Tetesi: Kampuni ya Indiana Mining imesema haitasita kukamata ndege za Tanzania kama haitalipwa madai yao

Tetesi: Kampuni ya Indiana Mining imesema haitasita kukamata ndege za Tanzania kama haitalipwa madai yao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

Tulifika huko kutokana na Sera za awamu ya 5

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

..hapa walaumiwe Prof.Kabudi aliyekuwa waziri wa sheria, na Prof.Kilangi aliyekuwa mwanasheria mkuu.

..hao ndio waliokuwa washauri wakuu wa ktk mikataba na masuala ya sheria ktk serikali ya awamu ya 5.

Hata kuundwa kwa taasisi iliyokuwa inaongozwa na huyo aliyeongeza bei ya ndege ya CARGO, ulikuwa ni ushauri wao kwa jiwe ili kukwepa kukamatwa kwa hizo ndege kama zingekuwa na umiliki wa ATCL!
Sasa hizi ndege kwa wakati huu zinamilikiwa na Serikali hivyo wadai wa ATCL hawawezi kuzikamata theoretically !!! Lakini Serikali yenyewe ina kesi za madai na makampuni iliyoingia nao mikataba ambayo baadae ilikuja kuivunja hivyo wanaweza kukamata ndege hizo kama dhamana mpaka hapo watakapolipwa!!
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Umeuliza maswali ya msingi, na kutoa ushauri mzuri, lakini usitegemee hayo kutokea.

Hata mimi nina hamu ya kujua ni kesi ngapi nchi yetu imeshitakiwa huko nje; ngapi tumeshinda na ngapi tumeshindwa.

Ni watu/mashirika ya wapi haya ambayo tumepata usumbufu mkubwa nayo kiasi hiki, na sababu zake ni nini hasa?
Hawa ni watawala wetu wa huko nyuma, sasa wanatuweka ndani ya mstari wao tena?

Hii siyo serikali inayowajibika kwa wananchi; ni wananchi ndio wanaopashwa kusikiliza na kukubali yanayosemwa na serikali.
 
Inakuaje madai hewa na kesi imetajwa bwashee?
Lakini hii pia si inaweza kuwa njia nzuri ya upigaji kati ya wabia waliopo hapa na hao wenye kesi zao?
Akina Acacia si walikuwa na wakala wao hapa hapa; na hata ndani ya serikali yenyewe?

Hao wanaotengeneza na kupitisha mikataba mibovu wao hawana njaa?

Nchi hii tulipofikia sasa uzalendo ni neno haramu.
 
Chanzo cha haya matatizo ni uSiri unaofanywa na Serikali wanapoingia mikataba hii na sisi wananchi tunapotaka tuambiwe hiyo mikataba wanayosaini inasemaje , tunaambiwa kuna vipengele kwenye hiyo mikataba vinavyokataza mikataba kuwekwa wazi!!! Lakini mikataba hiyo inapoleta matatizo, mizigo yote tunatupiwa wananchi ingawa tuliambiwa ni mikataba ya siri!!! Na ndio kama hivyo sasa Serikali inatakiwa ilipe mabillioni ya shilling au ndege zitakamatwa na sisi walipa kodi ndio tunatakiwa kubeba hilo zigo!! Hii ni haramu.
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

EeeenHeeeee Heeeee! On a lighter note:

Nimepata wazo na ni wazo zuri.

Kumbe CEO wa Kampuni hii ni mama fulani?

Sasa tukiishiwa mavitu kama ndege, kwa nini tusitumie raslimali watu zetu katika maswala kama haya.

Tukimweka mtu kama the Babtisti kuwa mbadala wa ndege yetu, huyo mama hawezi kukubali?

Sijamwona jukwaani leo, au tayari yupo njiani kwenda kusawazisha mambo huko?
 
Thread Ya Namna Hii Ccm Hupita Na Magenge Yao Ila Hawasemi Kibwagizo Chetu Kuwa Anaupiga Mwingi, Anaifungua Tanzania

Mikataba Ni Mwiba Kwa Nchi Hawa Watia Saini Wanapumbazwa Na Nini Mpaka Sisi Tuwe Mwakuliwa Siku Zote, Fungu La Kukosa.
Mlimani City Watu Walikuja Na Laki Moja Wakavuna Cash Ndefu Tena Chuo Kikuu Kwenye Wasomi Tele Wakitumbua Macho
 
Back
Top Bottom