BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kampuni hizo ni pamoja na Mulla Pride Ltd, iliyopigwa faini ya Tsh. 50,404,970. Taasisi hii inamiliki 'App' za kutoa huduma za Mikopo za FairCash na KeCredit, imebainika kutumia Taarifa Binafsi za Wateja ili kudai Madeni .
Pia, kuna Klabu ya Starehe ya Casa Vera Lounge ambayo imekutwa na Kosa la Kuchapisha mtandaoni bila Idhini Picha za mteja wakati akipata burudani ndani ya Baa hiyo. Italipa faini ya Tsh. 31,344,267.
Nyingine ni Taasisi ya Elimu ya Roma iliyoko Uthiru, Nairobi ambayo imebainika kuchapisha mtandaoni bila idhini za Wazazi/Walezi, picha za Watoto. Italipa faini ya Tsh. 77,089,955.
Wakati hayo yakitokea Nchini Kenya, ni mambo yanafanyika hapa Nchini na umetambua yanakiuka Haki ya Faragha?