samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,223
Mkuu usipojiamini huwezi fanya kitu kamwe.
Reli ya TAZARA ilijengwa na wachina mwaka 1971-1975, in FOUR YEARS.
Waarekani waliita bamboo railway ili kuwakatisha tamaa, kwa kjiamini wachina walijenga narei hiyo ipo mpaka leo , kiteknolojiabado inadunda.
Tatizo kubwa watanzania wengi wanabaki kuwa wa vitabuni na si practical.
Watu waajiita maconsultant wa engineering lakini hata kukoroga na kulitofauisha zege la class 15, 20 ,25 au 30 hawawezi practically na hawajui watumie njia ipi kufikia huko.
Sasa hebu niambie hapa kilicho kigumu kjenga barabara ya lami kutua Ndege na jingo la kupokelea abiria ni lipi haswa?
Kujenga kiwanja cha ndege kuna procidure zake na viwango zake zaidi ya kushindilia na kumwaga rami, inaweza kuwa rahisi kwa kufikiri hata kufanya lakini mwisho wa siku kuna ndege itatua ikiwa na weight yake na itakimbia kwa speed yake ili iruke au itue. Ubora wa kazi na usalama mwisho wa siku ndio kitu muhimu na kuvipata hivi lazima ujiridhishe kwa uliyempa kazi ndio maana hapo kinakuja kigezo cha Uzoefu na Exposure..
Sijakataa watu kupewa kazi ila mashaka yangu ni ubora na usalama wa kazi husika, huwezi kuanzisha leo kampuni ya Ujenzi kwa sababu unajiamini basi kesho tukakupa kazi ya 500bil..
Mchina alipokuja kujenga reli ya Tazara tayari alishajenga reli kama hizo nyingi sana huko china kwa mikono, USA walimcheke kwa sababu kiteknolojia walikuwa mbele maili nyingi kuliko yeye.