Tetesi: Kampuni ya Indiana Mining imesema haitasita kukamata ndege za Tanzania kama haitalipwa madai yao

Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Sio tetesi tena ni confirmed

Hii kesi ni kutokana na uamuzi wa ajabu uliofanywa na awamu ya 5 wa kufuta retention licenses zote na kisha kuwapora wawekezaji huku wakiqa wamekwishatumia mabilioni ya pesa kufanya utafiti.

Lilikuwa ni kosa la wazi kabisa. Sheria ilikuwa inazitambua retention licenses, waliomba wakapewa, halafu mtu akalala na kuamka na kisha kutangaza kuwa kuanzia leo hakuna retention licenses, na wote waliokuwa wanamiliki retention licenses hawana chao!! Ilishangaza sana.

Hii nchi wanaoididimiza ni watawala.
Wewe nawe acha ujinga, hebu fuatilia Sababu za magufuli kufanya hivyo alishasema watu wanatafiti miaka 20, lakini ujue kwamba ili mtu au watu wapone lazima apatikane mtu WA kujitolea mganga kupitia maamuzi mengi hayo mnayoyaita ya hovyo ambayo mikataba mingi ilikuwa ya kinyonyaji alishaivunja na tuanze upya.
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Hata hivyo zinajiendesha kwa hasara. Toka zimekuwepo na hata zisipokuwepo hamna unafuu wowote wa Maisha. wachukue tu. Tofauti na hapo wanufaika mnaweza kuendelea kulalamika. Hapa ndio tulipofikia Natamani sana raia wote wawaze kama mimi. Sio wanaonufaika ni wachache(viongozi fisadi) then wakichenjiwa ndio wanarudi kwa wananchi wote kuomba sapoti. Wapambane tu kama wanavyokula pesa wenyewe.
 
Wewe nawe acha ujinga, hebu fuatilia Sababu za magufuli kufanya hivyo alishasema watu wanatafiti miaka 20, lakini ujue kwamba ili mtu au watu wapone lazima apatikane mtu WA kujitolea mganga kupitia maamuzi mengi hayo mnayoyaita ya hovyo ambayo mikataba mingi ilikuwa ya kinyonyaji alishaivunja na tuanze upya.
Alikuwa mkurupukaji tuu kwani Kuna deadline ya kutafiti? Nini maana ya utafiti?
 
Ebu fuatilia Kwa kina Hiyo kampuniimeanza lini utafiti na serikali Kwa kipindi hicho chote kilipata nini na watu waliondolewa pale walipata nini ndio useme alikuwa mkurupukaji.
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Wewe pambana kwanza na bei ya vyakula, hayo ya huko juu huyawezi. Kwani hujui kila mtu atakula kwa urefu wa kamba aliyofungiwa shingoni kwake!!?, wewe kamba yako urefu wake upo hapa chini👇🏻👇🏻

Bei ya sembe??, Bei ya dagaa??, Bei ya mandondo??, ya nyanya, kitunguu, mafuta ya kula, kuni, mkaa, mchicha nk,

Hapo sijagusa bei ya gesi, nyama na mchele kwani hivyo ni vyakula vya anasa kwa sasa usisahau na huduma za afya.🤣🤣
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

