Kampuni ya Australia iliyofutiwa leseni yatishia kukamata ndege ya Tanzania

Wenye akili waliliona hili mapeeeeeema Sana !! Wapumbavu hawajielewi!! Mliambiwa huwezi vunja mikataba halali uliokwisha sainiwa!?! Wakasema wapinzani wanapinga Kila kitu !!;haya Sasa twende kaziiiiii
Hao walio sign ndo majizi yenyewe
 
hopeless and stress, The Sun always heat the surface. believe me... there is something called Miracle.
 
Huo ni mchongo wa watu sampuli ya Nimrod Mkono, yanauza kesi na kula 10% kwenye fidia.., hii nchi hatujawahi kushinda kesi
 
Eti ‘Tanzania took my asset’ , kwani ukipewa leseni na ukakiuka masharti ya leseni kinachofuata ni nini kama sio kunyang’anywa?? Kwanini hata wasimpeleke Kibatala kwenye hizo kesi?
 
angepeleka wanasheria kwenda kushindana kwa hoja na hatimaye ndege yetu kukombolewa kama alivyofanya kipindi hicho.lakini huyu wa sasa kwa kuwa ni dhaifu atakimbilia kulipa wakati mkataba wenyewe haukuwa na faida kwa nchi ispokuwa kwa mabeberu.
 
Umetoa somo zuri sana Kwa wale wachangiaji wenye mihemko na hawajui lolote kuhusu biashara na mikataba. Jifunzeni mambo na siyo unachangia mada Kwa kujaza punda. Hongera sana Kwa maelezo Yako.
 
Eti ‘Tanzania took my asset’ , kwani ukipewa leseni na ukakiuka masharti ya leseni kinachofuata ni nini kama sio kunyang’anywa?? Kwanini hata wasimpeleke Kibatala kwenye hizo kesi?
Sio umahiri wa mwanasheria; swala ni je, taratibu zilizopo kwenye mikataba zilifuatwa! ? Yaani wengi hapa wangejua Haya makampuni yanavyohangaika huko kwao kupata mtaji, na jinsi wanavyohangaika huku kwetu kwenda porini kufanya utafiti na kutafuta madini(exploration) wasinge comment kirahisi hivi!

Hii kampuni wapo huko porini Nachingwea tangu mwaka 2007. Wametoboa mashimo kwa mamia ardhini wakitafuta madini. Sampo wamehangaika Nazo mpaka wamefika mahali wameona madini. Haya mambo yote yana taratibu zake na deadline zake zilizowekwa na Serikali. Ghafla tu Mwaka 2017 Serikali hiyo hiyo inawanyang'anya bila kufuata mikataba iliyopo. Bila kujali kuwa wametumia zaidi ya Bil 120 miaka yoote hiyo!! Wakishtaki kwenye koti za kimataifa ambazo tumejiunga kama Nchi Ili kuvutia uwekezaji, tunaanza kuongea hovyo: ooh mabeberu, wahuni, wasaliti!!! Hata waTanzania wenzetu wakionya, wakitahadharisha, wakitoa maoni Yao tunawaona ni wasaliti wanaowasaidia mabeberu!!!
 
Jiulize, hicho kitalu cha madini nani anakimiliki kwa sasa? Serikali? Kama ni serikali kwanini hawamrudishii na JPM keshaondoka..., tafakari kwanza
 
Zimeibuka lini? Usijitoe ufahamu mzee walikamata south na Canada huko enzi za Magu
Tena kama ameshahu, wakati wa Magu lilikamatwa mpaka jengo la Tanzania huko Washington, wakawahi kulipa deni kinya kimya. Yakaisha.

Dawa ya madeni ni kulipa tu.
 
Serikali ilivirudisha vitalu vyote na kuvitangaza upya kwa wawekezaji wapya!!
Huyo mwekezaji mpya ni nani?, fuatilia, utakuta ni huyo huyo anaetushtaki ila kwa kutumia jina jipya, hii ni michezo tu tunachezewa.., wewe unaweza kwenda kupora gari halafu umpe tu mtu mwingine, hivi hivi tu? For no reason?!
 
Wakili ni lazima aajiriwe kuifanya hiyo kazi, hajiamulii tu kisa ni wakili. Atamuwakilisha nani? Serikali iliyofujwa haishughuliki, wananchi hawajitambui.
Kaka serikali haina wanasheria wake?
 
Kaka serikali haina wanasheria wake?
Inao chini ya mwanasheria mkuu wa Serikali. Ila wataingia pua wakati wanajua hawashindi. Nina imani wanajadiliana chini kwa chini, kwani ni aibu!
 
Huyo mwekezaji mpya ni nani?, fuatilia, utakuta ni huyo huyo anaetushtaki ila kwa kutumia jina jipya, hii ni michezo tu tunachezewa.., wewe unaweza kwenda kupora gari halafu umpe tu mtu mwingine, hivi hivi tu? For no reason?!
Surprise surprise!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…