#COVID19 Kampuni ya kutengeneza chanjo za COVID-19, Moderna inatarajia kuanza majaribio ya Chanjo za UKIMWI mwezi huu

Malengo yametimia Idadi wa watu wanaotakiwa kuishi kwenye Chanjo ya Corona, Chanjo ya ukimwa ikipatikana Machine hazifanyi kazi
 
Aisee! kwahiyo unataka kuniambia kwamba hakuna kabisa hiyo side effect ya kuganda kwa damu kwenye hizi chanjo?
 
Labda iwe hutaki tu kujibu tu hilo swali, unataka tuelewe kwamba chanjo zimefanyiwa majaribio hivyo ni salama ila nikiuliza kama hilo la kuganda lilionekana kwenye majaribio unasema nje ya mjadala.
 
Aisee! kwahiyo unataka kuniambia kwamba hakuna kabisa hiyo side effect ya kuganda kwa damu kwenye hizi chanjo?

Hakuna mkuu .ukiona mtu amechanjwa kisha damu ikaganda basi imesababishwa na vitu vingine.....Kumbuka waliochwanjwa mpaka sasa ni aroun 4B.....ingekuwa chanjo inaleta blood clot means watu karibu 1B wangekuwa washakufa kwa blood clot.
 
Labda iwe hutaki tu kujibu tu hilo swali, unataka tuelewe kwamba chanjo zimefanyiwa majaribio hivyo ni salama ila nikiuliza kama hilo la kuganda lilionekana kwenye majaribio unasema nje ya mjadala.
Matokeo ya majaribio ni lazima yawe tofauti na matokeo halisi.Unapofanya majaribio mfano ya watu elfu kumi ni tofauti na unapochanja watu milioni moja.Kumbuka watu milioni moja ina watu mbalimbali ukilinganisha na watu elfu kumi.Watu milioni moja ina tabia ya watu wengi zaidi kwenye masuala ya DNA,magonjwa na kadhalika ukilinganisha na sample ya watu elfu kumi.

Hii maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa kukutana na matokeo tofauti unapochanja watu wengi ukilinganisha na unapochanja sample na hii inamaanisha kuwa kufanya majaribio haimaanishi kuwa umemaliza kazi wala majaribio siyo mwarubaini wa kubaini matatizo yote kweye chanjo.Changamoto hapa ni kwamba ni ngumu sana na haiwezekani kuweka tabia za watu wote katika sample ya majaribio.Kuna tabia ambazo ni ngumu kuzifikia katika majaribio.Mfano ni ngumu sana kuweka watu wenye kila aina ya magonjwa katika sample ya majaribio na kadhalika lakini hii haimaanishi kuwa majaribio siyo muhimu.

Majaribio hutoa picha pana ya ufaulu wa chanjo lakini siyo Mungu wala mwarubaini wa kubaini matatizo yote ya chanjo kwa sababu sample ni limited katika tabia za watu ukilinganisha na entire population.
 
itapingwa tu kwanini imechelewa ...?
Kuchelewa siyo hoja kwa sababu magonjwa yanatofautina katika ugumu wa kuyadhibiti.

Inaweza kuwa rahisi sana kupata chanjo ya ugonjwa A lakini ikawa ngumu sana kupata chanjo ya ugonjwa B kutokana na complexity ya wadudu wanaosababisha ugonjwa B.

Complexity ya wadudu wanaosababisha ebola ni tofauti kabisa na complexity ya wadudu wanaosababisha malaria.Hii ina uwezo wa kufanya chanjo ya ebola kupatikana haraka sana lakini chanjo ya malaria ikachukua miaka mingi sana kupatikana.
 
Mara Unaambiwa hata ukichanja,

* Haikuzuii kupata maambukizi mapya wala

*Haikuzuii kueneza kwa wengine.

*Unatakiwa uendelee kutumia Condom.

Halafu kuna watu watahamasisha wenzao wapeleke mabega kuchanjwa.

Wameona watu hawatumii akili zao sawasawa kupitia hii chanjo ya Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…