ifike kipindi tuache kupokea baadhi ya wawekezaji toka baadhi ya nchi. na kwa upande wetu, viongozi wanaowapokea kwa rushwa, au wale wanaovunja mikataba kienyeji bila hata kusikiliza wanasheria, wapewe wanachostahili.
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Serikali iacha biashara bali iingie ubia wa 49/51% na makampuni ili:
1. Kuepukana na kadhia za kukamatwa
2. Kuleta ufanisi kibiashara
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Unapotoa taarifa kama hii inabidi uende indeed Kwa kuwa chombo cha habari kimenukuu habari amboyo Ni ya upande mmoja
Sasa ulipaswa kuandikia Kwa ufafanuzi Zaidi kwamba kampuni hii iliingia nchini lini na ilikuja Kwa lengo gani , utafiti umechukua muda gani,historia ya kampuni kwenye utafiti, sehemu husika iliyofanyiwa utafiti Kuna watu wamelipwa fidia au ilibidi waendelee kusubili utafiti uishe Kwa muda husiojulikana na Kwanini JPM aliamua kufuta leseni zote zilizokuwa zinafanya tafiti na kati ya hizo zipo ambazo zinaendelea na uzalishaji na zile za maslai zimetafuta Sababu .
Magufuli alipoamua kurekebisha Sheria za madini na utafiti ilikuwa Ni maamuzi magumu Kwa maslai ya kizazi kijacho ,mikataba ya madini ilikuwa imeifunga nchi Kwa TAARIFA TU mikataba mingi ya utafiti inatumika kuzalisha na mikataba mingi ya migodi viongozi WA mkoa na walikuwa hawakuwa na mamlaka ya KUINGIA mgodini na kuhoji.
 
Wewe nawe acha ujinga, hebu fuatilia Sababu za magufuli kufanya hivyo alishasema watu wanatafiti miaka 20, lakini ujue kwamba ili mtu au watu wapone lazima apatikane mtu WA kujitolea mganga kupitia maamuzi mengi hayo mnayoyaita ya hovyo ambayo mikataba mingi ilikuwa ya kinyonyaji alishaivunja na tuanze upya.
Wewe una tatizo kubwa. Kwa vyovyote upo kwenye jukwaa hili kimakosa. Jukwaa halina kizuizi chochote. Hata vichaa na punguani wana uwezo wa kuingia. Ndiyo maana hata ninyi wenye uelewa duni tunawavumilia. Ila kama hujaathirika sana upstairs, nakuomba:

Waache wenye akili timamu wajadili hoja iliyoletwa. Haya mambo yanazidi mbali sana uwezo wako wa akili, uelewa na upeo wako.

Ulivyo na uelewa mdogo, eti mikataba mingi ilikwishavunja, ebu itaje mikataba ya madini iliyovunjwa.

Huelewi utofauti wa mkataba na sheria.
 
Unapotoa taarifa kama hii inabidi uende indeed Kwa kuwa chombo cha habari kimenukuu habari amboyo Ni ya upande mmoja
Sasa ulipaswa kuandikia Kwa ufafanuzi Zaidi kwamba kampuni hii iliingia nchini lini na ilikuja Kwa lengo gani , utafiti umechukua muda gani,historia ya kampuni kwenye utafiti, sehemu husika iliyofanyiwa utafiti Kuna watu wamelipwa fidia au ilibidi waendelee kusubili utafiti uishe Kwa muda husiojulikana na Kwanini JPM aliamua kufuta leseni zote zilizokuwa zinafanya tafiti na kati ya hizo zipo ambazo zinaendelea na uzalishaji na zile za maslai zimetafuta Sababu .
Magufuli alipoamua kurekebisha Sheria za madini na utafiti ilikuwa Ni maamuzi magumu Kwa maslai ya kizazi kijacho ,mikataba ya madini ilikuwa imeifunga nchi Kwa TAARIFA TU mikataba mingi ya utafiti inatumika kuzalisha na mikataba mingi ya migodi viongozi WA mkoa na walikuwa hawakuwa na mamlaka ya KUINGIA mgodini na kuhoji.
Jifunze kuandika vizuri kwanza. Hata uwezo tu wa kuandika vizuri huna. Uwasilishaji wa mchango wako ni wa hovyo, nadhani ni kwa sababu ya uwezo mdogo.

Kiufupi, unatakiwa ufahamu kuwa hakuna kampuni inayofanya utafiti wa madini inaingia mkataba wowote na Serikali.

Kampuni zinazosaini MDA ni zile tu za uchimbaji madini, ambazo zina SML. Kampuni zenye ML haziingii mkataba wowote na Serikali badala yake zinahitajika kufuata Mining Act tu. Hakuna mkataba.

