Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje

Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje

Sidhani kama shida ni corona, wao wamesema mradi una haribu mazingira.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata nyumbani kwako watoto wakidai uwanunulie mpira wakati una madeni ya kulipia kodi ya nyumba
huwa hatusemi mambo ya kodi,bali tunasema mpira si muhimu kwa wakati huu,lakini kama jana
walimuona mwenye nyumba anakudai,anaelewa kwamba umemjibu kiutu uzima.
 
Huko Chato naona Betri inaweza kupiga shoti
Yaani ule mradi ambao ndio ilikuwa karata ya kampeni nao ndio huo Corona nayo inatafuna uchumi kila kukicha

Mbuga za wanyama hazina mtalii hata wa dawa

Mahoteli yamefungwa huku TRA bado wanagonga milango ili wapewe chao

Majirani wametususa na kutufungia mipaka

Wauguzi huko hospitali wanapukutika kwa ukosefu wa PPE

Halafu guess what!...order inatoka kwamba Mrema aende kuchukua mabulungutu ya fedha za walipakodi ili akafanye mkutano wa kumsifu Tausi
 
Hata nyumbani kwako watoto wakidai uwanunulie mpira wakati una madeni ya kulipia kodi ya nyumba
huwa hatusemi mambo ya kodi,bali tunasema mpira si muhimu kwa wakati huu,lakini kama jana
walimuona mwenye nyumba anakudai,wanaelewa
Point yako ni ipi hasa? , maana umeeka mafumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni habari mbaya kwa siku nyengine baada ya Sweden kusitisha ku fund kampuni ya Egypt, ambayo ndio walikua constructor wa mradi huu.
Link hii hapa.
ElSewedy Electric Co - Council on Ethics

Sent using Jamii Forums mobile app
"Tuna Rais wa jabu sana haijapata kutokea" -Tundu Lissu. Haya ndiyo matokeo ya ukaidi wa wa Magufuli. Anajidai ana maono kumbe ZERO tupu kichwani. JKN mwenyewe aliyebuni huo mradi hakutekeleza, Marais waliomfuata watatu hawakutekeleza, yeye anaamua kwa akili zake ndogo kuingia kichwa kichwa.

"The reserve is also one of the last remaining large-scale wilderness areas in Africa and considered of extraordinary importance for the preservation of biodiversity. The hydroelectric power plant will cause widespread and irreversible damage to the world heritage site’s outstanding universal values. Mitigating measures would have little impact on this outcome."

Yaani hili wanaliona wazungu walio nje, kweli Watanzania wote Milioni 60 tuliopo leo hatulioni?
 
Huko Chato naona Betri inaweza kupiga shoti
Yaani ule mradi ambao ndio ilikuwa karata ya kampeni nao ndio huo Corona nayo inatafuna uchumi kila kukicha

Mbuga za wanyama hazina mtalii hata wa dawa

Mahoteli yamefungwa huku TRA bado wanagonga milango ili wapewe chao

Majirani wametususa na kutufungia mipaka

Wauguzi huko hospitali wanapukutika kwa ukosefu wa PPE

Halafu guess what!...order inatoka kwamba Mrema aende kuchukua mabulungutu ya fedha za walipakodi ili akafanye mkutano wa kumsifu Tausi
Hahahhahahahahhahahaha, unajua huyu tausi Kazi anayoweza ni kutumia pisto na SMG kusaka watu, hasira zake huishia hapo hapo Mkuu atahangaika kukutafuta nakuambia huyu mtu ameliangamiza taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Description
Norges Bank / Noregs Bank is the central bank of Norway. Apart from having traditional central bank responsibilities such as financial stability and price stability, it manages The Government Pension Fund of Norway, a stabilization fund that may be the world's largest sovereign wealth fund.
 
Kama ni kweli, itakuwa ni laana ya CCM inachowafanyia wananchi wake.
 
Nimesoma Wizara imetenga kwenye bajeti zaidi ya 60% kukamilisha huo ujenzi

Sioni mradi ukiathirikia
Yaani hiyo 60% iliyotengwa ni mwaka 2020/21 na utazidi kutengwa kila mwaka. Rest assured Tanzania kwanza haina uwezo wa kufund miradi mikubwa kama hii kwa makusanyo ya ndani. Uchumi wa Tanzania unasinyaa mwaka hadi mwaka toka Magufuli amekuja madarakani. Alipokea nchi wakati growth rate ilikuwa 7% na uchumi umekuwa unakuwa kila mwaka mfululizo kuanzia mwaka 2004. Lakini sasa uchumi unakuwa kwa 4,2%, sekta binafsi ni Magufuli mwenyewe anaipiga vita (Yusuf Manji, Mo Dewji, Ali Mufuruki (RIP), Salum Shamte (RIP), Peter Zakaria, etc, wawekezanji wa nje wanapata harassment ya kutisha (Halotel, Vodacom), mtaji mpya hauji nchini toka aje Dangote mwaka 2014, wananchi wanzidi kuwa maskini, biashara zisizo rasmi nazo zinabanwa na TRA.

Ni ndoto STIGLERS' Gorge Electric Power kukamilika mwaka 2023 kama walivyokuwa wanasema. Magufuli atafikisha miaka 10 (kama atashinda uchaguzi) na mradi utakuwa haujafika hata 35%. Sintoshangaa atakayekuja kmbadili Magufuli hata kama atatoka CCM ku-abandon mradi wa umeme wa Stiglers for good kama Magufuli mwenyewe alivyo abandon umeme wa gas au bandari ya Bagamoyo kwa maneno ya kejeli na ufedhuli kwa mtangulizi wake JK.
 
Back
Top Bottom