Kampuni inayomiliki Tigo yabadili jina, sasa ni Honora Tanzania

Mwekezaji mpya hupewa likizo ya Kodi Kwa miaka mitano.Hivyo Kila ukibadilisha jina unapata tax exemption ya miaka hiyo mitano.
Sio kubadilisha jina ni kuuza majority of shares za umiliki wa kampuni kwa mtu mwingine ambaye automatically ndiye atabadiri jina. Ila ukibadili jina halafu majority of shares zikawa bado mikononi mwako utalipishwa kodi stahiki after five years.

Pia kusajiri Kampuni kwenye nchi nyingi ni moja ya njia ya kukwepa kodi kama ilivyofanyika ila sehemu zote mbili wanakuwa hawajavunja sheria
 
Hukumbuki before then ilikuwa buzz?
Hio ni brand tu ila Milicom ipo toka 1993.

Mwaka 1993 iliitwa Mobitel wakati huo ikiwa kama Joint Venture na Serikali, baadae ikanunua kampuni nyengine na kuitwa Buzz, baadae ikanunua Hisa za Serikali na kuitwa Tigo, wakati wote huu ni Hio Hio MIC kampuni mama haijawahi kubadilika.

Hizo stori zenu mnazoongea hapa ni za vijiweni tu mnadanganya watu.

Acha mipasho kwenye mijadala kinachouzwa ni hisa na ndio hubadili kila kitu buzz, mobitel, tigo zimetokana na kuuzwa kwa hisa
Kampuni iko kama jumba tupu, wanahisa ndio uhai wa kampuni na ndio wanaofanya biashara.. Wakipata faida ama hasara ni ya kwao sio kampuni
 
Kitu pekee kinachonishangaza kwanini kampuni nyingi hata kama zinamilikiwa na watz lazima wakazifungulie nje
Ni mbinu mojawapo ya kukwepa kodi bila kuvunja sheria za nchi hasa wakitumia mianya ya udhaifu wa sheria za kodi zenyewe.

Zamani mtu alikuwa anafungulia kampuni Namanyere Simbawanga halafu shughuli nyingi zinafanyika ilala Dar es salaam. Kwa kuwa Namanyere hawabanwi sana kulipa kodi kwa kuwa wako vijijini basi inawapa nafasi ya kuenjoy super normal profit. Watu wa TRA wakitaka a submit returns za hesabu yeye anapanda gari kwenda Namanyere anakowajibika. Anacholipa ilala ni leseni ya biashara na tozo zinginezo za halmashauri ila sio corporate tax.

Basi kwa mfano huo inaendana kabisa na mtu akisajiri kampuni Mauritius ambako anahisi kodi kule iko chini kutokana na sera za nchi husika kuhusu namna ya kuvutia wawekezaji. Mfanyabiashara yeyote lazima ajue mbinu salama za kukwepa kodi bila kuvunja sheria za nchi
 
Acha mipasho kwenye mijadala kinachouzwa ni hisa na ndio hubadili kila kitu buzz, mobitel, tigo zimetokana na kuuzwa kwa hisa
Kampuni iko kama jumba tupu, wanahisa ndio uhai wa kampuni na ndio wanaofanya biashara.. Wakipata faida ama hasara ni ya kwao sio kampuni
Wewe ndo unaongea mambo usiyoyajua nimekuekea link angalau usome, badala ya kusoma uelewe unarudi kuja kujiaibisha tena.

Mwaka 1993 ilipoanzishwa Hio Venture Mic (hao wa Luxembourg) walikua na Hisa asilimia 72.3 na Serikali chini ya TPTC wakawa na asilimia 27.7

Mwaka 2006 MIC wakanunua Hisa za Serikali na Kurebrand Buzz kwenda Tigo.

Mobitel, Tigo, Buzz hii ni brand name, Mic ndio jina la kampuni. So toka 1993 mpaka Leo kampuni ni ile ile Mic haijabadilika, sasa hivi hao Honora ndio wamenunua na kubadili kampuni mama kwa mara ya kwanza.

Una Argue wewe hapa ni kama Azam kubadili Soda ya Apolina na kuiita Apple punch useme kwamba Wamebadilisha jina ili wakwepe kodi.
 
Umejiuliza kwanini kuna hiyo biashara ya hisa? Unadhani ni kwa ajili ya kujifurahisha?
 
Acha mipasho kwenye mijadala kinachouzwa ni hisa na ndio hubadili kila kitu buzz, mobitel, tigo zimetokana na kuuzwa kwa hisa
Kampuni iko kama jumba tupu, wanahisa ndio uhai wa kampuni na ndio wanaofanya biashara.. Wakipata faida ama hasara ni ya kwao sio kampuni
Wewe ni mweupe kichwani.
 
Back
Top Bottom