Baada ya kukupa elimu hii ndogo, andika upya hoja yako. Maana inaonekana kwenye eneo hili upo mtupu kabisa.
 
Ebu fuatilia Kwa kina Hiyo kampuniimeanza lini utafiti na serikali Kwa kipindi hicho chote kilipata nini na watu waliondolewa pale walipata nini ndio useme alikuwa mkurupukaji.
Wewe hujui chochote kwenye hii sekta. Ni aheri ungekaa kimya, usome michango ya wenye kuelewa ili uelimike.

Unatakiwa ufahamu kuwa kila leseni ya madini ina muda wake:

PL ni miaka 4
RL ni miaka 4

Hiyo kampuni ilikuwa na RL. Hii ni leseni ambayo hutolewa kwa kampuni ambayo ilikuwa na PL, halafu kukawa na mazingira ambayo hayaiwezeshi hiyo kampuni kuanza uchimbaji. Hivyo kipindi cha RL huwa hakuna kazi yoyote, labda kipindi hicho kampuni inatafuta mtaji wa kwenda kwenye ML au SML.

Na baada ya miaka 4, RL inakuwa imemaliza muda wake. Na muda ukiisha, mmiliki wa RL haruhusiwi kuongeza muda wa RL wala kurudi tena kwenye PL. Option aliyo nayo ni kwenda kwenye uchimbaji kwa kuomba ML au SML, kwa kutegemea ukubwa wa mtaji.

Kampuni hiyo, wakati RL zinafutwa, ilikuwa imebakiza miezi 8 tu. Kama tungekuwa na kiongozi mwenye busara, angesubiri miezi 8 tu. Hao wangekuwa na option au ya kuomba ML au SML, au kuamua kuachia. Na kama wangeomba ML au SML, ni lazima.ndani ya miezi 36, sheria inawataka waanze kujenga mgodi.

Papara na kukurupuka ndiko kumeliingiza Taifa kwenye hasara ambayo ingeweza kuepukika kiurahisi kabisa.

Baada ya hayo makosa, marehemu alipogundua kpsa walilofanya, waliamua kuwasiliana na wamiliki wote wa RL, na kuwataarifu kuwa maeneo yamerudishwa, wamiliki wa RL waombe ML au SML kwenye maeneo yale yale ambayo yalikuwa na RL, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya makampuni, ikiwemo hii ya Indiana, yaligoma kurudi, na kuamua kuendelea na madai yao mahakamani.

Kwa hiyo, marehemu mwenyewe, aligundua kuwa walikuwa wamekurupuka.
 
Nashukuru umejitaidi Kwa kiasi kuutafuta ukweli kitu ambacho Mimi nilitaka ukiweke hapa ili kunifanya msomaji aellewe Jambo lenyewe.
Katika maelezo yako umehainisha kuwa Ni kweli Kuna kampuni ziliathirika na ubadrishaji WA Sheria lakini ninachokifahamu Mimi Ni kwamba kampuni zote zilitariifiwa uwepo wa mabadiliko ya Sheria za madini,Ila baadhi ya kampuni zilitaka kuonesha umwamba kupitia Sheria za mikataba ya kibiashara ambazo tokea dunia imeumbwa waafrika ndio waathiliwa wakubwa.
Kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba magufuli alikuwa anapigania usawa Kwa Mali asili zetu,maana ndio kipindi amekuta watu wanafukuzwa kwenye maeneo yenye madini Kwa kisingizio cha uwekezaji, na wakati mwingine wizara zinatoka azarani na kusema kuwa eneo husika lilikuwa na leseni ya uchimbaji kitendo hicho alikipinga na aliamini waafrika tunaweza tukiamua.
Namalizia Kwa kukuomba ulete ya uzoefu WA kampuni,kampuni ilikabidhiwa kitalu mwaka gani,wakazi WA eneo husika walikuwa wanachimba kabla au kampuni ndio imeanzisha utafiti hakukuwa na watu hapo,tuletee data kamili za gharama halisi walizotumia tokea waanze utafiti na mwisho je?uwepo wao ulikuwa na faida gani katika Sheria za zamani na kuondoka Kwao licha ya madai Yao kutakuwa kumelisaidia nini taifa maana Sheria za sasa zinataka serikali iwe na Shea.
Ni mfano WA bwawa la mwalimu Nyerere wazungu walikataa lakini serikali ikaamua nchi ina watu wanafiki Hakuna wazalendo madini sasa yatatiroshwa TU ujinga huu ulishaisha.
 
