Hercule Poirot
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 1,718
- 1,481
Mabadiliko yoyote ya Sheria huwa na tathmini ya athari na gharama(hasi na chanya) zake kwa taifa.Hii kesi ni kutokana na uamuzi wa ajabu uliofanywa na awamu ya 5 wa kufuta retention licenses zote na kisha kuwapora wawekezaji huku wakiqa wamekwishatumia mabilioni ya pesa kufanya utafiti.
Lilikuwa ni kosa la wazi kabisa. Sheria ilikuwa inazitambua retention licenses, waliomba wakapewa, halafu mtu akalala na kuamka na kisha kutangaza kuwa kuanzia leo hakuna retention licenses, na wote waliokuwa wanamiliki retention licenses hawana chao!! Ilishangaza sana.
Hii nchi wanaoididimiza ni watawala.
Inasikitisha sana namna nchi tunavyopata hasara kwa maamuzi yetu wenyewe. Hii sijui ni fidia ya ngapi tutalipa na wanaoumia ni wananchi kutwishwa mzigo mkubwa wa kodi na tozo. Kwa kweli halikubaliki