Wachina inapo kuja swala la Ushirikiano wako juu sana. Viwanda vyao vingi na hata kampuni zinazo kuja kuwekeza huku na kupewa tenda za kujenga Barabara na Majumba ni muunganiko wa watu wengi walikaa na kuunda.
Unakuta kampuni au kiwanda kimeanzishwa na watu 100 au hata 500 na kila mmoja ana majukumu yake. Katika watu 500 kuna Ma injinia humo, kuna watu wa masoko kuna kila aina ya mtalamu na wote wana piga kazi.
Unakuuta malengo yao ni kuwa na viwanda hata 500 ambapo baada hata ya miaka 30 Wote watakuwa na viwanda.
Hufanya hivyo ili kuunganisha nguvu/mitaji yao na kuwa na nguvu moja.
KIBONGOBONGO
Hilo bongo haliwezekani kila mtu anataka aonekane yeye, watu wanawaza kudhurumiana tu kuibiana na kadhalika.
Unakuta mtu ana kampuni ya ujenzi wa Barabara muda wote wa uhai wake ataishia kujenga barabara za vijijini tu make hana mtaji wa kushika tenda kubwa na pia hataki kuungana na wenzake na wenzake pia hatawaki kuungana.
Ni vigumu sana kushindsna na Wachina wenye nguvu kubwa sana na walio ungana. Ndo maana wameshika tenda Africa nzima za kujenga majumba na Barabara.