi huu. Hata mkirudi madarakani tena, mtatumia nguvu kubwa kuwatuliza wananchi wenye hasira, wasio na woga tena. Wananchi wanaweza kuamua chochote saa yeyote ile.

Hivi ni kwanini tulazimishane!
 
Haki kwao imekuwa kitu adimu sana. Wanatulazimisha kuwa tunawapenda.

Uchaguzi ulio huru wa haki wala wenye kuaminika haupo.

1. Tutajihimu vituoni.
2. Hakuna kura hadi tujiridhishe kuwa mawakala wetu wapo kamili gado.
3. Tutapiga kura.
4. Tukimaliza kupiga kura hatuondoki.
5. Matokeo mtatutangazia vituoni.

Walizoea kupiga? Sawa. Karibuni. JKNIA mlipenda twende?

Basi JKNIA kwa hili ilikuwa cha mtoto.
 
Oooh Iam laughing and making loud noise

Tutashinda ccm

ccm tutashinda

Haya yote tutayatekeleza kuanzia 2021

Hata sisi tumejifunza kitu kuwa upendo ni moyoni mwa watu ,Hivyo kuanzia 2021 tutajitahidi kuingia mioyoni
 
CCM hawawezi siasa za ushindani, wanachojua ni kutawala kwa mabavu. Kama CCM wangekua ni watawala wema, wangesikiliza matakwa ya wananchi kupitia uongozi wa mashina mpaka wabunge. Kinacho wasaidia CCM ni woga wa raia...
Leo nimesikia mawakala wao wamepewa maelekezo kuwa wakiona Ccm wamezidiwa kura waanzishe fujo vituoni alafu polisi wataingilia kati kwa kuwatoa watu na hapo ndo Ccm wataingiza kura zao zilizochakachuliwa. Chadema tujiandae na kuchukua tahadhari
 
Yule mental case anadai kuwa akichaguliwa kuwa Rais ataongeza mishahara ya wafanyakazi,yaani hakumbuki kuwa hata mwaka 2015 aliahidi pia![emoji1787]Halafu alisikia Tundu Lissu akinadi sera yao ya bima ya afya kwa kila mtu na yeye akaidandia kama zuzu vile wakati kwenye ilani yao hata haipo![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yule mental case anadai kuwa akichaguliwa kuwa Rais ataongeza mishahara ya wafanyakazi,yaani hakumbuki kuwa hata mwaka 2015 aliahidi pia![emoji1787]Halafu alisikia Tundu Lissu akinadi sera yao ya bima ya afya kwa kila mtu na yeye akaidandia kama zuzu wakati kwenye ilani yao hata haipo![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mzee Kingugwe aliona mbali sana, Magufuli ni mtekelezaji wa mipango ya boss lakini si mwanasiasa.
 
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, kura za madiwani pamoja na kura za Wabunge na Rais baada ya kujumlishwa na kuandikwa katika fomu za matokeo, wasimamizi walizipeleka katani ili ziunganishwe na kupata matokeo ya jumla kwa kata husika.

Baada ya hapo, nakala halisi za matokeo hayo zilipelekwa jimboni ili kuunganishwa na kupata jumla kwa jimbo huku nakala zingine wakipewa mawakala.

Ikumbukwe hapa ilikuwa ni rahisi kudhibiti ikiwa kutatokea nyongeza ya VITUO HEWA vya kupigia kura.

LAKINI MWAKA 2020;

Baada ya kura kuhesabiwa na kupata matokeo ya kituo husika,ni matokeo ya MADIWANI tu yatakayounganishwa katani lakini matokeo ya WABUNGE NA RAISI kwa kila kituo, HAYATAUNGANISHWA KATANI badala yake yatapelekwa jimboni kuunganishwa.

IMG_20201026_193517.jpg



TATIZO LINAWEZA KUTOKEA:

Tatizo hili linaweza kuwa kuongeza vituo hewa endapo mawakala hawatakuwa na orodha ya vituo vyote vya jimbo na ikiwa hawatakuwa makini wakati wa kujumlisha kura.

VYAMA VYOTE VYA SIASA, CHUKUA TAHADHARI.
 
Mzee Kingugwe aliona mbali sana, Magufuli ni mtekelezaji wa mipango ya boss lakini si mwanasiasa.
Yaani ukimfuatilia majukwaani ni kama mtu mwenye matatizo ya akili.Anaweza kwenda Mbeya akasema maendeleo hayana vyama halafu akienda Manyara(Kama alivyofanya wiki hii) anawaambia wananchi kuwa awamu iliyopita sijaleta barabara hapa kwa sababu mlichagua mbunge wa upinzani.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ni mental case!
 
Nilicho jifunza ni kuwa Watanzania,japo sii wote ila waliokuwa na maslahi ya moja lisa moja ama walio shurutishwa katika mazingira fulani fulani wamekuwa na hisia zilizo fichika ndani kwa ndani kiasi kwamba nilianza kujiuliza maswali mengi sana.

kwanini Watanzania wengi wamekuwa hawapo tayari kuusema ukweli au kusimamia haki zao za msingi zisizotimizwa, hata wakati fulani nikajiuliza kwanini unafiki umeongezeka miongoni Mwa raia.

Ila yote ya yote yanatokana na mapito waliyo ya pitia katika kipindi cha hivi karibuni. Ila sasa nawaelewa kikamilifu. Asanteni wote.
 

Kama ni ushindi basi utakuwa ni ushindi haramu ambao unaweza kuhusisha umwagaji mkubwa sana wa damu ambao unaweza kusababisha vifo vingi. Hilo likitokea Watanzania tunaojitambua na Jumuiya ya Kimataifa tutamshinikiza huyo anayejiita MWENDAWAZIMU kwa mauaji ya kutisha aliyoyafanya hastahili kubaki madarakani. Serikali ya maridhiano itastahili kuundwa ambayo itasimamia upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi.
CCM hawawezi siasa za ushindani, wanachojua ni kutawala kwa mabavu. Kama CCM wangekua ni watawala wema, wangesikiliza matakwa ya wananchi kupitia uongozi wa mashina mpaka wabunge. Kinacho wasaidia CCM ni woga wa raia...
 
Kama ni ushindi basi utakuwa ni ushindi haramu ambao unaweza kuhusiana na umwagaji mkubwa sana wa damu ambao unaweza kusababisha vifo vingi. Hilo likitokea Watanzania tunaojitambua na jumuiya ya Kimataifa tutamshinikiza huyo anayejiita MWENDAWAZIMU kwa mauaji ya kutisha aliyoyafanya hastahili kubaki madarakani. Serikali ya maridhiano itastahili kuundwa ambayo itasimamia upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi.
Ninakumbuka Mbowe aliwahi kuomba maridhiano. Wakati ule wenye mamlaka walimdharau, watayajutia yale maneno.
 
Acheni kujidanganya, hakuna Mwananchi anayeweza kuamua chochote, Mapinduzi yote Dunaini yana Viongozi nyuma yake, Wanananchi kama Wananchi hawajawahi kufanya Mapinduzi popote pale tangia Binadamu aanze kuishi Dunia hii, na chadema &Co. wanapenda kufanya Mapinduzi lkn hawana huo uwezo, kama wangekuwa nao wangeshautumia siku nyingi sana, ...
 
Back
Top Bottom