Kampuni inayomiliki Tigo yabadili jina, sasa ni Honora Tanzania

Japo nilikuwa simkubali wala kumpenda JPM ila kwenye hili nimemkumbuka Bwana Yule.
 
Ndio ushangae..bunge badala ya kubadili hizi sheria wako busy kubadili sheria ili DP World achukue bandari milele...
Ujinga umekujaa [emoji1787][emoji1787]

Hivi unawezaje kuzikataa trilioni 26 kila fiscal year katikati mwa dunia ya soko huria?!!

Unaye mwekezaji atakayetupa trilioni 80?!!!
 
[emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Conspiracy theories....

Ukwepe kodi?!!

Kweli miluzi mingi humpoteza mbwa....
Hujui sheria za uwekezaji na misamaha ya kodi. Wanakupa miaka 3 uanze biashara, baada ya hapo unaanza kulipa kodi. Ukifika mwaka wa tatu unasema bashara imenishinda nauza shares zangu zote. Unamuuzia dada yako/kaka yako, (danganya toto) mchezo unaanza upya.....
 
Ukwepaji wa kodi unaofanyika unasababishwa na tiharei wenyewe baadhi au wengi wa watumishi wao kupendelea rushwa zaidi.

mfano Kodi inatakiwa kulipiwa milioni 60, maafisa wanachezesha mchongo wanapewa milioni 10 jamaa analipa kodi milioni 20. hiii ndio ipo sana nadhani wengi mnalijua hili, ndio nama natamani tuwe na sheria ya kunyonga,

Tunanyonga anaetoa rushwa, tunanyonga anaepokea rushwa na tunanyonga anaetumia vibaya kodi za wananchi lazima nchi itasonga mbele.
 
Kwani si kampuni imenunuliwa na Rostam na wawekezaji wenzake? Mbona sisi Watanzania tunapenda kulalamika hivi? Kampuni zinauzwa na kununuliwa kila siku huo ndo uwekezaji wenyewe.
 
Eka ushahidi kwamba mzawa akinunua kampuni anapewa msamaha wa kodi.
 
Hizo ni kodi za Level ndogo, Makampuni ya simu yanaingiza Kodi kupitia system kama Mpesa, Tigopesa na Vifurushi, Kodi zao ni mabilioni.

Vodacom Wamelipa kodi Bilioni 29 nusu mwaka,
 
Ulaya kuna Monaco, America kuna Panama etc.
 
Sasa unajua MIC tanzania ina miaka mingapi TANZANIA ikiendesha shughuri zake
Ina zaidi ya miaka 30
Na ilichukua kijiti toka kwa MOBITEL TANZANIA baada kununua hisa nyingi toka kwa serikali na kuwa reading SHAREHOLDER then mwaka 2006 ikabadili brand name toka BUZZ na KADIPOA kuja TIGO

Elewa ineuza SHARE zake za MIC TANZANIA kwa kampuni ya HONORA 7bu kuu wamekuwa wakipata HASARA kwa miaka 3 mfululIzo
HONORA anaendeleza BIASHARA alipoishia MIC tanzania

Hiyo SHERIA unayosema inaapply kwa MWEKEZAJI mpya anayeanza kufanya BIASHARA mpya kabisa na kampuni mpya KABISA sio kununua HISA kwa kampuni
Ambapo MWEKEZAJI akishindwa ndani ya hiyo miaka 3 anafunga BIASHARA anasepa HASARA inakuwa kwa serikali yako ya TANZANIA yeye kashajipigia ela anakuja tena mwaka mwingine kwa mgongo mwingine wa kuwekeza anapiga tena ela anasema amepata hasara ndani ya miaka 3 anayeya tena mchezo ndo huo huo

Sasa Hii iliyofnyika Ni kama ni MIC TANZANIA nao iliinunua ZANTEL TANZANIA BARA
Na sasa HONORA amenunua MIC tanzania

Tena ukumbuke ukinunua KAMPUNI unanunua mpk na madeni yote pia hivyo MIC tanzania kama ana madeni HONORA atalipa yote
 
Aliyekwambia ukibadilisha jina la biashara wakwepa kodi nani?
Huwezi windup biashara bila kumalizana na TRA
Nilihamishia biashara yangu kwa mtu mwingine. Nikaenda TRA kubadili umiliki. Meneja akasema bora umekuja. Maana ungesema unafunga tungekosa mapato. Nafikiri kunatechnicalities za kikodi ambazo zinacheza kwenye kuuza, kufunga au kuhamisha umiliki wa biashara.
 
Vyote vinawezekana, ........
 
Nimeusoma ila hamna kilichoandikwa jinsi watu wanavyoiibia serikali kwa kubadilisha jina !!

Kuna vitu viwili hapa ambavyo hatupaswi kuchanganya, kubadilisha jina au Kampuni kuuzwa/kufa nakuanzishwa nyingine. Mimi nnachojua nikwamba ukibadilisha jina taarifa za Tin na VRN zitaendelea kubaki zilezile na deni liko palepale... na hata ikiizwa maana unauziwa assets na liabilities zote za kampuni iliyouzwa... ni kazi ya serikali kufuatilia na kulipwa chao na sio kukusanya 30% mfukoni alafu wananwasamee kwa madai alieyekua anadaiwa alifilisika na hana mali zozote za kutaifisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…