Kampuni ya Amsons Group yenye makao makuu yake nchini Tanzania, inaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya hatua ya juu ya kuinunua kampuni ya Oryx Energies katika dili linalokadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 250 (Zaidi ya shilingi bilioni 650 za Kitanzania), kwa mujibu wa taarifa kutoka Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Amsons Group, Edha NahdiWataalamu wa sekta hiyo wanadai kuwa ununuzi huo unaohusisha biashara ya mafuta ya Oryx, vilainishi, na kampuni ya International Petroleum Reserves Limited (Tiper) huenda tayari umekamilika, ingawa hakuna kampuni yoyote iliyothibitisha taarifa hizo hadharani.
Tiper inamilikiwa kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 kati ya Serikali ya Tanzania, kupitia Msajili wa Hazina, na kampuni ya Oryx Energies SA yenye makao makuu yake Geneva.
Tiper uliyopo katika Eneo la Viwanda la Kigamboni jijini Dar es Salaam, inaendesha moja ya vituo vikubwa zaidi vya kuhifadhia mafuta na petroli katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hapo awali kituo hiki kiliundwa kama kiwanda cha kusafishia mafuta, lakini sasa kinatumika kama bohari kuu ya matanki ya kuhifadhia bidhaa za petroli kwa ajili ya kampuni mbalimbali za uuzaji wa mafuta.
Kama ununuzi huu utakamilika, utaiweka Amsons Group katika nafasi ya kuwa msambazaji mkubwa zaidi wa nishati Afrika Mashariki na mtoa huduma ya uhifadhi mafuta, hivyo kutanua kwa kiasi kikubwa ushawishi wake katika soko la mafuta la kikanda na gesi ya kupikia (LPG).
Taarifa hizi za ununuzi zinakuja wakati soko la gesi ya kupikia (LPG) nchini Tanzania likishuhudia ukuaji wa kasi wakati ambao pia kuna ongezeko la mahitaji ya nishati safi ya kupikia.
Kihistoria, Oryx imekuwa ikitawala soko la LPG nchini Tanzania, ambapo hapo awali ilikuwa ikishikilia zaidi ya asilimia 46 ya soko. Hata hivyo, ushindani mkubwa, hasa kutoka kwa Taifa Gas, umelibadilisha soko hilo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa sasa Oryx inashikilia asilimia 35.2 ya soko la LPG, ingawa baadhi ya watu wa ndani ya sekta hiyo wanaamini takwimu hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.
Matumizi ya kitaifa ya gesi ya kupikia (LPG) yalipanda kwa asilimia 38 hadi kufikia zaidi ya tani za kimeta (metric tonnes) 403,600 ndani ya mwaka mmoja, ongezeko linalochochewa kwa kiasi kikubwa na kampeni ya serikali ya nishati safi ya kupikia na mikakati ya kutoa ruzuku ya mitungi ya gesi inayolenga kupunguza utegemezi wa mkaa, kuni, na mabaki ya mazao.
Mkakati wa serikali wa nishati safi ya kupikia unalenga kuongeza idadi ya kaya zinazotumia nishati safi kwa ajili ya kupikia kutoka takriban asilimia saba mwaka 2024 hadi kufikia zaidi ya asilimia 80 ifikapo mwaka 2034. Makadirio ya sasa yanaonesha viwango vya ufikiaji vipo karibu asilimia 24.
Katika hatua inayolenga kuleta utengamano wa ugavi na kushusha gharama kwa walaji, hivi karibuni EWURA iliingiza gesi ya kupikia (LPG) katika mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement system).
Tanzania inazidi kujiweka katika nafasi ya kimkakati kama kituo kikuu cha usambazaji wa gesi ya kupikia (LPG Hub) kwa ajili ya Afrika Mashariki na Kati, huku kampuni kubwa za nishati zikiwekeza kwa nguvu katika vituo vya mapokezi na miundombinu ya uhifadhi jijini Dar es Salaam na Tanga.
Credit: The Citizen
Mkurugenzi Mkuu wa Amsons Group, Edha Nahdi
Tiper uliyopo katika Eneo la Viwanda la Kigamboni jijini Dar es Salaam, inaendesha moja ya vituo vikubwa zaidi vya kuhifadhia mafuta na petroli katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hapo awali kituo hiki kiliundwa kama kiwanda cha kusafishia mafuta, lakini sasa kinatumika kama bohari kuu ya matanki ya kuhifadhia bidhaa za petroli kwa ajili ya kampuni mbalimbali za uuzaji wa mafuta.
Kama ununuzi huu utakamilika, utaiweka Amsons Group katika nafasi ya kuwa msambazaji mkubwa zaidi wa nishati Afrika Mashariki na mtoa huduma ya uhifadhi mafuta, hivyo kutanua kwa kiasi kikubwa ushawishi wake katika soko la mafuta la kikanda na gesi ya kupikia (LPG).
Wachambuzi wanasema dili hilo litaipa Amsons fursa ya kutumia miundombinu mikubwa ya kuhifadhia mafuta ya Oryx, viwanda vya kuchanganya vilainishi, na mtandao mpana wa vituo vya mafuta katika kanda yote, jambo litakalozidi kuimarisha nafasi yake katika sekta ya nishati.Taarifa hizi za ununuzi zinakuja wakati soko la gesi ya kupikia (LPG) nchini Tanzania likishuhudia ukuaji wa kasi wakati ambao pia kuna ongezeko la mahitaji ya nishati safi ya kupikia.