Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Indiana Mining kutoka Australia, Bi. Bronwyn Barnes, amesema Hatasita Kukamata Ndege za Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania, ikiwa Serikali Itashindwa Kuilipa Fidia ya Dola za Marekani milioni 98.83 (Tsh bilioni 231.7) kwa hasara ya uwekezaji wao nchini.
“Tanzania ilichukua Mali zangu..nina furaha kufanya kama walichonifanyia”. - amesema Bi. Barnes.
Mnamo Julai 2017, Serikali ya Tanzania ilifanyia marekebisho Sheria ya Madini ya 2010 kwa, pamoja na mambo mengine, kufuta msingi wa kisheria wa uainishaji wa Leseni ya Uhifadhi bila uainishaji mbadala.
2018, Januari 10, Tanzania ilichapisha Kanuni za Madini (Mineral Rights) za 2018, ambazo zilifuta Leseni zote za Uhifadhi zilizotolewa kabla ya tarehe 10 Januari 2018 ambapo zilikoma kuwa na athari yoyote ya kisheria na haki zote zikahamishiwa Serikali ya Tanzania.
2019, Disemba 19, Tume ya Madini ya Tanzania ilitangaza mwaliko wa umma wa kutoa zabuni kwa ajili ya uendelezaji wa pamoja wa maeneo yaliyokuwa yakimilikiwa na leseni za uhifadhi.
Hapo awali, zabuni hiyo ilikuwa na masharti kuwa mzabuni atakayeshinda atamfidia mmiliki wa leseni wa awali gharama zake za uchunguzi (exploration costs). Sharti hili liliondolewa baadaye.
Bosi wa Indiana Mining akatoa taarifa yake:-
“Sasa ni wazi kwamba Tanzania imeondoa umiliki wa mradi kutoka kwa wawekezaji, na kwa kufanya hivyo imekiuka wajibu wake kwa wawekezaji chini ya BIT [mkataba wa uwekezaji baina ya nchi mbili] na sheria za kimataifa.”
Nimesikitishwa sana kwamba Serikali ya Tanzania imefuta leseni yetu ya kubakiza na baadaye kutangaza mradi huo kwenye tovuti yake kama unapatikana kwa wawekezaji wapya bila mashauriano.”
Malalamiko hayo yaliyofikishwa kwenye Kituo cha kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, ICSID, kampuni hiyo inadai fidia ya Dola za Marekani milioni 98.83 (Tsh bilioni 231.7) kwa hasara ya uwekezaji wao nchini (pamoja na riba hadi Julai 2022).
Kulingana na Barnes, kampuni yake hadi kufikia mwaka 2020 ilikuwa imewekeza zaidi ya AUD$60m (Tsh. Bilioni 95) katika mradi wake wa Nikeli wa Ntaka Hill huko Nachingwea.
The African Report