Mimi ninachojua kuna wabongo&wahuni ambao ndio huwashinikiza hao majambazi wa ubeberuni wakamate mali za nchi kwa manufaa ya hawa wabongo wahuni wachache na hao mabeberu majambazi.
Hiz issues ziliopoa sana, mbn zimeibuka baada ya kumsoma huyu madam prezdent mood yake na upole wake?
Anyway lipen maden ya watu na muwadake hao wabongo wachache wanaolinafikia hili taifa kwa manufaa yao
Inaelekea uelewa wako wa Biashara za kimataifa na uwekezaji, na mikataba ya kimataifa ya uwekezaji kati ya Nchi na Nchi au baina ya makundi ya Nchi ni mdogo sana! Lakini si kosa lako, maana inawezekana hujaenda shule kiasi Cha kutosha kuelewa Haya mambo.
Si rahisi kukusomesha hapa nafasi na muda havitoshi; ila kama unaweza Google, jaribu kusoma Bileteral and Multilateral Investment Treaties. Majadiliani ya biashara na uwekezaji Duniani Huwa ni magumu sana na huwa yanachukua muda mrefu sana. (Mfano angalia Uruguay Round of negotiations au angalia ya hapa kwetu 'EU-EAC free trade and investments negotiations' ambayo kwa miaka takriban 10 hakuna makubaliano. Ni kwasababu Haya mambo yanahusu uwekezaji na Kodi baina ya Nchi na Makampuni binafsi. Yanahusu Mali!!
Na hii mikataba inayoingiwa ni kwasababu Duniani Kuna hatari nyingi za kupoteza Mali (Wealth, not only Money)Miaka ya baada ya Vita ya pili ya Dunia, hasa miaka ya 1950-1980 kuliibuka mapinduzi na Madikteta wengi Duniani; hatari ya Dikteta mmoja kuamka asubuhi na kusema 'kuanzia Leo nimetaifisha hiki au kile' iliongezeka! Nchi ilibidi ziunde makubaliano ya kimataifa ya kisheria ya kulinda uwekezaji dhidi ya hatari ya Madikteta, au Vita, au Machafuko ya kisiasa. Uruguay round ni maarufu sana kwenye hili eneo. Ndio maana Kuna WTO, UNCTAD, IATA, nk. Mengine ni ya Nchi na Mengine ni ya Industry! Na Nchi zilijiunga kwa hiyari, bila kulazimishwa, kwasababu ilikuwa ndio njia ya kuaminiwa na Nchi nyingine, na Makampuni ya kimataifa: kwamba wote tutafuata tulichokubaliana, hatutakuwa wakurupukaji na kufanya mambo ya ajabu yasiyo ya kistaarabu! Makampuni yakienda kukopa Mabilioni mabenki makubwa Duniani wanaangalia: Hawa wanenda kuwekeza North Korea au Sweden? Kama North Korea wanakutolea nje; kwani Dikteta wa North Korea anaweza kufanya ujuha siku yoyote pesa zikapotea zote!
Kwa hiyo hakuna mchawi wala wahuni, ni mambo yetu tuu! Nafasi haitoshi, lakini tafuta kitabu kinaitwa 'Introduction to International Trade and Investments' na kingine kinaitwa "Introduction to International Business'. Tahadhari: vitabu hivi vina kurasa karibu 500 Kila kimoja, kwa hiyo usiwe mvivu kusoma. Hata Mwaka wa kwanza chuo Kikuu hawakisomi chote, wanapewa chapters zile muhimu zaidi. Hata hivyo, hakikisha unasoma Chapter ya kwanza 'Introduction' kwasababu itakupa muongozo.mzuri wa kuelewa mambo kabla hujachagua chapters nyingine unazozipenda zaidi, hasa zile zinazoongelea mikataba ya kimataifa ya uwekezaji.
Karibu!