Kampuni Forex Trade Saccotz Ltd ni halali?

Kampuni Forex Trade Saccotz Ltd ni halali?

Attachments

  • Screenshot_20231209-061548.png
    Screenshot_20231209-061548.png
    102.9 KB · Views: 22
Wana affiliate program, red flag hii

4% kwa saa? ukiweka hiyo 500$(1.2M) unakuja kupata 980$(2.4M) baada ya siku moja, na hiyo ni basic plan😂 shtuka
1702123654701.png
 
Hivi tatizo hasa linakuwa ni nini? Ujinga, umasikini, kurogwa, au? Maana mtu anaweza akaanzisha scheme ya utapeli na anapata watu wengi tu...hao watu akili zao huwa ziko wapi?
 
Huu mkeka wao unatamanisha sana boss wangu
Mkuu,

Umeelewa mpango wao?

Twende mahesabu mepesi;

Tuseme umewekeza kiasi kidogo kabisa cha $500, ambayo kwa muktadha huo unapata 4% kwa kila saa.

Kwa mahesabu mepesi ni 0.04×$500=$20.

Yaani kwa kila saa unapata dollar 20. Ambayo kwa masaa 24 yao inakuwa;
$20×24=$480.

Yaani kusema kwamba ndani ya masaa 24 umepata faida ya dollar 480.

Ndiyo kusema ndani ya masaa 24 una jumla ya kiasi cha dollar 980 ($500+$480=$980). Ndani ya siku moja umepata kiasi sawa na mtaji ulioweka?

HAIWEZEKANI Mkuu.

Kimbia zaidi ya Bolt. Usiangalie nyuma.

Unapigwa.
 
Hii kampuni ya forex trade wamenipa mchanganua wao wa jinsi ninavyoweza kupiga hela nikitrade nao, lakini nahitaji mwongozo wenu, na hasa, waliowahi kufanya nao biashara.


Watanzania wa Pumbavu sanq
 
Tumewachoka kumamina zenu kila siku mnapigwa tu, marufuku kuleta tena nyuzi za kijinga humu.
 
Back
Top Bottom