Kampuni ya Deepal kutoka China wamezindua mpinzani wa Toyota Prado, Tesla Cybertruck na Tesla Model S.

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Ni vita na mapinduzi zaidi kutoka China yanaendelea katika sekta ya magari.

Deepal wanekuja na hybrid na EV tatu ambazo zimeletwa mahususi kupambana na SUV, offroad trucks na Executive Sedans.

Deepal G318

Hii ni REEV off-road SUV inayokuja na four au two wheel drive, ikiwa na engine ya 1.5L turbo, battery la 18 kWh au 35kWh LFP.

Battery linakupeleka kilometa 174 tu, ila ukiwa full charge na full tank litakupelea hadi kilometa 1000.

Hii gari inakupa power ya 248 au 424 horsepower kutegemea na version utakayonunua.

Deepal E07

Hii inakuja na option mbili, either EV full au REEV, na kwa muonekano ina slopping rear kama ya Tesla Cybertruck.

Kwa upande wa EV, utachagua single au dual motors, ikija na battery la 90 kWh inayokupa 650 km.

REEV ya 007 inakuja na 1.5L turbo engine na motor mbili na 39 kWh battery, itakayokupa 230 km in EV model na 1100 km in hybrid mode.

Deepal L07

Hii Electric Sedan (lift back sedan) nayo inakuja na EV au REEV.

Hii sio model mpya ila ni updated version zamani ilikua SL03 ila sasa kuanzia September wameintroduce kama L07.

REEV inashare na mwenzie E07 truck.
 
Bei Gani Hilo kama Prado!
 
Watanganyika bado tungaling'ang'ana na rav 4 masawe sijui prado mchaga mara vitara Kimario. Halafu sijui kwanini haya magari kuu kuu yamepewa sana majina ya wachaga, au ndo wa kwanza kuyamiliki nchini? Anyway, Serikali iangalie maswala ya Tozo na miundombinu ya hizi gari tuanze kumiliki hizi EV. Gari zuri mno.
 
Pradonni tested and proven kwa ground. Huyu mchina lazima atleast iwe tested 10 yrs kwa mazingira ya kwetu au australia.
Ila 1.5 kwa hiyo engine ni attractive package, fuel efficiency imezingatiwa zaidi
 
Ukiniambia nichague Kati ya hii E07 na cyber truck ya Tesla nitachukua hiyo ya mchina fasta sanaaa
Hizo gari zikishaingia TANZANIA nahisi itakuwa mwisho wa mjapan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…