Kw
Jifunze kuandika vizuri kwanza. Hata uwezo tu wa kuandika vizuri huna. Uwasilishaji wa mchango wako ni wa hovyo, nadhani ni kwa sababu ya uwezo mdogo.

Kiufupi, unatakiwa ufahamu kuwa hakuna kampuni inayofanya utafiti wa madini inaingia mkataba wowote na Serikali.

Kampuni zinazosaini MDA ni zile tu za uchimbaji madini, ambazo zina SML. Kampuni zenye ML haziingii mkataba wowote na Serikali badala yake zinahitajika kufuata Mining Act tu. Hakuna mkataba.

Baada ya kukupa elimu hii ndogo, andika upya hoja yako. Maana inaonekana kwenye eneo hili upo mtupu kabisa.
Kwa hiyo wewe mwenye Akili nyingi na mjuzi WA kuandika Kwa upeo wako huo WA karunguyeye unaona Ni Sahihi kampuni kufanya utafiti bila mikataba,wewe kweli kilaza haya si Ni mfano wa Yale ya wazungu kuomba makontena Kwa makontena kwenda kufanya utafiti ulaya alafu mpumbavu mmoja unashangilia tulikuwa tunaibiwa nenda kasome Sheria ya utafiti upya na ya madini upya alafu ufananishe na kauli zako.
 
Wewe una tatizo kubwa. Kwa vyovyote upo kwenye jukwaa hili kimakosa. Jukwaa halina kizuizi chochote. Hata vichaa na punguani wana uwezo wa kuingia. Ndiyo maana hata ninyi wenye uelewa duni tunawavumilia. Ila kama hujaathirika sana upstairs, nakuomba:

Waache wenye akili timamu wajadili hoja iliyoletwa. Haya mambo yanazidi mbali sana uwezo wako wa akili, uelewa na upeo wako.

Ulivyo na uelewa mdogo, eti mikataba mingi ilikwishavunja, ebu itaje mikataba ya madini iliyovunjwa.

Huelewi utofauti wa mkataba na sheria.
Wewe ndiye huna uelewa unaletaje habari ambayo imenukuliwa upande mmoja Bila uchambuzi WA kuwafahamisha watu kipi Ni kipi, usijifiche kwenye kichaka cha kunitoa kasoro wakati hoja yangu umeielewa.
 
Kwa Mujibu wa The African Report, Kampuni ya Indiana Mining ya Marekani imesema Haitasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania ikiwa Serikali itashindwa kuilipa madai Yao.

Mwenyekiti Mtendaji wa Indiana Mining Brownywn Barnes amesema atachukua hatua hiyo ikibidi ikiwa Kampuni yake Haitalipwa Award yake kwenye case aliyoshinda yenye namba "ICSID Award" Kwa kile alichodia Tanzania ilichukua Mali zake.

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Mali yetu halafu utushitaki!
 
Tulifika huko kutokana na Sera za awamu ya 5

My Take.

1.Serikali Mko wapi mje kutoa Ufafanuzi? Hizi kesi ni za nini?

2.Mbona mambo haya yanaibuka Sasa? Je Kuna watu wanafanya connection Ili wanamufaike Kwa udalali?

3.Mwisho ni Bora Serikali ikaenda Bungeni na kueleza Umma kesi zote za Nje inazodaiwa, inazodai na inazoendelea na mashauri Ili Watanzania wajue maana Sasa imekuwa too much..

Viongozi wa hovyo waisababishia nchi hasara kubwa kubwa
 
Back
Top Bottom