Wewe hujui chochote kwenye hii sekta. Ni aheri ungekaa kimya, usome michango ya wenye kuelewa ili uelimike.
Unatakiwa ufahamu kuwa kila leseni ya madini ina muda wake:
PL ni miaka 4
RL ni miaka 4
Hiyo kampuni ilikuwa na RL. Hii ni leseni ambayo hutolewa kwa kampuni ambayo ilikuwa na PL, halafu kukawa na mazingira ambayo hayaiwezeshi hiyo kampuni kuanza uchimbaji. Hivyo kipindi cha RL huwa hakuna kazi yoyote, labda kipindi hicho kampuni inatafuta mtaji wa kwenda kwenye ML au SML.
Na baada ya miaka 4, RL inakuwa imemaliza muda wake. Na muda ukiisha, mmiliki wa RL haruhusiwi kuongeza muda wa RL wala kurudi tena kwenye PL. Option aliyo nayo ni kwenda kwenye uchimbaji kwa kuomba ML au SML, kwa kutegemea ukubwa wa mtaji.
Kampuni hiyo, wakati RL zinafutwa, ilikuwa imebakiza miezi 8 tu. Kama tungekuwa na kiongozi mwenye busara, angesubiri miezi 8 tu. Hao wangekuwa na option au ya kuomba ML au SML, au kuamua kuachia. Na kama wangeomba ML au SML, ni lazima.ndani ya miezi 36, sheria inawataka waanze kujenga mgodi.
Papara na kukurupuka ndiko kumeliingiza Taifa kwenye hasara ambayo ingeweza kuepukika kiurahisi kabisa.
Baada ya hayo makosa, marehemu alipogundua kpsa walilofanya, waliamua kuwasiliana na wamiliki wote wa RL, na kuwataarifu kuwa maeneo yamerudishwa, wamiliki wa RL waombe ML au SML kwenye maeneo yale yale ambayo yalikuwa na RL, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya makampuni, ikiwemo hii ya Indiana, yaligoma kurudi, na kuamua kuendelea na madai yao mahakamani.
Kwa hiyo, marehemu mwenyewe, aligundua kuwa walikuwa wamekurupuka.