#COVID19 Kampuni ya kutengeneza chanjo za COVID-19, Moderna inatarajia kuanza majaribio ya Chanjo za UKIMWI mwezi huu

#COVID19 Kampuni ya kutengeneza chanjo za COVID-19, Moderna inatarajia kuanza majaribio ya Chanjo za UKIMWI mwezi huu

Malengo yametimia Idadi wa watu wanaotakiwa kuishi kwenye Chanjo ya Corona, Chanjo ya ukimwa ikipatikana Machine hazifanyi kazi
 
Pole sana mkuu ,fuatilia hiyo chanjo kwanini ilisimamishwa,kulitokea cases kadhaa kwa waliochanjwa ,wakasimamisha kuchunguza kama ni kweli chanzo ni chanjo ,wakaja kugundua chanjo haijasababisha kuganda kwa damu na W.H.O wakairuhusu iendelee...Ndio maana swali langu la awali niliuliza ushawahi kufatilia vitu vinavyosababisha blood clot? Wataalam wanasema mtu aliyechanja ana chance ndogo sana ya kupata blood clot kuliko ambaye hajachanjwa.

Kwa kukusaidia baadhi ya mambo yanayosababisha blood clot:-

1.Uvutaji wa sigara.
2.Madawa ya uzazi wa mpango
3.Mwili kuwa inactive kwa muda mrefu hasa kwa wale waliolazwa kitandani
4.Covid19
5.Obesity

Please note sio watu wenye hivyo vitu au watumiaji wa hivyo vitu watapata blood clot yaani chances ni kubwa ukiwa na hivyo vitu ila unaweza usipate.
Aisee! kwahiyo unataka kuniambia kwamba hakuna kabisa hiyo side effect ya kuganda kwa damu kwenye hizi chanjo?
 
Mkuu najali sana juu ya ni kitu gani kilitokea wakati wa majaribio lakini kwa bahati mbaya hiyo siyo mjadala wetu kwa sasa.Kwa sasa hivi mjadala wetu unahusu majaribio yalifanyika au la.

Kuna vitu viwili ambavyo nimejifunza kutoka kwako.Moja, either una nia ya kututoa kwenye reli ya mjadala wetu au mbili huenda kuna point unataka kuiunganisha na mjadala wetu lakini unashindwa kuiunganisha inavyotakiwa.

Kama kuna kitu unataka kukiunganisha katika mjadala wetu kaa chini ufikirie namna ya kukiunganisha vizuri kwenye mjadala bila kuonekana kuwa unataka ututoe kwenye reli ya mjadala.Ni wajibu wako kujenga hoja vizuri ili uonekane kuwa upo ndani ya mjadala wetu na huna nia ya kututoa kwenye reli.
Labda iwe hutaki tu kujibu tu hilo swali, unataka tuelewe kwamba chanjo zimefanyiwa majaribio hivyo ni salama ila nikiuliza kama hilo la kuganda lilionekana kwenye majaribio unasema nje ya mjadala.
 
Aisee! kwahiyo unataka kuniambia kwamba hakuna kabisa hiyo side effect ya kuganda kwa damu kwenye hizi chanjo?

Hakuna mkuu .ukiona mtu amechanjwa kisha damu ikaganda basi imesababishwa na vitu vingine.....Kumbuka waliochwanjwa mpaka sasa ni aroun 4B.....ingekuwa chanjo inaleta blood clot means watu karibu 1B wangekuwa washakufa kwa blood clot.
 
Labda iwe hutaki tu kujibu tu hilo swali, unataka tuelewe kwamba chanjo zimefanyiwa majaribio hivyo ni salama ila nikiuliza kama hilo la kuganda lilionekana kwenye majaribio unasema nje ya mjadala.
Matokeo ya majaribio ni lazima yawe tofauti na matokeo halisi.Unapofanya majaribio mfano ya watu elfu kumi ni tofauti na unapochanja watu milioni moja.Kumbuka watu milioni moja ina watu mbalimbali ukilinganisha na watu elfu kumi.Watu milioni moja ina tabia ya watu wengi zaidi kwenye masuala ya DNA,magonjwa na kadhalika ukilinganisha na sample ya watu elfu kumi.

Hii maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa kukutana na matokeo tofauti unapochanja watu wengi ukilinganisha na unapochanja sample na hii inamaanisha kuwa kufanya majaribio haimaanishi kuwa umemaliza kazi wala majaribio siyo mwarubaini wa kubaini matatizo yote kweye chanjo.Changamoto hapa ni kwamba ni ngumu sana na haiwezekani kuweka tabia za watu wote katika sample ya majaribio.Kuna tabia ambazo ni ngumu kuzifikia katika majaribio.Mfano ni ngumu sana kuweka watu wenye kila aina ya magonjwa katika sample ya majaribio na kadhalika lakini hii haimaanishi kuwa majaribio siyo muhimu.

Majaribio hutoa picha pana ya ufaulu wa chanjo lakini siyo Mungu wala mwarubaini wa kubaini matatizo yote ya chanjo kwa sababu sample ni limited katika tabia za watu ukilinganisha na entire population.
 
Aisee! basi sawa.

Ndiyo Hivyo Mkuu,Story nyingi mitandaoni za uongo ,fuatilia kutoka kwa WHO....TZ mpaka sasa tumechanjwa 106K.

VW.jpg
 
itapingwa tu kwanini imechelewa ...?
Kuchelewa siyo hoja kwa sababu magonjwa yanatofautina katika ugumu wa kuyadhibiti.

Inaweza kuwa rahisi sana kupata chanjo ya ugonjwa A lakini ikawa ngumu sana kupata chanjo ya ugonjwa B kutokana na complexity ya wadudu wanaosababisha ugonjwa B.

Complexity ya wadudu wanaosababisha ebola ni tofauti kabisa na complexity ya wadudu wanaosababisha malaria.Hii ina uwezo wa kufanya chanjo ya ebola kupatikana haraka sana lakini chanjo ya malaria ikachukua miaka mingi sana kupatikana.
 
Mara Unaambiwa hata ukichanja,

* Haikuzuii kupata maambukizi mapya wala

*Haikuzuii kueneza kwa wengine.

*Unatakiwa uendelee kutumia Condom.

Halafu kuna watu watahamasisha wenzao wapeleke mabega kuchanjwa.

Wameona watu hawatumii akili zao sawasawa kupitia hii chanjo ya Corona.
 
Back
Top Bottom